13-Swahiyh Al-Bukhaariy: Kitabu Cha 'Iyd Mbili - كتاب العيدين
كِتابُ العِيدين
13-Kitabu Cha 'Iyd Mbili
01-Mlango
باب فِي الْعِيدَيْنِ وَالتَّجَمُّلِ فِيهِ ‘Iyd Mbili Na Kujipamba Kwa Ajili Yake
|
حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، قَالَ أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، قَالَ أَخْبَرَنِي سَالِمُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُمَرَ، قَالَ أَخَذَ عُمَرُ جُبَّةً مِنْ إِسْتَبْرَقٍ تُبَاعُ فِي السُّوقِ، فَأَخَذَهَا فَأَتَى رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ ابْتَعْ هَذِهِ تَجَمَّلْ بِهَا لِلْعِيدِ وَالْوُفُودِ. فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " إِنَّمَا هَذِهِ لِبَاسُ مَنْ لاَ خَلاَقَ لَهُ ". فَلَبِثَ عُمَرُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَلْبَثَ، ثُمَّ أَرْسَلَ إِلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِجُبَّةِ دِيبَاجٍ، فَأَقْبَلَ بِهَا عُمَرُ، فَأَتَى بِهَا رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّكَ قُلْتَ " إِنَّمَا هَذِهِ لِبَاسُ مَنْ لاَ خَلاَقَ لَهُ ". وَأَرْسَلْتَ إِلَىَّ بِهَذِهِ الْجُبَّةِ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " تَبِيعُهَا أَوْ تُصِيبُ بِهَا حَاجَتَكَ ".
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Umar
’Umar alinunua joho la hariri kutoka sokoni, akampelekea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Lichukue joho hili na ujipambie joho hili wakati wa Sikukuu za ‘Iyd na wakati wawakilishi wanapokuja kukuzuru.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Vazi kama hili ni la wale wasio na sehemu ya kheri (huko Aakhirah).” Baada ya muda mrefu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimpelekea ’Umar joho la hariri lililodariziwa. ’Umar akaja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na lile joho akamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah! Ulisema kuwa nguo kama hii ni ya wale wasiokuwa na sehemu ya kheri huko Aakhirah, juu ya hivyo umeniletea mimi hili joho?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Liuze na ukidhie shida zako kwalo.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 948 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 1
|
02-Mlango
باب الْحِرَابِ وَالدَّرَقِ يَوْمَ الْعِيدِ
Maonyesho Ya Mikuki Na Ngao Wakati Wa Sikukuu Za ‘Iyd
|
حَدَّثَنَا أَحْمَدُ، قَالَ حَدَّثَنَا ابْنُ وَهْبٍ، قَالَ أَخْبَرَنَا عَمْرٌو، أَنَّ مُحَمَّدَ بْنَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ الأَسَدِيَّ، حَدَّثَهُ عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ دَخَلَ عَلَىَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَعِنْدِي جَارِيَتَانِ تُغَنِّيَانِ بِغِنَاءِ بُعَاثَ، فَاضْطَجَعَ عَلَى الْفِرَاشِ وَحَوَّلَ وَجْهَهُ، وَدَخَلَ أَبُو بَكْرٍ فَانْتَهَرَنِي وَقَالَ مِزْمَارَةُ الشَّيْطَانِ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَقْبَلَ عَلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ ـ عَلَيْهِ السَّلاَمُ ـ فَقَالَ " دَعْهُمَا " فَلَمَّا غَفَلَ غَمَزْتُهُمَا فَخَرَجَتَا. وَكَانَ يَوْمَ عِيدٍ يَلْعَبُ السُّودَانُ بِالدَّرَقِ وَالْحِرَابِ، فَإِمَّا سَأَلْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَإِمَّا قَالَ " تَشْتَهِينَ تَنْظُرِينَ ". فَقُلْتُ نَعَمْ. فَأَقَامَنِي وَرَاءَهُ خَدِّي عَلَى خَدِّهِ، وَهُوَ يَقُولُ " دُونَكُمْ يَا بَنِي أَرْفِدَةَ ". حَتَّى إِذَا مَلِلْتُ قَالَ " حَسْبُكِ ". قُلْتُ نَعَمْ. قَالَ " فَاذْهَبِي ".
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها):
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuja nyumbani kwangu wakati wasichana wawili walikuwa wakiimba nyimbo za Bu’aath (Simulizi kuhusu vita baina ya makabila mawili ya ki-Answaariy yaani Al-Khazraj na Al-‘Aws kabla ya Uislamu). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alijilaza akageuza uso wake upande mwingine. Kisha Abu Bakr akaja na akanikemea mimi akisema: “Ala za mziki za shaytwaan karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamgeukia akamwambia: “Waache hao.” Abu Bakr alipokuwa hasikii, mimi niliwapa ishara wasichana waondoke wakaenda zao nje. Ilikuwa siku ya ‘Iyd, na wale watu weusi walikuwa wakicheza na ngao na mikuki. Kwa hiyo ima mimi nilimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), au yeye aliniuliza iwapo mimi nitapenda kuangalia maonyesho ya michezo yao. Mimi nikasema: Naam! Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alinisimamisha nyuma yake, na huku shavu langu lilikuwa linaligusa shavu lake, naye akawa anasema: “Endeleeni enyi Bani Arfidah.” Hadi nikachoka. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniuliza: “Umeridhika (hiyo inakutosha?).” Nikajibu: Naam nimetosheka, naye akaniambia niondoke.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 949, 950 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 2
|
03-Mlango
باب سُنَّةِ الْعِيدَيْنِ لأَهْلِ الإِسْلاَمِ
Mapokeo Yanayohusu Jinsi Sikukuu Za ‘Iyd Zilivyoadhimishwa Na Waislamu
|
حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ أَخْبَرَنِي زُبَيْدٌ، قَالَ سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، عَنِ الْبَرَاءِ، قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَخْطُبُ فَقَالَ " إِنَّ أَوَّلَ مَا نَبْدَأُ مِنْ يَوْمِنَا هَذَا أَنْ نُصَلِّيَ، ثُمَّ نَرْجِعَ فَنَنْحَرَ، فَمَنْ فَعَلَ فَقَدْ أَصَابَ سُنَّتَنَا ".
Amesimulia Al-Baraa (رضي الله عنه):
Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anatoa Khutba akisema: “Kitu cha kwanza kufanywa katika siku hii (siku ya kwanza ya ‘Iydul-Adhwhaa (‘Iyd ya Hajj au ‘Iydul-Fitwr) ni kuswali kwanza na baada ya kurejea kutoka kuswali ndiyo tunachinja (kwa Jina la Allah) na kila atakayefanya hivyo atakuwa ametekeleza Sunnah yetu.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 951 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 3
|
حَدَّثَنَا عُبَيْدُ بْنُ إِسْمَاعِيلَ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ قَالَتْ دَخَلَ أَبُو بَكْرٍ وَعِنْدِي جَارِيَتَانِ مِنْ جَوَارِي الأَنْصَارِ تُغَنِّيَانِ بِمَا تَقَاوَلَتِ الأَنْصَارُ يَوْمَ بُعَاثَ ـ قَالَتْ وَلَيْسَتَا بِمُغَنِّيَتَيْنِ ـ فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ أَمَزَامِيرُ الشَّيْطَانِ فِي بَيْتِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَذَلِكَ فِي يَوْمِ عِيدٍ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " يَا أَبَا بَكْرٍ إِنَّ لِكُلِّ قَوْمٍ عِيدًا، وَهَذَا عِيدُنَا ".
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها):
Abu Bakr alikuja nyumbani kwangu wakati wasichana wadogo wawili wa ki-Anaswaariy walikuwa wakiimba kando yangu nyimbo za kuwasifu Answaariy kuhusu Siku ya Bu’aath. Na hawakuwa waimbaji. Abu Bakr akasema kwa kulalamika: “Ala za muziki katika nyumba ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)!” Ilitokea mnamo siku ya ‘Iyd na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Abu Bakr! Ipo ‘Iyd kwa kila Ummah, na hii ni ‘Iyd yetu.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 952 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 4
|
04-Mlango
باب الأَكْلِ يَوْمَ الْفِطْرِ قَبْلَ الْخُرُوجِ
Kula Chakula Mnamo Siku Ya ‘Iydul-Fitwr Kabla Ya Kutoka Kwenda Kuswali Swalaah Ya ‘Iydul-Fitwr (‘Iyd Baada Ya Ramadhwaan).
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحِيمِ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، قَالَ حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، قَالَ أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي بَكْرِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لاَ يَغْدُو يَوْمَ الْفِطْرِ حَتَّى يَأْكُلَ تَمَرَاتٍ. وَقَالَ مُرَجَّى بْنُ رَجَاءٍ حَدَّثَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ قَالَ حَدَّثَنِي أَنَسٌ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَيَأْكُلُهُنَّ وِتْرًا.
Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه):
Rasuli wa Allaah (صلى لله عليه وآله وسلم) alikuwa kamwe haendi kuswali Siku ya ‘Iydul-Fitwr mpaka alipokwishakula tende.
