Kababu Za Kuku Katika Sosi Ya Nyanya
Kababu Za Kuku Katika Sosi Ya Nyanya
Vipimo Vya Kababu
Kidari cha kuku - 1 kilo
kitunguu saumu(thomu/galic)na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Kitunguu kilichokatwa vipande vidogo - 1
Pilipili mbichi - 1
Pilipili manga - 1 kijiko cha chai
Bizari upendayo - 1 kijiko cha chai
Siki - 1 kijiko cha supu
Mayai - 4 – 5
Mafuta - Kiasi ya kukaangia
Sosi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Vitunguu vilivyokatwa (chopped) - 2
Nyanya zilizosagwa - 3
Nyanya ya kopo - 1
Pilipili manga - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Kotmiri iliyokatwa (chopped)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kababu
- Chemsha kidari cha kuku kwa siki, thomu, kitunguu kilichosagwa, pilipili mbichi bizari zote na kufunika kipikike bila ya maji hadi kikauke.
- Tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage bila ya kuta maji, kitasagika wenyewe.
- Tia katika bakuli na upige mayai na kuchanganya. Mchanganyiko uwe unaweza kufanya viduara vya kababu. Kama umekuwa laini ongeza mayai.
- Katika karai tia mafuta kiasi kidogo tu ya kuweza kugeuza geuza kababu zipikike.
- Epua na weka katika sufuria.
Sosi
- Kaanga vitunguu kisha tia nyanya, nyanya ya kopo, pilipili manga, chumvi na endelea kukaanga iwe sosi.
- Tia kotmiri, kisha mwagia katika sufuria iliyokuwemo kababu.
- Pika katika moto mdogo kababu zitokote kidogo hadi ziwive vizuri.
- Epua na pakua katika bakuli, mwagia kotmiri kidogo.