16-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Unyenyekevu Wake: Akiwafundisha Maswahaba Fadhila Za Unyenyekevu Kuwa Unapandisha Daraja
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
16-Unyenyekevu Wake:
Akiwafundisha Maswahaba Fadhila Za Unyenyekevu Kuwa Unapandisha Daraja
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إلاَّ عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلاَّ رَفَعَهُ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kutoa sadaka hakupunguzi mali, Allaah Humzidishia mja ‘izzah (utukufu) kwa ajili ya kusamehe kwake. Na yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah, Allaah Aliyetukuka Atampandisha Daraja [Atamtukuza]. [Muslim]