10-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake Aliwabashiria Masikini Jannah

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

10-Unyenyekevu Wake Aliwabashiria Masikini Jannah   

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ حَارِثَةَ بْنِ وَهْبٍ الْخُزَاعِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ:‏ "‏أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَهْلِ الْجَنَّةِ، كُلُّ ضَعِيفٍ مُتَضَاعِفٍ، لَوْ أَقْسَمَ عَلَى اللَّهِ لأَبَرَّهُ، أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَهْلِ النَّارِ كُلُّ عُتُلٍّ جَوَّاظٍ مُسْتَكْبِرٍ‏"‏‏.‏

 

Kutoka kwa Haarithah bin Wahbi Al-Khuzaa’iyy kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je, nikujulisheni watu wa Jannah? Ni kila aliye dhaifu na duni na anapochukua kiapo kwa Allaah kuwa atafanya jambo, Allaah Humtimiza kiapo chake. Je, nikujulisheni watu wa Motoni? Ni kila jeuri muonevu, mwenye kujinata na kutakabari. [Al-Bukhaariy]

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((احْتَجَّتْ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَقَالَتْ النَّارُ: فِيَّ الْجَبَّارُونَ وَالْمُتَكَبِّرُونَ. وَقَالَتْ الْجَنَّةُ: فِيَّ ضُعَفَاءُ النَّاسِ وَمَسَاكِينُهُمْ: فَقَضَى الله بَيْنَهُمَا: إِنَّكِ الْجَنَّةُ رَحْمَتِي أَرْحَمُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ.  وَإِنَّكِ النَّارُ عَذَابِي أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ.  وَلِكِلَاكُمَا عَلَيَّ مِلْؤُهَا)) رواه مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jannah na moto zilihojiana. Moto ukasema: Kwangu kunapatikana watu majabari na wenye kiburi.  Jannah ikasema: Kwangu kunapatikana watu madhaifu na masikini wao.  Allaah Akahukumu baina yao (Akisema): Wewe Jannah ni Rahma Yangu, Nitamrehemu kwa sababu yako Nimtakaye. Na wewe moto ni adhabu Yangu, Nitamwadhibu Nimtakaye kwa sababu yako, na nyote Nitawajaza)). [Muslim]

 

Na pia,

 

(Wataingia Jannah Waislamu masikini kabla ya matajiri wao kwa nusu siku ambayo ni miaka 500)). [Swahiyh At-Tirmidhiy, Al-Albaaniy]

 

Share