17-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Zakaah: Zakaah Ya Ng’ombe

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Zakaah

 

17-Zakaah Ya Ng’ombe

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Viwango Vya Ng’ombe Na Kiasi Cha Zakaah Yake

 

 

Toka kwa Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: ((Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinituma kwenda Yemen, na akaniamuru nichukue katika kila ng’ombe arobaini musinnah, na katika kila thelathini tabiy dume au jike)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (619), Abu Daawuwd (1561), An-Nasaaiy (5/26) na Ibn Maajah (1803)]

 

Idadi hii huwajumuisha nyati wa kufugwa pamoja na ng’ombe, kwa kuwa nyati hawa ni jamii ya ng’ombe kwa Ijma’a, na kwa hivyo hujumuishwa nao.

 

Na wewe unaona kuwa Hadiyth haikuainisha kiwango kidogo zaidi, lakini Jumhuri ya ‘Ulamaa wanasema kuwa hakuna Zakaah kwa ng’ombe chini ya 30. Wanapofikia 30, atatolewa tabiy dume au jike (jadha‘a dume au jike, na huyu ni mwenye mwaka mmoja), halafu kwa mujibu wa jedwali ifuatayo:

 

Idadi ya ng’ombe

 

Kiasi kilicho wajibu kutolewa

Kuanzia

Hadi

1

29

Hakuna Zakaah

30

39

Tabiy mmoja dume au jike. (Tabiy ni ndama aliyetimiza mwaka).

40

59

Musinnah mmoja. (Musinnah ni ng’ombe aliyetimiza miaka miwili).

60

69

Tabiy wawili

70

79

Tabiy mmoja na musinnah mmoja

80

89

Musinnah wawili

90

99

Tabiy watatu

100

109

Tabiy wawili na musinnah mmoja

 

Na hivi hivi kuendelea: kwa kila thelathini tabiy dume au jike, na kila arobaini musinnah.

 

Wakifikia 120, je wanakuwepo humo tabiy na musinnah? Inavyoonekana ni kuwa katika hali hii atachaguzwa baina ya kutoa tabiy wanne au musinnah watatu. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi. [Angalia Majmuw’u Al-Fataawaa]

 

 

Share