Kutoka kwa Anas pia amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akila tende kwa idadi ya Witr.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 953 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 5
|
05-Mlango
باب الأَكْلِ يَوْمَ النَّحْرِ
Kula Chakula Siku Ya An-Nahr (Siku Ya Kuchinja, Au Siku Ya ‘Iydul-Adhwhaa Tarehe 10 Dhul-Hijjah)
|
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " مَنْ ذَبَحَ قَبْلَ الصَّلاَةِ فَلْيُعِدْ ". فَقَامَ رَجُلٌ فَقَالَ هَذَا يَوْمٌ يُشْتَهَى فِيهِ اللَّحْمُ. وَذَكَرَ مِنْ جِيرَانِهِ فَكَأَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم صَدَّقَهُ، قَالَ وَعِنْدِي جَذَعَةٌ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ شَاتَىْ لَحْمٍ، فَرَخَّصَ لَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَلاَ أَدْرِي أَبَلَغَتِ الرُّخْصَةُ مَنْ سِوَاهُ أَمْ لاَ.
Amesimulia Anas (رضي الله عنه):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote atakayechinja kafara yake kabla ya Swalaah ya ‘Iyd, sharti achinje tena.” Mtu mmoja akasimama na kusema: “Hii ni siku ambapo kila mtu ana hamu ya nyama.” Na akataja jambo kuhusu majirani zake. Ilielekea kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimsadiki. Kisha mtu yuleyule aliongeza: “Ninaye mbuzi jike ambaye nampenda zaidi kuliko nyama ya kondoo wawili.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamruhusu amchinje mbuzi yule. Sielewi kama ruhusa ile ilikuwa ni ruhusa kwa ajili yake tu au kwa watu wengine pia.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 954 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 6
|
حَدَّثَنَا عُثْمَانُ، قَالَ حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنِ الشَّعْبِيِّ، عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ خَطَبَنَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ الأَضْحَى بَعْدَ الصَّلاَةِ فَقَالَ " مَنْ صَلَّى صَلاَتَنَا وَنَسَكَ نُسُكَنَا فَقَدْ أَصَابَ النُّسُكَ، وَمَنْ نَسَكَ قَبْلَ الصَّلاَةِ فَإِنَّهُ قَبْلَ الصَّلاَةِ، وَلاَ نُسُكَ لَهُ ". فَقَالَ أَبُو بُرْدَةَ بْنُ نِيَارٍ خَالُ الْبَرَاءِ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَإِنِّي نَسَكْتُ شَاتِي قَبْلَ الصَّلاَةِ، وَعَرَفْتُ أَنَّ الْيَوْمَ يَوْمُ أَكْلٍ وَشُرْبٍ، وَأَحْبَبْتُ أَنْ تَكُونَ شَاتِي أَوَّلَ مَا يُذْبَحُ فِي بَيْتِي، فَذَبَحْتُ شَاتِي وَتَغَدَّيْتُ قَبْلَ أَنْ آتِيَ الصَّلاَةَ. قَالَ " شَاتُكَ شَاةُ لَحْمٍ ". قَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَإِنَّ عِنْدَنَا عَنَاقًا لَنَا جَذَعَةً هِيَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ شَاتَيْنِ، أَفَتَجْزِي عَنِّي قَالَ " نَعَمْ، وَلَنْ تَجْزِيَ عَنْ أَحَدٍ بَعْدَكَ ".
Amesimulia Al-Baraa Bin ’Aazib (رضي الله عنه):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoa Khutba baada ya kuswali siku ya Al-Adhwhaa akasema: “Yeyote anayeswali kama sisi na akachinja kama sisi, basi Nusuk (kuchinja) yake itakubaliwa na Allaah. Na yeyote anayechinja kabla ya Swalaah ya ‘Iyd, basi huyo anakuwa hana Nusuk.” Abu Burdah bin Niyaar, ‘Amm wa Al-Baraa akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nimechinja kondoo wangu kabla ya Swalaah ya ‘Iyd, na nilifikiri kuwa leo hii ikiwa ni siku ya kula na kunywa (siyo vinywaji vilevi), na nikapenda kondoo wangu awe wa kwanza kuchinjwa nyumbani mwangu. Kwa hivyo nilimchinja kondoo wangu na nikala chakula kabla ya kuja kuswali.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Huyo kondoo uliyemchinja ni nyama tu ya kondoo (na siyo kafara).” Abu Burda akasema: “Ee Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)! Mimi ninaye mbuzi jike ambaye ninampenda kuliko kondoo wawili. Je, huyo atanitosheleza kuwa ni kafara yangu?” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naam, atatosheleza kwa ajili yako, lakini hatotosheleza (kuwa ni kafara) kwa ajili ya mtu yeyote baada yako.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 955 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 7
|
06-Mlango
باب الْخُرُوجِ إِلَى الْمُصَلَّى بِغَيْرِ مِنْبَرٍ
Kwenda Katika Muswallaa (Mahali Pa Kuswalia) Pasipokuwa Na Mimbari
|
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي مَرْيَمَ، قَالَ حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي زَيْدٌ، عَنْ عِيَاضِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي سَرْحٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَخْرُجُ يَوْمَ الْفِطْرِ وَالأَضْحَى إِلَى الْمُصَلَّى، فَأَوَّلُ شَىْءٍ يَبْدَأُ بِهِ الصَّلاَةُ ثُمَّ يَنْصَرِفُ، فَيَقُومُ مُقَابِلَ النَّاسِ، وَالنَّاسُ جُلُوسٌ عَلَى صُفُوفِهِمْ، فَيَعِظُهُمْ وَيُوصِيهِمْ وَيَأْمُرُهُمْ، فَإِنْ كَانَ يُرِيدُ أَنْ يَقْطَعَ بَعْثًا قَطَعَهُ، أَوْ يَأْمُرَ بِشَىْءٍ أَمَرَ بِهِ، ثُمَّ يَنْصَرِفُ. قَالَ أَبُو سَعِيدٍ فَلَمْ يَزَلِ النَّاسُ عَلَى ذَلِكَ حَتَّى خَرَجْتُ مَعَ مَرْوَانَ وَهْوَ أَمِيرُ الْمَدِينَةِ فِي أَضْحًى أَوْ فِطْرٍ، فَلَمَّا أَتَيْنَا الْمُصَلَّى إِذَا مِنْبَرٌ بَنَاهُ كَثِيرُ بْنُ الصَّلْتِ، فَإِذَا مَرْوَانُ يُرِيدُ أَنْ يَرْتَقِيَهُ قَبْلَ أَنْ يُصَلِّيَ، فَجَبَذْتُ بِثَوْبِهِ فَجَبَذَنِي فَارْتَفَعَ، فَخَطَبَ قَبْلَ الصَّلاَةِ، فَقُلْتُ لَهُ غَيَّرْتُمْ وَاللَّهِ. فَقَالَ أَبَا سَعِيدٍ، قَدْ ذَهَبَ مَا تَعْلَمُ. فَقُلْتُ مَا أَعْلَمُ وَاللَّهِ خَيْرٌ مِمَّا لاَ أَعْلَمُ. فَقَالَ إِنَّ النَّاسَ لَمْ يَكُونُوا يَجْلِسُونَ لَنَا بَعْدَ الصَّلاَةِ فَجَعَلْتُهَا قَبْلَ الصَّلاَةِ.
Amesimulia Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikwenda kwenye Muswallaa mnamo siku za ‘Iydul-Fitwr na ‘Iydul-Adhwhaa. Kitu cha kwanza cha kuanzia kilikuwa Swalaah, na baada ya hapo alisimama mbele ya watu, na watu waliendelea kukaa katika Swaff zao. Kisha akawakhutubia, akawapa mawaidha, akawausia na akawapa amri (yaani Khutba). Na baada ya hivyo, pindi akitaka kupeleka jeshi la kushambulia, basi alifanya hivyo.
Abu Sa’iyd aliendelea kusema: Au akiwa anataka kutoa amri, atatoa amri hizo na kisha huondoka. Watu walifuata mila ile mpaka nilipokwenda na Marwaan, Gavana wa Madiynah kwa ajili ya Swalaah ya ‘Iydul-Adhwhaa au ‘Iydul-Fitwr. Tulipowasili kwenye Muswallaa, kulikuweko Mimbari iliyotengenezwa na Kathiyr bin As-Swalt. Marwaan alitaka kupanda pale kwenye Mimbari kabla ya Swalaah. Nilizishika nguo zake lakini yeye akazivuta na akapanda juu ya Mimbari, akatoa Khutba kabla ya Swalaah. Nikamwambia: “Wa-Allaahi umegeuza (Sunnah ya Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) )!” Yeye akajibu: “Ee Abu Sa’iyd! Unayoyafahamu wewe yamepitwa na wakati.” Mie nikasema: “Wa-Allaahi! Ninachofahamu ni bora kuliko nisichofahamu.” Marwaan akasema: “Watu hawakai kusikiliza Khutba yetu baada ya Swalaah, kwa hivyo nimetoa Khutba kabla ya Swalaah.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 956 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 8
|
07-Mlango
باب الْمَشْىِ وَالرُّكُوبِ إِلَى الْعِيدِ بِغَيْرِ أَذَانٍ وَلاَ إِقَامَةٍ
Kutembea Na Kupanda Kipando Kwa Ajili Ya Swalaah Ya ‘Iyd. Swalaah Ya ‘Iyd Huswaliwa Kabla Ya Kutoa Khutba, Na Huwa Haina Adhana Wala Iqaamah
|
حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، قَالَ حَدَّثَنَا أَنَسٌ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ،. أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يُصَلِّي فِي الأَضْحَى وَالْفِطْرِ، ثُمَّ يَخْطُبُ بَعْدَ الصَّلاَةِ.
