67-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُبِينُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْمُبِينُ
الْمُبِينُ Al-Mubiyn Mwenye Kubainisha
|
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَوْمَئِذٍ يُوَفِّيهِمُ اللَّـهُ دِينَهُمُ الْحَقَّ وَيَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ الْمُبِينُ ﴿٢٥﴾
Siku hiyo Allaah Atawalipa kikamilifu malipo yao ya haki; na watajua kwamba Allaah Ndiye wa Haki, Mwenye kubainisha. [An-Nuwr (24): 25]