Vipi Uweze Kuhifadhi Qur-aan? (كَيْفَ تَحْفَظُ الْقُرآن)

 

 

Vipi Uweze Kuhifadhi Qur-aan?

 

كَيْفَ تَحْفَظُ الْقُرآن؟

 

 

 

Imekusanywa Na: Ummu Iyyaad

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

 

01- Utangulizi

 

02- Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

 

03- Umri Bora Wa Kuhifadhi Qur-aan

 

04- Nasaha Za Kuhifadhi Qur-aan

 

05- Utaratibu Wa Kuhifadhi Qur-aan

 

06- Zingatia Aayah Zinazoshabihiana (Aayaat Al-Mutashaabihaat)

 

07- Kuithibitisha Qur-aan Baada Ya Kuihifadhi

 

08- Hitimisho

 

 

 

 

01-Utangulizi:

 

 

Qur-aan ni maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى), Aliyopelekewa Wahyi Nabiy Muhammad kupitia Jibriyl ‘alayhis-salaam, akawasomea Swahaba, nao wakawasomea waliofuatia, ikaendelea kusomwa na kufundishwa hadi kutufikia sisi.  Qur-aan ni Mwongozo wetu na Nuru inayonawirisha nyoyo zetu. Qur-aan ni kamba nene inayounganisha Waislamu, ni miyzani ya uadilifu, ni shifaa ya moyo ya kila aina ya maradhi; maradhi ya kufru, shirki, unafiki, uhasidi, uchoyo na ni kinga ya kila aina ya maasi na maovu. Imejaa hikma katika Aayah zake na Shariy’ah zake ambazo zinamfaa bin-Aadam wakati wowote, zama zote, na popote alipo. Amri na makatazo Yake Allaah (سبحانه وتعالى) humo pamoja na kumtii Rasuli Wake ni sababu ya furaha na kufaulu kwa bin Aadam katika dunia yake na Aakhirah yake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾ قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٥٨﴾

Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwa Rabb wenu, na shifaa ya yale yaliyomo vifuani, na mwongozo na rahmah kwa Waumini. Sema: Kwa fadhila za Allaah na kwa rahmah Yake basi kwa hayo wafurahi. Hayo ni khayr kuliko wanayoyakusanya. [Yuwnus (10: 57-58)]

 

 

Lakini manufaa na fadhila hizo haziwezi kumfikia mtu isipokuwa kwa atakayeisoma Qur-aan kwa njia itakayomridhisha Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema: 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ

Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake; hao ndio wanaokiamini. [Al-Baqarah (2: 121)]

 

Kitabu hiki In Shaa Allaah, kitaweza kumsaidia anayetaka kuhifadhi Qur-aan pindi mtu atakapoweka azimio la nguvu na kuanza kwanza Niya safi moyoni mwake na kuomba du’aa, pia kufanya juhudi kubwa ya kuendelea nayo Hifdhi yake bila ya kukata tamaa na kuithibitisha Qur-aan baada ya kuihifadhi. Hapo ndipo itakapomthibitikia kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) iliyokariri mara nne katika Suwratul-Qamar:

 

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿١٧﴾

Na kwa yakini Tumeiwepesisha Qur-aan kwa kuikumbuka, basi je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika? [Al-Qamar: (54: 17, 22, 32, 40)]

 

 

Namuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Ajaalie kazi hii iwe kwa ajili ya kupata Radhi Zake Pekee na Ajaalie iwe yenye manufaa kwa ndugu zetu wa Kiislamu na namuomba Atughufurie na Atusamehe kwa makosa yoyote yatakayokuwemo. 