Amesimulia ’Abdullaah bin ’Umar (رضي الله عنهما):
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalaah ya ‘Iydul-Adhwaa au ‘Iydul-Fitwr kisha hutoa Khutba baada ya Swalaah.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 957 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 9
|
حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، قَالَ أَخْبَرَنَا هِشَامٌ، أَنَّ ابْنَ جُرَيْجٍ، أَخْبَرَهُمْ قَالَ أَخْبَرَنِي عَطَاءٌ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ سَمِعْتُهُ يَقُولُ إِنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ يَوْمَ الْفِطْرِ، فَبَدَأَ بِالصَّلاَةِ قَبْلَ الْخُطْبَةِ. قَالَ وَأَخْبَرَنِي عَطَاءٌ، أَنَّ ابْنَ عَبَّاسٍ، أَرْسَلَ إِلَى ابْنِ الزُّبَيْرِ فِي أَوَّلِ مَا بُويِعَ لَهُ إِنَّهُ لَمْ يَكُنْ يُؤَذَّنُ بِالصَّلاَةِ يَوْمَ الْفِطْرِ، إِنَّمَا الْخُطْبَةُ بَعْدَ الصَّلاَةِ. وَأَخْبَرَنِي عَطَاءٌ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالاَ لَمْ يَكُنْ يُؤَذَّنُ يَوْمَ الْفِطْرِ وَلاَ يَوْمَ الأَضْحَى. وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ سَمِعْتُهُ يَقُولُ إِنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَامَ فَبَدَأَ بِالصَّلاَةِ، ثُمَّ خَطَبَ النَّاسَ بَعْدُ، فَلَّمَا فَرَغَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نَزَلَ فَأَتَى النِّسَاءَ، فَذَكَّرَهُنَّ وَهْوَ يَتَوَكَّأُ عَلَى يَدِ بِلاَلٍ، وَبِلاَلٌ بَاسِطٌ ثَوْبَهُ، يُلْقِي فِيهِ النِّسَاءُ صَدَقَةً. قُلْتُ لِعَطَاءٍ أَتَرَى حَقًّا عَلَى الإِمَامِ الآنَ أَنْ يَأْتِيَ النِّسَاءَ فَيُذَكِّرَهُنَّ حِينَ يَفْرُغُ قَالَ إِنَّ ذَلِكَ لَحَقٌّ عَلَيْهِمْ، وَمَا لَهُمْ أَنْ لاَ يَفْعَلُوا
Amesimulia Ibn Jurayj (رضي الله عنه):
’Atwaa amesema: “Jaabir bin ’Abdillaah amesema: “Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka siku ya ‘Iydul-Fitwr akaswalisha Swalaah kabla ya kutoa Khutba.” ’Atwaa aliniambia kuwa nyakati za mwanzo za Ibn Az-Zubayr, Ibn ‘Abbaas alimpelekea ujumbe yeye akamwambia kuwa Adhana kwa ajili ya Swalaah ya ‘Iyd haikuwa inanadiwa (katika uhai wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na Khutba ilikuwa ikitolewa baada ya Swalaah. ’Atwaa aliniambia mimi kuwa Ibn ‘Abbaas na Jaabir bin ’Abdillaah wamesema: “Hakukuweko Adhaan kwa ajili ya Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr na ‘Iydul-Adhwhaa.” ’Atwaa amesema: “Nilimsikia Jaabir bin ’Abdillaah akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama akaanza kwa Swalaah kisha akatoa Khutba. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomaliza (Khutba) alikwenda kwa wanawake akawakhutubia, wakati yeye ameegemea mkono wa Bilaal. Bilaal alikuwa katandaza nguo yake na wanawake walikuwa wanaweka swadaqah mle. Nilimuuliza ’Atwaa: Unadhani Imaam anawajibika kwenda kwa wanawake kuwakhutubia baada ya kumaliza Swalaah na Khutba?
’Atwaa akajibu: “Bila shaka ni wajibu wa Imaam kufanya hivyo, na kwa nini wasifanye hivyo?”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 958, 959, 960, 961 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 10
|
08-Mlango
باب الْخُطْبَةِ بَعْدَ الْعِيدِ
Khutba Sharti Itolewe Baada Ya Swalaah Ya ‘Iyd
|
حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، قَالَ أَخْبَرَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي الْحَسَنُ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ شَهِدْتُ الْعِيدَ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ وَعُثْمَانَ ـ رضى الله عنهم ـ فَكُلُّهُمْ كَانُوا يُصَلُّونَ قَبْلَ الْخُطْبَةِ.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):
Niliswali Swalaah ya ‘Iyd pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na akina Abu Bakr, ’Umar, na ’Uthmaan (رضي الله عنهم) na wote waliswali kabla ya kutolewa Khutba.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 962 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 11
|
حَدَّثَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، قَالَ حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَبُو بَكْرٍ وَعُمَرُ ـ رضى الله عنهما ـ يُصَلُّونَ الْعِيدَيْنِ قَبْلَ الْخُطْبَةِ.
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما):
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na akina Abu Bakr na ’Umar (رضي الله عنهما) walikuwa wakiswali Swalaah mbili za ‘Iyd kabla ya kutolewa Khutba.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 963 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 12
|
حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَدِيِّ بْنِ ثَابِتٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم صَلَّى يَوْمَ الْفِطْرِ رَكْعَتَيْنِ، لَمْ يُصَلِّ قَبْلَهَا وَلاَ بَعْدَهَا، ثُمَّ أَتَى النِّسَاءَ وَمَعَهُ بِلاَلٌ، فَأَمَرَهُنَّ بِالصَّدَقَةِ، فَجَعَلْنَ يُلْقِينَ، تُلْقِي الْمَرْأَةُ خُرْصَهَا وَسِخَابَهَا.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali Swalaah ya Rakaa mbili mnamo siku ya ‘Iydul-Fitwr na hakuswali kabla au baada Swalaah hiyo. Kisha akaenda kwa wanawake pamoja na Bilaal na akawaamuru watoe Swadaqah. Kwa hivyo wakaanza kutoa hereni za masikioni na shanga zao za shingoni (kama Swadaqah).
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 964 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 13
|
حَدَّثَنَا آدَمُ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ حَدَّثَنَا زُبَيْدٌ، قَالَ سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " إِنَّ أَوَّلَ مَا نَبْدَأُ فِي يَوْمِنَا هَذَا أَنْ نُصَلِّيَ، ثُمَّ نَرْجِعَ فَنَنْحَرَ، فَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ فَقَدْ أَصَابَ سُنَّتَنَا، وَمَنْ نَحَرَ قَبْلَ الصَّلاَةِ فَإِنَّمَا هُوَ لَحْمٌ قَدَّمَهُ لأَهْلِهِ، لَيْسَ مِنَ النُّسْكِ فِي شَىْءٍ ". فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ يُقَالُ لَهُ أَبُو بُرْدَةَ بْنُ نِيَارٍ يَا رَسُولَ اللَّهِ، ذَبَحْتُ وَعِنْدِي جَذَعَةٌ خَيْرٌ مِنْ مُسِنَّةٍ. فَقَالَ " اجْعَلْهُ مَكَانَهُ، وَلَنْ تُوفِيَ أَوْ تَجْزِيَ عَنْ أَحَدٍ بَعْدَكَ ".
Amesimulia Al-Baraa Bin ’Aazib (رضي الله عنه):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jambo la kwanza ambalo tutalifanya katika siku hii yetu ni kuswali, kisha turudi kuchinja. Kwa hivyo mtu yeyote afanyaye hivyo anakuwa kakidhi Sunnah na yeyote anayechinja kabla ya Swalaah, inakuwa ni nyama tu aliyowapa familia yake na wala haitohesabika kuwa ni Nusuk (kafara ya kuchinja). Mtu mmoja wa ki-Answaariy aitwaye Abu Burdah bin Niyaar amesema: “Ee Rasuli wa Allaah, Nilichinja (kabla ya Swalaah). Lakini nina mbuzi mdogo ambaye ni bora kuliko kondoo mkubwa.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mtoe kuchinjwa huyo badala ya yule wa kwanza, lakini haitatosheleza (kama Nusuk) hiyo kwa ajili ya mtu yeyote baada yako.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 965 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 14
|
09-Mlango
باب مَا يُكْرَهُ مِنْ حَمْلِ السِّلاَحِ فِي الْعِيدِ وَالْحَرَمِ
Inachukiza Kuchukua Silaha Siku Ya ‘Iyd Na Katika Eneo La Haram (Mahali Patukufu)
|
وَقَالَ الْحَسَنُ نُهُوا أَنْ يَحْمِلُوا السِّلاَحَ يَوْمَ عِيدٍ إِلاَّ أَنْ يَخَافُوا عَدُوًّا.
Na Al-Hasan amesema: “Katika uhai wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ilikatazwa kuchukua silaha mnamo siku ya ‘Iyd isipokuwa kukiweko khofu kutoka kwa maadui.”
حَدَّثَنَا زَكَرِيَّاءُ بْنُ يَحْيَى أَبُو السُّكَيْنِ، قَالَ حَدَّثَنَا الْمُحَارِبِيُّ، قَالَ حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سُوقَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ كُنْتُ مَعَ ابْنِ عُمَرَ حِينَ أَصَابَهُ سِنَانُ الرُّمْحِ فِي أَخْمَصِ قَدَمِهِ، فَلَزِقَتْ قَدَمُهُ بِالرِّكَابِ، فَنَزَلْتُ فَنَزَعْتُهَا وَذَلِكَ بِمِنًى، فَبَلَغَ الْحَجَّاجَ فَجَعَلَ يَعُودُهُ فَقَالَ الْحَجَّاجُ لَوْ نَعْلَمُ مَنْ أَصَابَكَ. فَقَالَ ابْنُ عُمَرَ أَنْتَ أَصَبْتَنِي. قَالَ وَكَيْفَ قَالَ حَمَلْتَ السِّلاَحَ فِي يَوْمٍ لَمْ يَكُنْ يُحْمَلُ فِيهِ، وَأَدْخَلْتَ السِّلاَحَ الْحَرَمَ وَلَمْ يَكُنِ السِّلاَحُ يُدْخَلُ الْحَرَمَ.
