42-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْحَكَمُ - الْعَدْلُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْحَكَمُ - الْعَدْلُ
الْحَكَمُ Al-Hakam Hakimu Mwadilifu Wa Haki Zaidi Kuliko Wote
|
الْعَدْلُ Al-‘Adl Mwadilifu Kuliko Wote
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewahukumu waja Wake humu duniani na Aakhirah kwa haki na uadilifu wake. Hatamdhulumu yeyote hata kwa uzito wa chembe ndogo kabisa ya hardali, na hakuna atakayebebeshwa mzigo wa mwingine. Hakuna mja atakayezidishiwa adhabu kuliko dhambi yake, atapewa anachostahiki tu. Hakuna haki ya mtu hata mmoja atakayonyimwa. Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Mwadilifu katika Shariy’ah na amri Zake.
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنِّي تَوَكَّلْتُ عَلَى اللَّـهِ رَبِّي وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَابَّةٍ إِلَّا هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٦﴾
Hakika mimi nimetawakali kwa Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakuna kiumbe chochote kitembeacho isipokuwa Yeye (Allaah) Anamkamata kwa kipaji chake. Hakika Rabb wangu Yuko juu ya njia iliyonyooka. [Huwd (11): 56]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧﴾
Sema: Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anasimulia ya haki; Naye ni Mbora wa wenye kuamua hukumu. [Al-An’aam (6): 57]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾
Je, kwani Allaah Si Mwadilifu zaidi wa wanaohukumu kuliko mahakimu wote? [At-Tiyn (95): 8]