 

وَصَلَّ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّنا مُحَمَّدٍ وَعَلى آلِهِ وَاَصْحَابِهِ وَسَلَّمَ تَسْلِيماً  كَثِيراً

 

Ummu Iyyaad

20 Rabiy’ul-Awwal 1434 (2 Februari 2003)

Kimehaririwa 18 Swafar 1442H (5 Oktoba 2020)

 

02- Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Amewafanyia Ihsaan kubwa Waumini kwa kuwaletea Maneno Yake Mwenyewe kupitia kwa Rasuli Wake kama Anavyosema:

 

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾

Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah); japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. [Aal-‘Imraan: 164]

 

 

Na ihsaan na fadhila hiyo inatokana na du’aa ya baba wa Manabii ambaye ni Nabiy Ibraahiym (عليه السلام), ambaye aliomba baada ya kujenga Al-Ka’bah:

 

رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾

Rabb wetu, wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Baqarah: (2:  129)]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾

Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah (Sunnah), na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua. [Al-Baqarah (2: 151)]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢﴾

 

Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa wasiojua kusoma wala kuandika miongoni mwao anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu na Hikmah na japo walikuwa hapo kabla katika upotofu bayana. [Al-Jumu’ah (62: 2)]

 

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akaendelea kumuamrisha Rasuli Wake aisome Qur-aan katika Aayah zifuatazo: 

 

إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَـٰذِهِ الْبَلْدَةِ الَّذِي حَرَّمَهَا وَلَهُ كُلُّ شَيْءٍ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩١﴾ وَأَنْ أَتْلُوَ الْقُرْآنَ ۖ

Hakika nimeamrishwa nimwabudu Rabb wa mji huu Ambaye Ameufanya mtukufu, na ni Vyake Pekee vitu vyote. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu. Na kwamba nisome Qur-aan [An-Naml: (27:  91-92)]

 

Na pia:

 

اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ

Soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyoletewa Wahy katika Kitabu na simamisha Swalaah. [Al-‘Ankabuwt (29:  45)]

 

 

Nabiy akawasomea Sahaba zake nao wakaendeleza kuisoma na kuifundisha hadi kuwafikia Waumini wa zama zote.  

 

Kuisikiliza au kuisoma Qur-aan   kunampelekea msikilizaji au msomaji kuhisi kuwa anasemeshwa na Muumba wake.  Hili ndilo linaloipa Qur-aan daraja na nafasi isiyokadirika kwa Muumini, kwani Muumini khasa ni yule anayeamini kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah yaliyoteremshwa kwa Nabiy Muhammad kupitia kwa Jibril (عليه السلام) na kwamba kusomwa kwake ni ‘ibaadah.

 

 

Fadhila za kusoma, kuhifadhi na kuisikiliza Qur-aan ni nyingi kama zilivyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Vitabu na makala nyingi zimeandikwa kuhusiana na hilo; zifuatazo ni baadhi ya fadhila zake:

 

 

i-Kuisoma Qur-aan Ni Biashara Isiyofilisika, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾ لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾

Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea. Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Faatwir (35: 29-30)]

 

 

ii-Mwenye Kujifundisha Kisha Akaifundisha Naye Ni Mbora Miongoni Mwa Waumini:

 

 

Bila shaka jambo lenye ubora, au uzuri wa kitu, huthibiti kwa sababu hii au ile au kwa kufungamana na mwenye hicho kitu; na ubora au uzuri wa Qur-aan ni kwa kuwa ni Maneno ya Aliyembora kabisa; na kuna ubora gani ulimwengu huu kuliko mtu kujifunza au  kufundisha Maneno ya Allaah; jambo alilolianza  mwalimu aliyebora kuliko wote hapa duniani ambaye ni Nabiy . Hivyo hakuna kazi wala amali iliyobora kuliko ile kazi au amali aliyoifanya Nabiy ambayo ni kusoma na kuisomesha Qur-aan kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

 

 عَنْ عُثْمَانَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((خَيْرُكُمْ مَنْ تَعَلَّمَ الْقُرْآنَ وَعَلَّمَهُ)) 

Imepokelewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy amesema: ((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhy, An-Nasaaiy, Abu Daawuwd, Ahmad ]

 

 

 

iii-Kuisoma Qur-aan Ni Kuchuma Thawabu Kwa Kila Herufi Moja:

 

 

Kuisoma au kuisomesha Qur-aan ni ‘ibaadah kama ilivyotangulia; na ni ‘ibaadah yenye malipo makubwa kama itafungamana na sharti mojawapo katika masharti ya ‘ibaadah katika Uislamu; nayo ni    ikhlaasw (Niya safi kwa ajili ya Allaah). Hivyo mwenye kuisoma Qur-aan kwa ikhlaasw huwa ana matarajio ya malipo kama haya yaliyothibiti katika Hadiyth ya ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Nabiy amesema:

