29-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْقَدِيرُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْقَدِيرُ
الْقَدِيرُ Al-Qadiyr Muweza Wa Yote Daima
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Mwenye nguvu timilifu na kamilifu na uwezo. Kwa nguvu Zake Amefanya kila kitu kiwepo. Kwa nguvu hiyo Yeye hupanga kila kitu. Kwa nguvu hiyo, Ameumba na kukamilisha uumbaji. Kwa nguvu hiyo, Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Huhuisha na kufisha. Kwa nguvu hiyo Atafufua waja kwa ajili ya jazaa yao; kuwapa malipo waliofanya mema na kuwaingiza Motoni kwa waliotenda uovu. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye, Anapotaka jambo liwe huliambia tu:
كُن فَيَكُونُ
Kun! basi (jambo) huwa!
Kwa nguvu Zake Allaah (سبحانه وتعالى) na uwezo, hugeuza nyoyo na kuzielekeza kwa yeyote Amtakaye.
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٤٨﴾
Na kila mmoja ana upande wa kuuelekea. Basi shindaneni kwenye mambo ya khayr. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja (Qiyaamah). Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-Baqarah (2): 148]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾
Ulipokusibuni msiba ingawa mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo ni kutoka kwenu wenyewe. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. [Aali ‘Imraan (3): 165]