05-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyeyekevu Wake: Akikaa Na Maswahaba Kuongea Nao

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

05-Unyeyekevu Wake: Akikaa Na Maswahaba Kuongea Nao

 

www.alhidaaya.com

 

 

عن أنس بن مالك رضي الله عنه يَقُولُ إِنْ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لَيُخَالِطُنَا حَتَّى يَقُولَ لأَخٍ لِي صَغِيرٍ"‏ يَا أَبَا عُمَيْرٍ مَا فَعَلَ النُّغَيْرُ ‏"‏‏.‏

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa akichanganyika na sisi mno hadi kwamba alikuwa akimwambia mmoja kati ya aliye mdogo kwetu: ((Ee Abaa ‘Umayr, An-Nu’ayr (aina ya ndege mdogo) amefanya nini?)) [Al-Bukhaariy]

 

Na pia,

 

عَنْ أَبِي ذَرٍّ، وَأَبِي، هُرَيْرَةَ قَالاَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَجْلِسُ بَيْنَ ظَهْرَىْ أَصْحَابِهِ فَيَجِيءُ الْغَرِيبُ فَلاَ يَدْرِي أَيُّهُمْ هُوَ حَتَّى يَسْأَلَ فَطَلَبْنَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ نَجْعَلَ لَهُ مَجْلِسًا يَعْرِفُهُ الْغَرِيبُ إِذَا أَتَاهُ - قَالَ - فَبَنَيْنَا لَهُ دُكَّانًا مِنْ طِينٍ فَجَلَسَ عَلَيْهِ وَكُنَّا نَجْلِسُ بِجَنْبَتَيْهِ وَذَكَرَ نَحْوَ هَذَا الْخَبَرِ فَأَقْبَلَ رَجُلٌ فَذَكَرَ هَيْئَتَهُ حَتَّى سَلَّمَ مِنْ طَرْفِ السِّمَاطِ فَقَالَ السَّلاَمُ عَلَيْكَ يَا مُحَمَّدُ.‏ قَالَ فَرَدَّ عَلَيْهِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم.‏

 

 

Abuu Dharr na Abuu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) wamehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiketi pamoja na Maswahaba wake. Basi pindi anapokua mtu mgeni huwa hamtambui mpaka pindi anapomuulizia. Kisha tukamuomba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tumfanyie kibaraza cha kukalia ili pindi anapokuja mtu mgeni aweze kumtambua. Tukamjengea kibaraza cha udongo ili akikalie, nasi huwa tunaketi pembeni yake. Akataja maelezo kama haya kwamba mtu mmoja, na akataja muonekano wake;  (Huyo mtu mgeni) alimkabili (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akamsalimia pembeni mwa ukumbi akasema:

Assalaamu ‘alayka Yaa Muhammad.”  Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu (maamkizi yake).” [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (4698)]

 

 

Share