Amesimulia Sa’iyd Bin Jubayr (رضي الله عنه):
Nilikuwa na Ibn ‘Umar wakati kichwa cha mkuki kilitoboa wayo wa mguu wake, na mguu wake ukang’ang’ania kwenye kitako cha tandiko la farasi. Nami nilishuka nikauvuta mguu wake ukatoka. Na hiyo ilitokea kule Minaa. Al-Hajjaaj alipata khabari hizi akaja kuulizia hali ya afya yake akasema: “Laiti tungemjua mtu aliyekujeruhi!” Naye Ibn ’Umar akajibu: “Wewe ndiwe uliyenijeruhi mimi.” Al-Hajjaaj akasema: “Ilikuwaje?” Ibn ’Umar akasema: “Ni wewe uliyeruhusu kuchukua silaha mnamo siku ambayo hakuna aliyekuwa akichukua silaha, na uliruhusu silaha kuchukuliwa ndani ya Haram ingawa haikuwa inaruhusiwa hapo zamani.’”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 966 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 15
|
حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ يَعْقُوبَ، قَالَ حَدَّثَنِي إِسْحَاقُ بْنُ سَعِيدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ سَعِيدِ بْنِ الْعَاصِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ دَخَلَ الْحَجَّاجُ عَلَى ابْنِ عُمَرَ وَأَنَا عِنْدَهُ، فَقَالَ كَيْفَ هُوَ فَقَالَ صَالِحٌ. فَقَالَ مَنْ أَصَابَكَ قَالَ أَصَابَنِي مَنْ أَمَرَ بِحَمْلِ السِّلاَحِ فِي يَوْمٍ لاَ يَحِلُّ فِيهِ حَمْلُهُ، يَعْنِي الْحَجَّاجَ.
Amesimulia Sa’iyd Bin ‘Amr Bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه):
Kutoka kwa baba yake kwamba: Al-Hajjaaj alikwenda kwa Ibn ’Umar wakati nilipokuwa kule. Al Hajjaaj alimwuliza Ibn ‘Umar: “Unajisikiaje hali yako?” Ibn ‘Umar akajibu: “Mimi sijambo.” Al-Hajjaaj akauliza: “Ni nani aliyekujeruhi?” Ibn ’Umar akajibu: “Ni yule aliyeruhusu silaha zichukuliwe mnamo siku ambayo ilikuwa imekatazwa kuchukua silaha (alimaanisha Al-Hajjaaj).”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 967 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 16
|
10-Mlango
باب التَّبْكِيرِ إِلَى الْعِيدِ
Kuswali Swalaah Ya ‘Iyd Mapema
|
وَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ بُسْرٍ إِنْ كُنَّا فَرَغْنَا فِي هَذِهِ السَّاعَةِ، وَذَلِكَ حِينَ التَّسْبِيحِ.
’Abdullaah bin Busr amesema: “Tulikuwa tukimaliza Swalaah ya ’Iyd (wakati wa uhai wa Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) mnamo wakati wa Tasbiyh (yaani wakati wa Ishraaq na Adhw-Dhwuhaa), yaani baada ya mawio (mapambazuko) ya jua.
حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ زُبَيْدٍ، عَنِ الشَّعْبِيِّ، عَنِ الْبَرَاءِ، قَالَ خَطَبَنَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ النَّحْرِ قَالَ " إِنَّ أَوَّلَ مَا نَبْدَأُ بِهِ فِي يَوْمِنَا هَذَا أَنْ نُصَلِّيَ ثُمَّ نَرْجِعَ فَنَنْحَرَ، فَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ فَقَدْ أَصَابَ سُنَّتَنَا، وَمَنْ ذَبَحَ قَبْلَ أَنْ يُصَلِّيَ فَإِنَّمَا هُوَ لَحْمٌ عَجَّلَهُ لأَهْلِهِ، لَيْسَ مِنَ النُّسُكِ فِي شَىْءٍ ". فَقَامَ خَالِي أَبُو بُرْدَةَ بْنُ نِيَارٍ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنَا ذَبَحْتُ قَبْلَ أَنْ أُصَلِّيَ وَعِنْدِي جَذَعَةٌ خَيْرٌ مِنْ مُسِنَّةٍ. قَالَ " اجْعَلْهَا مَكَانَهَا ـ أَوْ قَالَ اذْبَحْهَا ـ وَلَنْ تَجْزِيَ جَذَعَةٌ عَنْ أَحَدٍ بَعْدَكَ ".
Amesimulia Al-Baraa (رضي الله عنه):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoa Khutba mnamo siku ya An-Nahr (Siku ya kuchinja yaani ‘Iydul-Adhwhaa) akasema: “Kitu cha kwanza tulazimikacho kufanya mnamo siku yetu hii ni kuswali kisha turudi tukachinje (kafara zetu). Kwa hivyo yeyote anayefanya hivyo huwa katekeleza Sunnah yetu, na yeyote anayechinja kabla ya Swalaah basi hiyo ilikuwa nyama ya kawaida tu aliyoitoa kwa familia yake, na haitohesabiwa kuwa ni Nusuk (kafara ya kuchinja) kwa njia yeyote ile.” ‘Ammi yangu Abu Burda bin Niyaar akasimama na kusema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nilimchinja kabla ya Swalaah, lakini ninaye mbuzi jike mdogo ambaye ni mbora kuliko kondoo mkubwa.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mchinje huyo kwa niaba ya wa kwanza na mbuzi huyo hatohesabiwa kuwa ni kafara kwa ajli ya mtu yeyote baada yako.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 968 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 17
|
11-Mlango
باب فَضْلِ الْعَمَلِ فِي أَيَّامِ التَّشْرِيقِ
Fadhila Za Ayyaamut-Tashriyq (Masiku Ya Tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah)
|
وَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ وَاذْكُرُوا اللَّهَ فِي أَيَّامٍ مَعْلُومَاتٍ أَيَّامُ الْعَشْرِ، وَالأَيَّامُ الْمَعْدُودَاتُ أَيَّامُ التَّشْرِيقِ.
وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ وَأَبُو هُرَيْرَةَ يَخْرُجَانِ إِلَى السُّوقِ فِي أَيَّامِ الْعَشْرِ يُكَبِّرَانِ، وَيُكَبِّرُ النَّاسُ بِتَكْبِيرِهِمَا.
وَكَبَّرَ مُحَمَّدُ بْنُ عَلِيٍّ خَلْفَ النَّافِلَةِ.
Ibn ‘Abbaas amesema kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
(لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ))
((Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku zinazojulikana)) [Al-Hajj: 28]
Ni masiku kumi ya Dhul-Hijjah
وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ
Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. [Al-Baqarah: 203]
Ni Ayyaamut-Tashriyq (Siku za kukausha nyama; tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah).
Ibn ’Umar na Abu Hurayrah walikuwa wakienda sokoni kutamka kwa sauti Takbiyrah, na watu nao wakawa wanatamka Takbiyrah kwa sauti baada ya Takbiyrah zao.
Muhammad bin ’Aliy alikuwa akitamka Takbiyrah baada ya Nawaafil. (Swalaah za Sunnah)
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَرْعَرَةَ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ مُسْلِمٍ الْبَطِينِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ قَالَ " مَا الْعَمَلُ فِي أَيَّامِ الْعَشْرِ أَفْضَلَ مِنَ الْعَمَلِ فِي هَذِهِ ". قَالُوا وَلاَ الْجِهَادُ قَالَ " وَلاَ الْجِهَادُ، إِلاَّ رَجُلٌ خَرَجَ يُخَاطِرُ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ بِشَىْءٍ ".
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna amali njema zinazotendwa mnamo masiku mengineyo ziwe na ubora zaidi kuliko zile zinazotendwa mnamo siku hizi (siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah ndio bora zaidi).” Swahaba wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema: “Hata Jihaad? (Yaani siyo bora zaidi?)” Akajibu: “Hata Jihaad isipokuwa ya yule mtu ambaye anaitenda hiyo Jihaad kwa kujiweka yeye menyewe na mali zake hatarini, kwa ajili ya Allaah, kisha harejei na chochote kati ya hivyo vitu.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 969 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 18
|
12-Mlango
باب التَّكْبِيرِ أَيَّامَ مِنًى وَإِذَا غَدَا إِلَى عَرَفَةَ
Kutamka Takbiyrah Kwa Sauti Mnamo Siku Ya Minaa Na Wakati Wa Kwenda ‘Arafah
|
وَكَانَ عُمَرُ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ يُكَبِّرُ فِي قُبَّتِهِ بِمِنًى فَيَسْمَعُهُ أَهْلُ الْمَسْجِدِ، فَيُكَبِّرُونَ وَيُكَبِّرُ أَهْلُ الأَسْوَاقِ، حَتَّى تَرْتَجَّ مِنًى تَكْبِيرًا.
’Umar wakati akikaa Minaa alikuwa akitamka Takbiyrah katika hema lake kwa sauti kubwa kiasi kwamba watu waliokuwa Msikitini waliisikia nao wakaanza kutamka Takbiyrah, na watu sokoni pia wakatamka Takbiyrah, na kisha Minaa yote ikawa inatetemeka kwa Takbiyrah.
وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يُكَبِّرُ بِمِنًى تِلْكَ الأَيَّامَ وَخَلْفَ الصَّلَوَاتِ، وَعَلَى فِرَاشِهِ وَفِي فُسْطَاطِهِ، وَمَجْلِسِهِ وَمَمْشَاهُ تِلْكَ الأَيَّامَ جَمِيعًا.
Na mnamo siku hizo Ibn ’Umar alikuwa akitamka Takbiyrah pale Minaa, na baada ya Swalaah za fardhi, na pia alipokuwa kitandani ndani ya hema lake, wakati amekaa na wakati akitembea. Alikuwa akifanya hivyo mnamo siku zote hizo.
وَكَانَتْ مَيْمُونَةُ تُكَبِّرُ يَوْمَ النَّحْرِ. وَكُنَّ النِّسَاءُ يُكَبِّرْنَ خَلْفَ أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ وَعُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزَ لَيَالِيَ التَّشْرِيقِ مَعَ الرِّجَالِ فِي الْمَسْجِدِ.
Mayumwunah alikuwa akitamka Takbiyrah mnamo siku ya An-Nahr. Wanawake walikuwa wakitamka Takbiyrah (kwa sauti isiyosikika) nyuma ya Abaan bin ’Uthmaan na ’Umar bin ‘Abdil-‘Aziyz pamoja na wanamume Msikitini nyakati za kila usiku wa Ayyaamut-Tashriyq (Masiku ya tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah)
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، قَالَ حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ أَنَسٍ، قَالَ حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ أَبِي بَكْرٍ الثَّقَفِيُّ، قَالَ سَأَلْتُ أَنَسًا وَنَحْنُ غَادِيَانِ مِنْ مِنًى إِلَى عَرَفَاتٍ عَنِ التَّلْبِيَةِ كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ كَانَ يُلَبِّي الْمُلَبِّي لاَ يُنْكَرُ عَلَيْهِ، وَيُكَبِّرُ الْمُكَبِّرُ فَلاَ يُنْكَرُ عَلَيْهِ.
Amesimulia Muhammad Bin Abi Bakr Al-Thaqafiyy:
Tulipokuwa tunatoka kutoka Minaa kuelekea ’Arafah, nilimuuliza Anas bin Maalik kuhusu At-Talbiyah: Mlikuwa mkitamkaje Talbiyah mlipokuwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)? Anas akajibu: “Watu walikuwa wakitamka Talbiyah, nayo haikuwa inakatazwa, na walikuwa wakitamka Takbiyrah kwa sauti na hiyo pia haikuwa inakatazwa.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 970 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 19
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصٍ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ حَفْصَةَ، عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ، قَالَتْ كُنَّا نُؤْمَرُ أَنْ نَخْرُجَ يَوْمَ الْعِيدِ، حَتَّى نُخْرِجَ الْبِكْرَ مِنْ خِدْرِهَا، حَتَّى نُخْرِجَ الْحُيَّضَ فَيَكُنَّ خَلْفَ النَّاسِ، فَيُكَبِّرْنَ بِتَكْبِيرِهِمْ، وَيَدْعُونَ بِدُعَائِهِمْ يَرْجُونَ بَرَكَةَ ذَلِكَ الْيَوْمِ وَطُهْرَتَهُ.
Amesimulia Ummu ‘Atwiyyah (رضي الله عنها):
Tulikuwa tunaamrishwa kutoka nje mnamo siku ya ‘Iyd, na hata kuwaleta wasichana mabikira toka majumbani kwao na hata wanawake waliokuwa na hedhi ili wasimame nyuma ya wanamume na watamke Takbiyrah kwa sauti pamoja nao na waombe Du’aa kwa Allaah na kutaraji Baraka za siku ile na utakaso wa madhambi yao.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 971 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 20
|
13-Mlango
باب الصَّلاَةِ إِلَى الْحَرْبَةِ يَوْمَ الْعِيدِ
Kuswali Siku Ya ‘Iyd kwa Kutumia Harbah (Mkuki Mdogo Kama Sutrah)
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَهَّابِ، قَالَ حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ تُرْكَزُ الْحَرْبَةُ قُدَّامَهُ يَوْمَ الْفِطْرِ وَالنَّحْرِ ثُمَّ يُصَلِّي.
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما):
Mnamo siku ya ‘Iydul-Fitwr na ‘Iydul-Adhwhaa, mkuki ulikuwa ukisimikwa mbele ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (kama Sutrah wakati wa kuswali), kisha yeye huswali.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 972 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 21
|
14-Mlango
باب حَمْلِ الْعَنَزَةِ أَوِ الْحَرْبَةِ بَيْنَ يَدَىِ الإِمَامِ يَوْمَ الْعِيدِ
Kuweka ‘Anazah (Fimbo Yenye Kichwa Cha Mkuki) Au Harbah (Mkuki Mdogo) Mbele Ya Imaam Siku Ya ‘Iyd
|
حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، قَالَ حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو عَمْرٍو، قَالَ أَخْبَرَنِي نَافِعٌ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَغْدُو إِلَى الْمُصَلَّى، وَالْعَنَزَةُ بَيْنَ يَدَيْهِ، تُحْمَلُ وَتُنْصَبُ بِالْمُصَلَّى بَيْنَ يَدَيْهِ فَيُصَلِّي إِلَيْهَا.
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akienda kwenye Muswallaa na ‘Anazah ikawa inachukuliwa kabla yake na ikasimikwa ndani ya Muswallaa mbele yake, naye akawa anaswali huku akiielekea hiyo ‘Anaza (kama Sutrha).
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 973 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 22
|
15-Mlango
باب خُرُوجِ النِّسَاءِ وَالْحُيَّضِ إِلَى الْمُصَلَّى
Kutoka Kwa Wanawake Na Wanawake Wenye Hedhi Kwenda Muswallaa
|
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْوَهَّابِ، قَالَ حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ، قَالَتْ أُمِرْنَا أَنْ نُخْرِجَ، الْعَوَاتِقَ وَذَوَاتِ الْخُدُورِ. وَعَنْ أَيُّوبَ عَنْ حَفْصَةَ بِنَحْوِهِ. وَزَادَ فِي حَدِيثِ حَفْصَةَ قَالَ أَوْ قَالَتِ الْعَوَاتِقَ وَذَوَاتِ الْخُدُورِ، وَيَعْتَزِلْنَ الْحُيَّضُ الْمُصَلَّى.
Amesimulia Muhammad (رضي الله عنه):
Ummu ‘Atwiyyah amesema: “Tuliamrishwa (na Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) tutoke nje pamoja ya wasichana waliovunja ungo karibuni, wenye hedhi, na wanawali.” Na kutoka kwa Ayyuwb kutoka kwa Hafswah amesimulia kama hivyo au kasema Hafswah: “Wasichana waliovunja ungo karibuni, wenye hedhi, na wanawali wakiwa wametengwa mbali na Muswallaa.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 974 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 23
|
16-Mlango
باب خُرُوجِ الصِّبْيَانِ إِلَى الْمُصَلَّى
Wavulana Kutoka Kwa Ajili Ya Kuhudhuria Muswallaa
|
حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَبَّاسٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ، قَالَ خَرَجْتُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ فِطْرٍ أَوْ أَضْحَى، فَصَلَّى ثُمَّ خَطَبَ، ثُمَّ أَتَى النِّسَاءَ فَوَعَظَهُنَّ وَذَكَّرَهُنَّ، وَأَمَرَهُنَّ بِالصَّدَقَةِ.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):
Wakati wa ujana wangu, nilikwenda nje na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya ‘Iydul-Fitwr na ‘Iydul-Adhwhaa. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali kisha akatoa Khutba kisha akaenda kwa wanawake akawakhutubia akawapa mawaidha na kuwakumbusha nasaha na kuwaamuru watoe Swadaqah.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 975 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 24
|
17-Mlango
باب اسْتِقْبَالِ الإِمَامِ النَّاسَ فِي خُطْبَةِ الْعِيدِ
Imamu Huelekeza Uso Wake Kwa Watu Wakati Anatoa Khutba Ya ‘Iyd
|
قَالَ أَبُو سَعِيدٍ قَامَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُقَابِلَ النَّاسِ.
Abu Sa’iyd amesema: “Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama akielekeza uso wake kwa watu.”
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، قَالَ حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ طَلْحَةَ، عَنْ زُبَيْدٍ، عَنِ الشَّعْبِيِّ، عَنِ الْبَرَاءِ، قَالَ خَرَجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ أَضْحًى إِلَى الْبَقِيعِ فَصَلَّى رَكْعَتَيْنِ، ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَيْنَا بِوَجْهِهِ وَقَالَ " إِنَّ أَوَّلَ نُسُكِنَا فِي يَوْمِنَا هَذَا أَنْ نَبْدَأَ بِالصَّلاَةِ، ثُمَّ نَرْجِعَ فَنَنْحَرَ، فَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ فَقَدْ وَافَقَ سُنَّتَنَا، وَمَنْ ذَبَحَ قَبْلَ ذَلِكَ فَإِنَّمَا هُوَ شَىْءٌ عَجَّلَهُ لأَهْلِهِ، لَيْسَ مِنَ النُّسُكِ فِي شَىْءٍ ". فَقَامَ رَجُلٌ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي ذَبَحْتُ وَعِنْدِي جَذَعَةٌ خَيْرٌ مِنْ مُسِنَّةٍ. قَالَ " اذْبَحْهَا، وَلاَ تَفِي عَنْ أَحَدٍ بَعْدَكَ ".