 

((مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللَّهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا لَا أَقُولُ الم حَرْفٌ وَلَكِنْ أَلِفٌ حَرْفٌ وَلَامٌ حَرْفٌ وَمِيمٌ حَرْفٌ))

((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata hasanah [jema] moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja)) [At-Tirimidhiy]

 

 

iv-Mwenye Kufungamana Na Qur-aan Huwa Ni Miongoni Mwa Watu Wake Allaah (سبحانه وتعالى) Walio Karibu Naye Na Awapendao:

 

 

Qur-aan kama tuaminivo ni Maneno ya Allaah, hivyo mwenye kushikamana nayo huwa ni miongoni mwa watu Wake Allaah Anaowapenda. Imethibiti hili katika Hadiyth ifuatayo: 

 

 عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ:  ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik  (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah amesema:  ((Allaah Ana watu wake (makhsusi) kati ya wanaadamu)) Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah,  hao ni akina nani? Akasema: ((Hao ni watu wa Qur-aan na ni watu wa Allaah wateule Wake (Awepandao))) [Ahmad, Ibn Maajah] 

 

 

 

v-Mwenye Kuisoma Kwa Mashaka  Hupata Thawabu Mara Mbili Yake:

 

 

Nabiy hakutaka Waislamu wakate tamaa au waache mara moja kuisoma au kujifunza Qur-aan; huenda kutokana na sababu ya kutokuwa na lafdhi ya lugha ya Kiarabu kwa wasiokuwa na asili ya Kiarabu au kwa sababu ya uzito wa ulimi na akili hivyo basi ikawa ni shida kwa mtu huyo kuisoma kwa kudodosa dodosa.  Basi Nabiy aliwatia nguvu Waislamu kwa kuwahakikishia kuwa malipo msomaji anayesumbuka kujifunza na kuisoma Qur-aan ni mara mbili: 

 

 عَنْ عَائِشَةَ قَالَتْ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ))  

Imepokelewa kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Rasuli wa Allaah amesema: ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah, watukufu, wema. Na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

vi-Harufu Nzuri Na Ladha Nzuri Kwa Anayeisoma Qur-aan:

 

 

Nabiy ametofautisha mfano wa Muumini anayesoma na asiyesoma Qur-aan katika Hadiyth ifuatayo: iliyopokelewa toka kwa

 

Kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه): kwamba Nabiy amesema:

 

 ((مَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ الْأُتْرُجَّةِ رِيحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا طَيِّبٌ وَمَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي  لَا يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ التَّمْرَةِ لَا رِيحَ لَهَا وَطَعْمُهَا حُلْوٌ))  

 ((Mfano wa Muumini ambaye anayesoma Qur-aan ni kama tunda la Utrujjah;  harufu yake nzuri na ladha yake nzuri. Na mfano wa Muumini asiyesoma Qur-aan mfano wake kama tende zisizokuwa na harufu lakini zina ladha tamu))

 

 

Utrujjah: Tunda linalofanana na ndimu lenye rangi ya orenji inayokaribia rangi ya dhahabu, linajulikana kama tufaha la ki-Ajemi. Lina harufu nzuri kabisa.

 

 

vii-Qur-aan Ni Shafaa’ah (Kiombezi) Siku Ya Qiyaamah:

 

 

Mwenye kupenda kutafuta marafiki na maswahiba wa kweli na wakumfaa basi afanye usahiba na Qur-aan kwa sababu haitamtupa kamwe    swahiba wake wakati wa shida na fazaa za Siku Ya Qiyaamah: 

 

 

عن أبي أُمَامَةَ الْبَاهِلِيُّ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لِأَصْحَابِهِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliyy (رضي الله عنه) ambaye amesema: “Nimemskia Rasuli wa Allaah akisema: ((Someni Qur-aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah ikimuombea aliyekuwa swahiba wake [mwenye kuisoma])) [Muslim]

 

 

 

viii-Qur-aan Humnyanyua Na Kumpandisha Daraja Mwenye Kushikamana Nayo:

 

 

 

قَالَ عُمَرُ أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ)) 

