57-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الأَوَّلُ - الآَخِرُ - الظَّاهِرُ - الْبَاطِنُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الأَوَّلُ - الآَخِرُ - الظَّاهِرُ - الْبَاطِنُ

 

 

 

الأَوَّلُ

Al-Awwal

Wa Kwanza Bila Mwanzo

 

 

الآَخِرُ

Al-Aakhir

Wa Mwisho, Hapana Kitu Baada Yake

 

 

الظَّاهِرُ

Adhw-Dhwaahir

Dhahiri Kwa Vitendo Vyake

 

 

الْبَاطِنُ

Al-Baatwin 

Asiyeonekana Na Viumbe

 

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameyaelezea Majina haya kwa maneno mafupi na dhahiri akisema:

 

 اللهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَليْسَ قَبْلكَ شيء، وَأَنْتَ الآخِرُ فَليْسَ بَعْدَكَ شيء، وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَليْسَ فَوْقَكَ شيء، وَأَنْتَ البَاطِنُ فَليْسَ دُونَكَ شيء، اقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَاغْنِنَا مِنَ الفَقْرِ

Ee Allaah, Wewe wa Awali hivyo basi hakuna kitu kabla Yako, Nawe ni wa Mwisho, basi hakuna kitu baada Yako, Nawe Uko juu kabisa hakuna kitu juu yako, Nawe uko karibu kabisa, hakuna kitu kilicho karibu kuliko Wewe, Nikidhie deni langu na nitosheleze kutokana na ufakiri. [Muslim]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾

Yeye Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yake, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yake, na Aliye juu kabisa hakuna kitu juu Yake, na Aliye karibu kabisa, hakuna kitu kilicho karibu kuliko Yeye, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.  [Al-Hadiyd (57): 3]

 

 

 

Share