Amesimulia Al-Baraa (رضي الله عنه):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikwenda kuelekea Al-Baqiy’ (kwenye makaburi ya Madiynah), mnamo siku ya ‘Iydul-Adhwhaa akaswalisha Rakaa mbili katika Swalaah ya ‘Iydul-Adhwhaa, kisha akaugeuzia uso wake kwetu akasema: “Katika siku hii yetu, tendo la kwanza kulitekeleza ni kuswali kisha tutarejea kwenda kuchinja na yeyote atakayefanya hivi atakuwa anatekeleza Sunnah yetu. Na yeyote atakayechinja kabla ya hivyo (yaani kabla ya kuswali), hicho kitakuwa kitu alichoandaa kabla na hakitohesabiwa kama Nusuk (kafara ya kuchinja).” Mtu mmoja akasimama akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nilichinja (mnyama kabla ya Swalaah). Ninaye mbuzi mdogo jike ambaye ni mbora kuliko kondoo wa makamo zaidi.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Mchinje huyo. Lakini kuchinja kama hivyo (ulivyofanya) haitotosheleza kwa mtu yeyote baada yako wewe.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 976 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 25
|
18-Mlango
باب الْعَلَمِ الَّذِي بِالْمُصَلَّى
Alama Ya Kwenye Muswallaa
|
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ سُفْيَانَ، قَالَ حَدَّثَنِي عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَابِسٍ، قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ، قِيلَ لَهُ أَشَهِدْتَ الْعِيدَ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ نَعَمْ، وَلَوْلاَ مَكَانِي مِنَ الصِّغَرِ مَا شَهِدْتُهُ، حَتَّى أَتَى الْعَلَمَ الَّذِي عِنْدَ دَارِ كَثِيرِ بْنِ الصَّلْتِ فَصَلَّى ثُمَّ خَطَبَ ثُمَّ أَتَى النِّسَاءَ، وَمَعَهُ بِلاَلٌ، فَوَعَظَهُنَّ وَذَكَّرَهُنَّ، وَأَمَرَهُنَّ بِالصَّدَقَةِ، فَرَأَيْتُهُنَّ يُهْوِينَ بِأَيْدِيهِنَّ يَقْذِفْنَهُ فِي ثَوْبِ بِلاَلٍ، ثُمَّ انْطَلَقَ هُوَ وَبِلاَلٌ إِلَى بَيْتِهِ.
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan Bin ‘Aabis (رضي الله عنه):
Ibn ‘Abbaas aliulizwa kama aliwahi kujiunga na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalaah ya ‘Iyd. Akajibu: “Naam! Na nisingejiunga naye pindi nisingekuwa mdogo. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka nje akaja hadi akafikia mahali penye alama ambayo ilikuwa karibu na nyumba ya Kathiyr bin As-Swalt, akaswalisha, akatoa Khutba, kisha akaenda kwa wanawake. Bilaal alifuatana naye. Aliwakhutubia wanawake akawatolea mawaidha na kuwakumbusha nasaha na akawaamuru watoe Swadaqah. Nikaona wanawake wale wanatoa mapambo yao kwa kunyoosha mikono yao na kuweka kwenye nguo ya Bilaal. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Bilaal wakarejea nyumbani.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 977 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 26
|
19-Mlango
باب مَوْعِظَةِ الإِمَامِ النِّسَاءَ يَوْمَ الْعِيدِ
Imaam Kuwatolea Mawaidha Wanawake Siku Ya ‘Iyd
|
حَدَّثَنِي إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ بْنِ نَصْرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، قَالَ حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي عَطَاءٌ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ سَمِعْتُهُ يَقُولُ قَامَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ الْفِطْرِ، فَصَلَّى فَبَدَأَ بِالصَّلاَةِ ثُمَّ خَطَبَ، فَلَمَّا فَرَغَ نَزَلَ فَأَتَى النِّسَاءَ، فَذَكَّرَهُنَّ وَهْوَ يَتَوَكَّأُ عَلَى يَدِ بِلاَلٍ وَبِلاَلٌ بَاسِطٌ ثَوْبَهُ، يُلْقِي فِيهِ النِّسَاءُ الصَّدَقَةَ. قُلْتُ لِعَطَاءٍ زَكَاةَ يَوْمِ الْفِطْرِ قَالَ لاَ وَلَكِنْ صَدَقَةً يَتَصَدَّقْنَ حِينَئِذٍ، تُلْقِي فَتَخَهَا وَيُلْقِينَ. قُلْتُ أَتُرَى حَقًّا عَلَى الإِمَامِ ذَلِكَ وَيُذَكِّرُهُنَّ قَالَ إِنَّهُ لَحَقٌّ عَلَيْهِمْ، وَمَا لَهُمْ لاَ يَفْعَلُونَهُ
Amesimulia Ibn Jurayj (رضي الله عنه):
’Atwaa aliniambia kuwa alimsikia Jaabir bin ’Abdillaah akisema: “Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama kuswalisha Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr. Akaanza kuwaswalisha kisha akatoa Khutba. Baada ya kumaliza akateremka chini (kutoka kwenye Mimbari), kisha akaenda kwa wanawake akawakumbusha nasaha huku akiegemea mkono wa Bilaal. Bilaal alikuwa katandaza nguo yake ambamo wanawake wale walikuwa wakiweka Swadaqah zao.” Nikamuuliza ’Atwaa iwapo hiyo ilikuwa ndiyo Zakaa yao ya Fitwr. Akajibu “Laa, hiyo ilikuwa Swadaqah tu iliyotolewa wakati ule. Mwanamke mmoja aliweka pete yake ya kidoleni, na wengine wakafanya vile vile.” Mimi nikamuuliza ’Atwaa kama Imaam anawajibika kuwanasihi wanawake mnamo siku ya ‘Iyd. Akajibu: “Bila shaka, ni wajibu wa Imaam kufanya hivyo. Kwa nini wao nao wasifanye hivyo?”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 978 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 27
|
قَالَ ابْنُ جُرَيْجٍ وَأَخْبَرَنِي الْحَسَنُ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ شَهِدْتُ الْفِطْرَ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ وَعُثْمَانَ ـ رضى الله عنهم ـ يُصَلُّونَهَا قَبْلَ الْخُطْبَةِ، ثُمَّ يُخْطَبُ بَعْدُ، خَرَجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَيْهِ حِينَ يُجْلِسُ بِيَدِهِ، ثُمَّ أَقْبَلَ يَشُقُّهُمْ حَتَّى جَاءَ النِّسَاءَ مَعَهُ بِلاَلٌ فَقَالَ يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ الآيَةَ ثُمَّ قَالَ حِينَ فَرَغَ مِنْهَا " آنْتُنَّ عَلَى ذَلِكَ ". قَالَتِ امْرَأَةٌ وَاحِدَةٌ مِنْهُنَّ لَمْ يُجِبْهُ غَيْرُهَا نَعَمْ. لاَ يَدْرِي حَسَنٌ مَنْ هِيَ. قَالَ " فَتَصَدَّقْنَ " فَبَسَطَ بِلاَلٌ ثَوْبَهُ ثُمَّ قَالَ هَلُمَّ لَكُنَّ فِدَاءٌ أَبِي وَأُمِّي، فَيُلْقِينَ الْفَتَخَ وَالْخَوَاتِيمَ فِي ثَوْبِ بِلاَلٍ. قَالَ عَبْدُ الرَّزَّاقِ الْفَتَخُ الْخَوَاتِيمُ الْعِظَامُ كَانَتْ فِي الْجَاهِلِيَّةِ.