'Umar (رضي الله عنه) amesema: “Nabiy wenu amesema: ((Allaah Atawanyanyua baadhi ya watu kwa kitabu hiki [Qur-aan] na Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki)) [Muslim Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

ix-Qur-aan Humpandisha Mtu Daraja Ya Jannah:

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((يُقَالُ لِصَاحِبِ الْقُرْآنِ اقْرَأْ وَارْتَقِ وَرَتِّلْ كَمَا كُنْتَ تُرَتِّلُ فِي الدُّنْيَا فَإِنَّ مَنْزِلَتَكَ عِنْدَ آخِرِ آيَةٍ تَقْرَأُ بِهَا))

 

Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Umar   (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy amesema: ((Huambiwa swahiba wa Qur-aan [aliyeshikamana na Qur-aan]: “Soma na panda [juu katika daraja za Pepo]  na uisome kwa 'Tartiyl' [ipasavyo kwa tajwiyd] kama ulivyokuwa ukiisoma ulipokuwa duniani, kwani makazi yako ni pale utakapofika katika Aayah ya mwisho utakayoisoma))  [At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

 

x-Huteremka Malaika Kwa Utulivu Na Rahmah Kwa Wanaosoma Qur-aan:

 

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلَّا نَزَلَتْ عَلَيْهِمْ السَّكِينَةُ وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَحَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ)) 

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah amesema ((Hawakusanyiki pamoja watu katika miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma kitabu cha Allaah, na wanafundishana baina yao, ila huwateremkia utulivu na hufunikwa na Rahmah na Malaika huwazunguka na Allaah Anawataja mbele ya [Malaika] aliokuwa nao)) [Muslim Abu Daawuwd, Ibn Maajah , Ahmad]

 

 

Pia,

 

عن أُسَيْدَ بْنَ حُضَيْرٍ بَيْنَمَا هُوَ لَيْلَةً يَقْرَأُ  فِي ِرْبَدِهِ، إِذْ جَالَتْ فَرَسُهُ، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أُخْرَى،  فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا. قَالَ أُسَيْدٌ:  "فَخَشِيتُ أَنْ تَطَأَ يَحْيَى فَقُمْتُ إِلَيْهَا فَإِذَا مِثْلُ الظُّلَّةِ فَوْقَ رَأْسِي فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". قَالَ: "فَغَدَوْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ بَيْنَمَا أَنَا الْبَارِحَةَ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ أَقْرَأُ فِي مِرْبَدِي إِذْ جَالَتْ فَرَسِي". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ:  "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَانْصَرَفْتُ وَكَانَ يَحْيَى قَرِيبًا مِنْهَا خَشِيتُ أَنْ تَطَأَهُ، فَرَأَيْتُ مِثْلَ الظُّلَّةِ فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تِلْكَ الْمَلَائِكَةُ كَانَتْ تَسْتَمِعُ لَكَ وَلَوْ قَرَأْتَ لَأَصْبَحَتْ يَرَاهَا النَّاسُ مَا تَسْتَتِرُ مِنْهُمْ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Usayd bin Khudhwayr, kwamba alipokuwa akisoma akiwa katika mirbad[1] yake akashtuka farasi wake. Akasoma, kisha    akashtuka   tena, akasoma kisha akashtuka tena. Akasema Usayd: Nikaogopa asije kumkanyaga Yahya (mwanawe). Nikainuka kumwendea (farasi) nikaona kitu kama kivuli juu ya kichwa changu kama kina kandili kikipanda mbinguni hadi kikapotea. Nikamwendea Rasuli wa Allaah siku ya pili nikwamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah! Jana usiku nilipokuwa katika mirbad yangu nikisoma Qur-aan, farasi wangu alishtuka!  Rasuli wa Allaah akasema: ((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah akasema: ((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah akasema ((Soma Ibn Khudhwayr)). Akasema niliondoka kwani Yahya alikuwa karibu naye, nikahofu asimkanyage. Nikaona kama kivuli kikiwa na taa kinapanda juu hadi kikapotea. Akasema Rasuli wa Allaah : ((Hao ni Malaika walikuwa wakikusikiliza, lau ungeliendelea kusoma hadi asubuhi watu wangelikiona kisingelipotea)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

xi-Kuhifadhi Na Kujifunza Maana Ya Qur-aan Ni Bora Kuliko Mapambo Ya Dunia:

