Mkate Wa Kifaransa (French Toast)
Mkate Wa Kifaransa (French Toast)
Vipimo
Mayai - 6
Maziwa- 1½ Vikombe vya chai
Vanilla/iliki- Kidogo
Mdalasini ya unga- ¼-½ Kijiko cha chai
Ganda la ndimu iliyokaruzwa - 1 kijiko cha supu
(lemon zest)
Maji ya machungwa - ¼ Kikombe cha chai
sukari - 1 Kijiko cha supu
Mkate wa slesi - 6-8
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya pamoja vipimo vyote isipokuwa mkate kwenye bakuli; weka
kando.
2. Panga mikate katika chombo kikubwa(trei) , kisha mimina ule
mchanganyiko wa mayai juu yake na iache irowanike dakika 5 hivi.
3. Weka chuma kipate moto, kisha tia siagi au/na mafuta na upange mikate
kadha kama itakavyotosha kwenye chuma cha kuchomea.
4. Iwche hadi iive na kuwa rangi ya dhahabu, kisha geuza upande wa pili
na endelea hivyo hivyo mpaka umalize mikate yote.
5.Panga katika sahani na itakuwa tayari kuliwa na shira ya matunda kama
maple syrup.