Amesimulia Al-Hasan bin Muslim (رضي الله عنه)
Kutoka kwa Twaawus kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Nilihudhuria pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Abu Bakr, ‘Umar, na ’Uthmaan (رضي الله عنهم) katika kuswali Swalaah za ‘Iydul-Fitwr. Walikuwa wakiswali kwanza kabla ya kutoa Khutba ambayo waliitoa baada ya Swalaah. Safari moja nilimuona Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoka kuswali Swalaah ya ‘Iyd, nami kana kwamba namuona akiwapungia mikono akiwaashiria watu waketi. Naye, huku akifuatana na Bilaal, alikwenda nyuma akivuka Swaff za watu hadi alipowafikia wanawake. Akasoma:
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِاللَّـهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ ۙ فَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾
Ee Nabiy! Wakikujia Waumini wa kike wanafungamana nawe ahadi ya utiifu kwamba hawatomshirikisha Allaah na chochote, na wala hawatoiba, na wala hawatozini, na wala hawataua watoto wao, na wala hawatoleta usingiziaji wa kashfa walioizua baina ya mikono yao na miguu yao na wala hawatakuasi katika mema; basi pokea ahadi yao ya utiifu, na waombee maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Mumtahinah: 12]
Baada ya kumaliza kusoma Aayah hiyo, akasema: “Enyi wanawake! Mnatekeleza ahadi zenu?” Hakuna mwanamke isipokuwa mmoja tu alijibu Naam! Hasan hakumjua ni nani mwanamke huyo. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Basi toeni Swadaqah.” Bilaal akatandaza nguo yake akasema: “Endeleeni kutoa Swadaqah. Acha baba yangu na mama yangu wajotilee fidia maisha yao kwa ajili yenu (enyi wanawake).” Kwa hivyo wanawake wakaendelea kutoa Swadaqah zao za Fatkh (pete kubwa) na aina zingine za pete katika nguo ya Bilaal. ’Abdur-Razaaq akasema: “Fatkh ni pete kubwa ambayo ilikuwa ikivaliwa nyakati za ujahiliya (nyakati za ujinga kabla ya Uislamu).”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 979 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 28
|
20-Mlango
باب إِذَا لَمْ يَكُنْ لَهَا جِلْبَابٌ فِي الْعِيدِ
Endapo Mwanamke Hana Jilbaab (Shungi) La Kuvaa Wakati Wa ‘Iyd
|
حَدَّثَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَارِثِ، قَالَ حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ حَفْصَةَ بِنْتِ سِيرِينَ، قَالَتْ كُنَّا نَمْنَعُ جَوَارِيَنَا أَنْ يَخْرُجْنَ يَوْمَ الْعِيدِ، فَجَاءَتِ امْرَأَةٌ فَنَزَلَتْ قَصْرَ بَنِي خَلَفٍ فَأَتَيْتُهَا فَحَدَّثَتْ أَنَّ زَوْجَ أُخْتِهَا غَزَا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثِنْتَىْ عَشْرَةَ غَزْوَةً فَكَانَتْ أُخْتُهَا مَعَهُ فِي سِتِّ غَزَوَاتٍ. فَقَالَتْ فَكُنَّا نَقُومُ عَلَى الْمَرْضَى وَنُدَاوِي الْكَلْمَى، فَقَالَتْ يَا رَسُولَ اللَّهِ، عَلَى إِحْدَانَا بَأْسٌ إِذَا لَمْ يَكُنْ لَهَا جِلْبَابٌ أَنْ لاَ تَخْرُجَ فَقَالَ " لِتُلْبِسْهَا صَاحِبَتُهَا مِنْ جِلْبَابِهَا فَلْيَشْهَدْنَ الْخَيْرَ وَدَعْوَةَ الْمُؤْمِنِينَ ". قَالَتْ حَفْصَةُ فَلَمَّا قَدِمَتْ أُمُّ عَطِيَّةَ أَتَيْتُهَا، فَسَأَلْتُهَا أَسَمِعْتِ فِي كَذَا وَكَذَا قَالَتْ نَعَمْ، بِأَبِي ـ وَقَلَّمَا ذَكَرَتِ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم إِلاَّ قَالَتْ بِأَبِي ـ قَالَ " لِيَخْرُجِ الْعَوَاتِقُ ذَوَاتُ الْخُدُورِ ـ أَوْ قَالَ الْعَوَاتِقُ وَذَوَاتُ الْخُدُورِ شَكَّ أَيُّوبُ ـ وَالْحُيَّضُ، وَيَعْتَزِلُ الْحُيَّضُ الْمُصَلَّى، وَلْيَشْهَدْنَ الْخَيْرَ وَدَعْوَةَ الْمُؤْمِنِينَ ". قَالَتْ فَقُلْتُ لَهَا آلْحُيَّضُ قَالَتْ نَعَمْ، أَلَيْسَ الْحَائِضُ تَشْهَدُ عَرَفَاتٍ وَتَشْهَدُ كَذَا وَتَشْهَدُ كَذَا
Amesimulia Ayyuwb (رضي الله عنه):
Hafswah Bint Siriyn amesema: Siku ya ‘Iyd tulikuwa tukiwakataza watoto wetu wa kike kwenda kuswali Swalaah ya ‘Iyd. Mwanamke mmoja alikuja akakaa katika kasri ya Bani Khalaf nami nikaenda kwake. Akasema “Mume wa dada yangu alishiriki katika vita vitukufu kumi na mbili pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na dada yangu alikuwa pamoja na mume wake katika vita sita kati ya hivyo. Dada yangu amesema walikuwa wakiwauguza wagonjwa na na wakiwatibu majeruhi. Wakati mmoja aliuliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Iwapo mwanamke hana ushungi, kuna dhara yoyote ikiwa hatotoka nje siku ya ‘Iyd?” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mwenziwe anayefutana naye wachangie kuuvaa ushungi huohuo wake mmoja pamoja, na wanawake sharti washiriki katika matendo mema na mihudhurio ya da’wah za Waumini.” Hafswa akaongeza: Ummu ‘Atwiyyah alipokuja, nilimuendea nikamuuliza: Je ulisikia kitu chochote kuhusu fulani na fulani? Ummu ’Atwiyyah akasema: “Naam! Baba yangu atolewe fidia kwa ajili ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)!” Na kila alipolitaja jina la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kila mara alikuwa akisema: “Baba yangu afanywe fidia kwa ajili yake.” Akasema: “Watoke nje (kuhudhuria ‘Iyd katika Muswallaa) wasichana waliovunja ungo karibuni, wenye hedhi, na wanawali (au amesema; wasichana waliovunja ungo karibuni na wanawali - Ayyuwb hana hakika kama imetajwa hedhi). Na wanawake wenye hedhi sharti wakae mbali na uwanja wa Swalaah, lakini washuhudie kheri na du’aa ya Waislamu.” Hafswa akaongeza: Kuhusu hilo nilimuuliza Ummu ‘Atwiyyah: Je, pia wale wenye hedhi? Ummu ’Atiyya akajibu: “Naam, kwani nao si wanahudhuria kule ’Arafah na kwengineko?”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 980 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 29
|
21-Mlango
باب اعْتِزَالِ الْحُيَّضِ الْمُصَلَّى
Wanawake Wenye Hedhi Wasihudhurie Katika Muswallaa
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، قَالَ حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي عَدِيٍّ، عَنِ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ قَالَتْ أُمُّ عَطِيَّةَ أُمِرْنَا أَنْ نَخْرُجَ فَنُخْرِجَ الْحُيَّضَ وَالْعَوَاتِقَ وَذَوَاتِ الْخُدُورِ. قَالَ ابْنُ عَوْنٍ أَوِ الْعَوَاتِقَ ذَوَاتِ الْخُدُورِ، فَأَمَّا الْحُيَّضُ فَيَشْهَدْنَ جَمَاعَةَ الْمُسْلِمِينَ وَدَعْوَتَهُمْ، وَيَعْتَزِلْنَ مُصَلاَّهُمْ.
Amesimulia Ummu Atwiyyah (رضي الله عنها):
Tuliamriwa kutoka nje (kwa ajili ya ‘Iyd) na pia kuwachukua wanawake wenye hedhi na wasichana waliovunja ungo karibuni, na wanawali.” Ibn ’Awn amesema: “Wasichana waliovunja ungo karibuni, na wanawali. Ama wanawake wenye hedhi watashuhudia kheri na du’aa ya Waislamu lakini watajitenga kando na uwanja wa Swalaah.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth:
|
22-Mlango
باب النَّحْرِ وَالذَّبْحِ يَوْمَ النَّحْرِ بِالْمُصَلَّى
Al-Nahr Na Uchinjaji Wa Wanyama (Kama Kafara) Pale Muswallaa Mnamo Siku Ya An-Nahr
|
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، قَالَ حَدَّثَنِي كَثِيرُ بْنُ فَرْقَدٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَنْحَرُ أَوْ يَذْبَحُ بِالْمُصَلَّى.
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitekeleza Nahr (kuchinja Siku ya An-Nahr tarehe 10 Dhul-Hijjah baada ya Swalaah ya ‘Iyd) au akichinja katika Muswallaa (mnamo ‘Iydul-Adhwhaa).
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 982 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 31
|
23-Mlango
باب كَلاَمِ الإِمَامِ وَالنَّاسِ فِي خُطْبَةِ الْعِيدِ، وَإِذَا سُئِلَ الإِمَامُ عَنْ شَيْءٍ وَهْوَ يَخْطُبُ
Maongezi Ya Imaam Na Watu (Maamuma) Wakati Wa Khutba Ya ‘Iyd Na Imaam Akiulizwa Jambo Wakati Anatoa Khutba
|
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو الأَحْوَصِ، قَالَ حَدَّثَنَا مَنْصُورُ بْنُ الْمُعْتَمِرِ، عَنِ الشَّعْبِيِّ، عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، قَالَ خَطَبَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ النَّحْرِ بَعْدَ الصَّلاَةِ فَقَالَ " مَنْ صَلَّى صَلاَتَنَا وَنَسَكَ نُسْكَنَا فَقَدْ أَصَابَ النُّسُكَ، وَمَنْ نَسَكَ قَبْلَ الصَّلاَةِ فَتِلْكَ شَاةُ لَحْمٍ ". فَقَامَ أَبُو بُرْدَةَ بْنُ نِيَارٍ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَاللَّهِ لَقَدْ نَسَكْتُ قَبْلَ أَنْ أَخْرُجَ إِلَى الصَّلاَةِ، وَعَرَفْتُ أَنَّ الْيَوْمَ يَوْمُ أَكْلٍ وَشُرْبٍ فَتَعَجَّلْتُ وَأَكَلْتُ وَأَطْعَمْتُ أَهْلِي وَجِيرَانِي. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " تِلْكَ شَاةُ لَحْمٍ ". قَالَ فَإِنَّ عِنْدِي عَنَاقَ جَذَعَةٍ، هِيَ خَيْرٌ مِنْ شَاتَىْ لَحْمٍ، فَهَلْ تَجْزِي عَنِّي قَالَ " نَعَمْ، وَلَنْ تَجْزِيَ عَنْ أَحَدٍ بَعْدَكَ ".
