40-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْفَتَّاحُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْفَتَّاحُ

 

 

الْفَتَّاحُ

Al-Fattaah

Mwingi Wa Kufungua, Kuhukumu

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Atakayewahukumu waja Wake kwa taratibu Zake za Shariy’ah. Taratibu Zake za amri na za jazaa. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewafumbua macho wale walio wakweli na niya safi kupitia ukarimu Wake. Allaah (عز وجل) ni Pekee Anayewafungua nyoyo zao ili waweze kumjua Yeye, wampende na watubu Kwake. Yeye hufungua milango ya Rahmah na rizki kwa waja Wake na Anawapa njia za kupata vyote viwili, mema ya humu duniani na Aakhirah.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَّا يَفْتَحِ اللَّـهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا ۖ وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢﴾

Rahmah yoyote Anayoifungua Allaah kwa watu, basi hakuna wa kuizuia, na Anayoizuia, basi hakuna wa kuipeleka baada Yake, Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Faatwir (35): 2]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ يَجْمَعُ بَيْنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفْتَحُ بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَهُوَ الْفَتَّاحُ الْعَلِيمُ ﴿٢٦﴾

Sema: Rabb wetu Atatukusanya, kisha Atahukumu baina yetu kwa haki, Naye Ndiye Hakimu, Mjuzi wa yote. [Sabaa (34): 26]

 

Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِي كَذَّبُونِ ﴿١١٧﴾

Akasema: Rabb wangu! Hakika watu wangu wamenikadhibisha.

 

فَافْتَحْ بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾

Basi Hukumu baina yangu na baina yao hukumu (Yako), na Uniokoe mimi na wale walio pamoja nami miongoni mwa Waumini. [Ash-Shu’araa (26):  117-118]

 

 

 

 

 

Share