01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swiyaam: Taarifu Ya Swawm
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swiyaam
01-Taarifu ya Swawm
[Al-Lubaab (1/162), Al-Majmuw’u (6/248) na Al-Mughniy (3/84)]
الصيام و الصوم “Swiyaam” na “HAJJ” katika lugha ya kawaida ina maana ya kujishika na kujizuia na kitu, na hutumiwa katika kujizuia kwa aina zote. Allaah Ta’aalaa Akimzungumzia Maryam (‘Alayhas Salaam) Amesema:
(( إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا))
((Hakika mimi nimeweka nadhiri ya swawm [ya kutozungumza] kwa Ar-Rahmaan)). [Maryam (19: 26)]
Yaani, kunyamaza, kujishika na kujizuia na kunena.
Ama kisharia, ni kujizuia na vyenye kufunguza Swawm toka kuchomoza Alfajiri hadi jua kuchwa pamoja na niya ya kumfanyia ‘ibaadah Allaah Ta’aalaa.