Amesimulia Al-Baraa Bin ‘Aazib (رضي الله عنه):
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitukhutubia Siku ya An-Nahr baada ya Swalaah ya ‘Iyd akasema: “Yeyote aliyeswali kama sisi na akatekeleza Nusuk (kuchinja) kama sisi basi huwa katekeleza Nusuk (kafara ya kuchinja). Na yeyote anayechinja kabla ya Swalaah, basi hiyo itakuwa nyama ya kawaida (siyo kafara)” Abu Burdah bin Nayaar akasimama na kusema: “Ee Rasuli wa Allaah! Wa-Allaahi mimi nilichinja kabla ya kuswali Swalaah ya ‘Iyd kwa kudhani kuwa leo ni siku ya kula na kunywa (visivyokuwa vilevi). Kwa hivyo nikaharakisha kuchinja, nikala na kuilisha familia yangu na majirani.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Basi ile ilikuwa nyama tu ya kawaida ya kondoo (siyo kafara).” Kisha Abu Burdah akasema: “Ninaye mbuzi jike mdogo ambaye ni mzuri kuliko kondoo wawili. Je, huyo anaweza kunitosheleza kuwa ni kafara yangu?” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naam, lakini hatokuwa anatosheleza (kama kafara) kwa yeyote baada yako.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 983 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 32
|
حَدَّثَنَا حَامِدُ بْنُ عُمَرَ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ مُحَمَّدٍ، أَنَّ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ، قَالَ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلَّى يَوْمَ النَّحْرِ، ثُمَّ خَطَبَ فَأَمَرَ مَنْ ذَبَحَ قَبْلَ الصَّلاَةِ أَنْ يُعِيدَ ذَبْحَهُ فَقَامَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، جِيرَانٌ لِي ـ إِمَّا قَالَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ، وَإِمَّا قَالَ بِهِمْ فَقْرٌ ـ وَإِنِّي ذَبَحْتُ قَبْلَ الصَّلاَةِ وَعِنْدِي عَنَاقٌ لِي أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ شَاتَىْ لَحْمٍ. فَرَخَّصَ لَهُ فِيهَا.
Amesimulia Anas Bin Maalik (رضي الله عنه):
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswalisha siku ya An-Nahr halafu akatoa Khutba. Kisha akaamrisha kuwa yeyote aliyechinja kabla ya kuswali basi arudie kuchinja tena. Mtu mmoja kutoka miongoni mwa Answaariy akasimama na kusema: “Ee Rasuli wa Allaah! Kwa sababu ya majirani zangu, (aliwafafanua kuwa wao walikuwa mafukara au wahitaji sana), nimechinja kabla ya Swalaah, lakini ninaye mbuzi mdogo jike ambaye kwangu ni bora kuliko kondoo wawili.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akampa ruhusa kumchinja yule kama kafara.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 984 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 33
|
حَدَّثَنَا مُسْلِمٌ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنِ الأَسْوَدِ، عَنْ جُنْدَبٍ، قَالَ صَلَّى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ النَّحْرِ ثُمَّ خَطَبَ، ثُمَّ ذَبَحَ فَقَالَ " مَنْ ذَبَحَ قَبْلَ أَنْ يُصَلِّيَ فَلْيَذْبَحْ أُخْرَى مَكَانَهَا، وَمَنْ لَمْ يَذْبَحْ فَلْيَذْبَحْ بِاسْمِ اللَّهِ ".
Amesimulia Jundab (رضي الله عنه):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswalisha na siku ya An-Nahr akatoa Khutba kisha akachinja na akasema: “Yeyote aliyechinja ya kuswali na achinje mnyama mwingine kwa kulipizia huyo aliyechinjwa kabla ya Swalaah; na yule ambaye bado hajachinja basi achinje kwa
بِاسْمِ اللَّهِ ".
BismiLLaah juu yake.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 985 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 34
|
24-Mlango
باب مَنْ خَالَفَ الطَّرِيقَ إِذَا رَجَعَ يَوْمَ الْعِيدِ
Yeyote Aliyerudi (Baada Ya Kuswali Swalaah Ya ‘Iyd), Mnamo Siku Ya ‘Iyd, Kwa Kupitia Njia Tofauti Na Ile Aliyoendea
|
حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، قَالَ أَخْبَرَنَا أَبُو تُمَيْلَةَ، يَحْيَى بْنُ وَاضِحٍ عَنْ فُلَيْحِ بْنِ سُلَيْمَانَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا كَانَ يَوْمُ عِيدٍ خَالَفَ الطَّرِيقَ. تَابَعَهُ يُونُسُ بْنُ مُحَمَّدٍ عَنْ فُلَيْحٍ. وَحَدِيثُ جَابِرٍ أَصَحُّ.
Amesimulia Jaabir Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما):
Mnamo siku ya ‘Iyd, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akirejea (baada ya kuswali Swalaah ya ‘Iyd) kwa kupitia njia tofauti na ile aliyoendea (Muswallaa).
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 986 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 35
|
25-Mlango
باب إِذَا فَاتَهُ الْعِيدُ يُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ Anayeikosa Swalaah Ya ‘Iyd Aswali Rakaa Mbili
|
وَكَذَلِكَ النِّسَاءُ، وَمَنْ كَانَ فِي الْبُيُوتِ وَالْقُرَى لِقَوْلِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «هَذَا عِيدُنَا أَهْلَ الإِسْلاَمِ».
وَأَمَرَ أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ مَوْلاَهُمُ ابْنَ أَبِي عُتْبَةَ بِالزَّاوِيَةِ، فَجَمَعَ أَهْلَهُ وَبَنِيهِ، وَصَلَّى كَصَلاَةِ أَهْلِ الْمِصْرِ وَتَكْبِيرِهِمْ.
وَقَالَ عِكْرِمَةُ أَهْلُ السَّوَادِ يَجْتَمِعُونَ فِي الْعِيدِ يُصَلُّونَ رَكْعَتَيْنِ كَمَا يَصْنَعُ الإِمَامُ.
وَقَالَ عَطَاءٌ إِذَا فَاتَهُ الْعِيدُ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ.
Na hali kadhalika wanawake na wale ambao wako majumbani mwao na vijijini wafanye vivyo hivyo, kama inavyothibitishwa na kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hii ni ‘Iyd yetu enyi Waislamu.”
Na Anas Bin Maalik kule Az-Zaawiyah, alimuamuru mtumwa wake Ibn Abi ‘Utbah akusanye ahli zake na watoto wake (Anas). Anas (رضي الله عنه) akaongoza Swalaah ambayo ni sawa na ya watu wa mjini akatamka Takbiyrah kwa sauti iliyo sawa na yao.
‘Ikrimah amesema: “Wanavijiji sharti wakusanyike mnamo siku ya ‘Iyd na waswali Rakaa mbili kama anavyofanya Imaam.”
’Atwaa amesema: “Yeyote anayeikosa Swalaah ya ‘Iyd basi aswali Rakaa mbili.”
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ أَبَا بَكْرٍ ـ رضى الله عنه ـ دَخَلَ عَلَيْهَا وَعِنْدَهَا جَارِيَتَانِ فِي أَيَّامِ مِنًى تُدَفِّفَانِ وَتَضْرِبَانِ، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم مُتَغَشٍّ بِثَوْبِهِ، فَانْتَهَرَهُمَا أَبُو بَكْرٍ فَكَشَفَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَنْ وَجْهِهِ فَقَالَ " دَعْهُمَا يَا أَبَا بَكْرٍ فَإِنَّهَا أَيَّامُ عِيدٍ ". وَتِلْكَ الأَيَّامُ أَيَّامُ مِنًى. وَقَالَتْ عَائِشَةُ رَأَيْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَسْتُرُنِي، وَأَنَا أَنْظُرُ إِلَى الْحَبَشَةِ وَهُمْ يَلْعَبُونَ فِي الْمَسْجِدِ، فَزَجَرَهُمْ عُمَرُ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " دَعْهُمْ، أَمْنًا بَنِي أَرْفِدَةَ ". يَعْنِي مِنَ الأَمْنِ.
Amesimulia ‘Urwah (رضي الله عنه) Kutoka ‘Aaishah (رضي الله عنها):
Katika siku za Minaa (tarehe 11, 12, na 13 za Dhul-Hijjah), Abu Bakr alikuja kwake wakati wasichana wadogo wawili walikuwa wakipiga dufu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa kalala huku kafunikwa na nguo zake. Abu Bakr aliwakemea. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafunua uso wake na akamwambia Abu Bakr: “Waachie hao, kwani hizi ni siku za ‘Iyd na siku za Minaa.” ‘Aaishah akaendelea kusema: Wakati mmoja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa kanificha mimi nyuma yake nami nilikuwa natazama maonyesho ya Wahabashi Msikitini, ’Umar akawakemea. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Waache hao! Bani Arfidah! Endeleeni, ninyi mko katika amani.”
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 987, 988 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 36
|
26-Mlango
باب الصَّلاَةِ قَبْلَ الْعِيدِ وَبَعْدَهَا Kuswali Swalaah Kabla Au Baada Ya Swalaah Ya ‘Iyd
|
وَقَالَ أَبُو الْمُعَلَّى سَمِعْتُ سَعِيدًا عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ كَرِهَ الصَّلاَةَ قَبْلَ الْعِيدِ.
Abu Al-Mu’laa amesema: “Nimemsikia Sa’iyd kwamba Ibn ‘Abbaas hakupenda kuswali kabla ya Swalaah ya ‘Iyd.
حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، قَالَ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ حَدَّثَنِي عَدِيُّ بْنُ ثَابِتٍ، قَالَ سَمِعْتُ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ يَوْمَ الْفِطْرِ، فَصَلَّى رَكْعَتَيْنِ لَمْ يُصَلِّ قَبْلَهَا وَلاَ بَعْدَهَا وَمَعَهُ بِلاَلٌ.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka Siku ya ‘Iydul-Fitwr, akaswali Rakaa mbili (Swalaatul-‘Iyd) na hakuswali Swalaah yoyote nyingine kabla au baada yake, na wakati ule Bilaal alikuwa kafuatana naye.
Swahiyh Al-Bukhaariy: Hadiyth: 989 |
||
Mjalada: 2
|
Kitabu: 13
|
Hadiyth: 37
|