33-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْحَافِظُ - الْحَفِيظُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْحَافِظُ - الْحَفِيظُ
الْحَافِظُ Al-Haafidhw Mwenye Kuhifadhi, Kulinda
|
الْحَفِيظُ Al-Hafiydhw: Mwenye Kuhifadhi, Kulinda
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayehifadhi na kutunza Alivyoviumba na Ambaye elimu Yake inavizunguka vyote Alivyovifanya viwepo. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewahifadhi marafiki Zake dhidi ya kuangukia katika madhambi na mambo ya hilaki. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Aliye Mkarimu kwao katika nyakati za harakati na mapumziko. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayehesabu amali za waja na malipo yao.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُ فَاتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٠﴾
Na kwa yakini Ibliys alisadikisha dhana yake juu yao, basi walimfuata isipokuwa kundi miongoni mwa Waumini.
وَمَا كَانَ لَهُ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِالْآخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِي شَكٍّ ۗ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ ﴿٢١﴾
Na yeye (Ibliys) hakuwa ana madaraka yoyote juu yao isipokuwa ili Tujue ni nani yule anayeamini Aakhirah na nani yule anayeitilia shaka. Na Rabb wako ni Mwenye kuhifadhi kila kitu. [Sabaa (34): 20-21]
Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) :
قَالَ هَلْ آمَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَا أَمِنتُكُمْ عَلَىٰ أَخِيهِ مِن قَبْلُ ۖ فَاللَّـهُ خَيْرٌ حَافِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٦٤﴾
Akasema: Je, nimwaminishe kwenu ila kama nilivyokuaminini juu ya kaka yake kabla? Basi Allaah ni Mbora wa wenye kuhifadhi. Naye ni Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu. [Yuwsuf (12): 64]