69-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُقْتَدِرُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْمُقْتَدِرُ
الْمُقْتَدِرُ Al-Muqtadir Mwenye Uwezo Wa Juu Kabisa
|
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ﴿٤٥﴾
Na wapigie mfano wa uhai wa dunia kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika kwayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha yakawa makavu yaliyovurugika yanapeperushwa na upepo. Na Allaah daima ni Mwenye Uwezo wa juu kabisa kwa kila kitu. [Al-Kahf (18): 45]