12-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akiwahudumia Wajakazi Na Kuwatimizia Haja Zao

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

12-Unyenyekevu Wake Akiwahudumia Wajakazi Na Kuwatimizia Haja Zao

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

عن انس بن مالك قَالَ : كَانَتِ الأَمَةُ مِنْ إِمَاءِ أَهْلِ الْمَدِينَةِ لَتَأْخُذُ بِيَدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَتَنْطَلِقُ بِهِ حَيْثُ شَاءَتْ‏.‏

Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema:  Mjakazi  katika wakaazi wa Madiynah alikuwa akikamata mkono Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kisha humpeleka atakako.” [Al-Bukhaariy]

 

Riwaayah ya Ibn Maajah imesema kuwa mpaka amtimizie haja zake:

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ إِنْ كَانَتِ الأَمَةُ مِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ لَتَأْخُذُ بِيَدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم   فَمَا يَنْزِعُ يَدَهُ مِنْ يَدِهَا حَتَّى تَذْهَبَ بِهِ حَيْثُ شَاءَتْ مِنَ الْمَدِينَةِ فِي حَاجَتِهَا ‏.‏

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba pindi Mjakazi katika wakaazi wa Madiynah akitaka kukamata mkono Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi hakuwa akikataa kuondosha mkono wake, mpaka ampeleke atakapo Madiynah ili amtimizie haja zake.” [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (3386)]

Share