11-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْعَلِيمُ - الْخَبِيرُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْعَلِيمُ - الْخَبِيرُ

 

 

 

 

الْعَلِيمُ

Al-‘Aliym

Mjuzi Wa Yote Daima

 

 

الْخَبِيرُ

Al-Khabiyr

Mjuzi Wa Undani Na Kina Cha Mambo,

Mwenye Ujuzi Wa Ya Dhahiri Na Ya Siri

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى), Yeye Ndiye Ambaye elimu Yake inazunguka mambo yote ya dhahiri na yaliyojificha, ya wazi na ya siri, mambo yote yanayolazimika kutukia, mambo yasiyowezekana kutukia na mambo ambayo huenda yakatukia. Anayajua mambo ya viumbe wote, yaliyopita, ya sasa na ya baadaye. Kwa hakika, hakuna kilichofichikana dhidi Yake.

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Hakika Allaah Ana elimu ya Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi, na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqman (31):34]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ﴿١٣﴾

Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana namwanamme na mwanamke, na Tukakujaalieni  mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye na hadhi zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni mwenye taqwa zaidi kati yenu. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Hujuraat (49): 13]

 

 

 

Share