09-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Amefariki Hali Ya Kuwa Hapakuwa Na Chakula Nyumbani Mwake Isipokuwa Chakula Duni
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
09-Zuhd Yake:
Amefariki Hali Ya Kuwa Hapakuwa Na Chakula Nyumbani Mwake Isipokuwa Chakula Duni
عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَمَا فِي بَيْتِي مِنْ شَىْءٍ يَأْكُلُهُ ذُو كَبِدٍ، إِلاَّ شَطْرُ شَعِيرٍ فِي رَفٍّ لِي، فَأَكَلْتُ مِنْهُ حَتَّى طَالَ عَلَىَّ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ.
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifariki ilhali hakuna kitu ndani ya nyumba yangu ambacho mtu aliye hai angeweza kula, isipokuwa shayiri iliyokuweko katika rafu. Kwa hivyo, nilikula hiyo kwa muda mrefu kwa kuipimia, na (baada ya kipindi kifupi) ikamalizika. [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na pia,
عَنْ عَائِشَةَ، زَوْجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَتْ لَقَدْ مَاتَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَمَا شَبِعَ مِنْ خُبْزٍ وَزَيْتٍ فِي يَوْمٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ .
‘Aaishah mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifariki hali yakuwa hakuwahi kushiba mkate na mafuta ya zaytuni mara mbili kwa siku.” [Muslim]
Na pia,
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّهَا قَالَتْ مَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم مِنْ خُبْزِ شَعِيرٍ يَوْمَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ حَتَّى قُبِضَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم .
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Familia ya Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) haikushiba mkate wa shayiri siku mbili kufuatana mpaka kufariki kwake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]