45-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: النُّورُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

النُّورُ

 

 

النُّورُ

An-Nuur

Mwenye Nuru, Mwanga

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Ana Nuru ya mbingu na dunia, ni Pekee Anayetia Nuru nyoyo za wanaomkhofu kwa ‘ilmu bila ya kumuona, bali wanamwamini na kutaraji mwongozo Wake. Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Aliyewasha angani na ardhini taa Alizoweka humo. Kizuizi Chake ni Nuru, na kama Angelikiondoa, basi Utukufu mkubwa na ubora wa Dhati Yake ingeunguza kila kiumbe ambacho uoni wake umekiangukia.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ ۖ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ ۖ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ مُّبَارَكَةٍ زَيْتُونَةٍ لَّا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ ۚ نُّورٌ عَلَىٰ نُورٍ ۗ يَهْدِي اللَّـهُ لِنُورِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣٥﴾

Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa Nuru Yake kama shubaka ndani yake mna taa yenye mwanga mkali. Taa hiyo yenye mwanga mkali iko katika (tungi la) gilasi. Gilasi hiyo ni kama kwamba nyota inayong’aa na kumeremeta, inawashwa kutokana na mti wa baraka wa zaytuni, hauko Mashariki wala Magharibi. Yanakaribia mafuta yake yang’ae japokuwa moto haujayagusa; Nuru juu ya Nuru. Allaah Anamwongoza kwa Nuru Yake Amtakaye. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu. Na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.   [An-Nuwr (24): 35]

 

 

 

 

 

 

Share