 

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِي الصُّفَّةِ فَقَالَ: ((أَيُّكُمْ يُحِبُّ أَنْ يَغْدُوَ كُلَّ يَوْمٍ إِلَى بُطْحَانَ أَوْ إِلَى الْعَقِيقِ فَيَأْتِيَ مِنْهُ بِنَاقَتَيْنِ كَوْمَاوَيْنِ فِي غَيْرِ إِثْمٍ وَلَا قَطْعِ رَحِمٍ؟)) فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ نُحِبُّ ذَلِكَ قَالَ: ((أَفَلَا يَغْدُو أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَسْجِدِ فَيَعْلَمُ أَوْ يَقْرَأُ آيَتَيْنِ مِنْ كِتَابِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ خَيْرٌ لَهُ مِنْ نَاقَتَيْنِ وَثَلَاثٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ ثَلَاثٍ وَأَرْبَعٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَرْبَعٍ وَمِنْ أَعْدَادِهِنَّ مِنْ الْإِبِلِ))

Imepokelewa toka kwa 'Uqbah bin 'Aamir(رضي الله عنه)   ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah alitujia wakati tulikuwa katika Swuffah[2] akauliza: ((Kuna yeyote miongoni mwenu anayetaka kwenda soko la Butw-haan[3] au [soko] la Al-'Aqiyq[4] na akapata humo ngamia wawili wakubwa na waliyonona bila ya kutenda dhambi au kukata undugu?)) Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata hivyo. Kisha akasema: ((Basi aende mmoja wenu msikitini akajifunze au asome Aayah mbili katika kitabu cha Allaah عزوجل basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia wawili. Na Aayah tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa ngamia)) [Muslim, Abu Daawuwd, Ahmad]

 

 

 

X2-Mwenye Kuhifadhi Qur-aan Huvalishwa Taji Siku Ya Qiyaamah:

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَجِيءُ الْقُرْآنُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ يَا رَبِّ حَلِّهِ،  فَيُلْبَسُ تَاجَ الْكَرَامَةِ ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ زِدْهُ، فَيُلْبَسُ حُلَّةَ الْكَرَامَةِ ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ ارْضَ عَنْهُ فَيَرْضَى عَنْهُ فَيُقَالُ لَهُ: اقْرَأْ وَارْقَ.  وَتُزَادُ بِكُلِّ آيَةٍ حَسَنَةً))  

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba, Rasuli wa Allaah amesema: ((Qur-aan itakuja siku ya Qiyaamah na itasema: “Ee Rabb, Mpambe” [Mwenye kuhifadhi Qur-aan]. Kisha atavalishwa taji. Kisha [Qur-aan] itasema: “Ee Rabb, muongeze”. Kisha huyo mtu atavishwa nguo ya heshim. Kisha itasema: “Ee Rabb, Ridhika naye”. Allaah, Ataridhika naye. Kisha ataambiwa: “Soma na panda”. Atapokea thawabu zaidi ya mema kwa kila Aayah [atakayosoma])) [At-Tirmidhy na Al-Haakim]

 

 

 

X3-Mwenye Ujuzi Zaidi Wa Qur-aan Huwa Na Mwanga Kaburini:

 

 

عن جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَجْمَعُ بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ مِنْ قَتْلَى أُحُدٍ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ ثُمَّ يَقُولُ:  ((أَيُّهُمَا أَكْثَرُ أَخْذًا لِلْقُرْآنِ)) فَإِذَا أُشِيرَ إِلَى أَحَدِهِمَا قَدَّمَهُ فِي اللَّحْدِ  

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kwamba alikuwa Rasuli wa Allaah akiwakusanya watu wawili waliokufa katika vita vya       Uhud katika nguo moja kisha anauliza, ((Nani katika hao mwenye ujuzi zaidi wa Qur-aan?)) Anapojulishwa mmoja kati ya hao, humtanguliza mwanandani)) [Al-Bukhaariy, An Nasaaiy]

 

 

03-Umri Muwafaka Wa Kuhifadhi Qur-aan

 

Umri muwafaka na bora zaidi utakaofanya sahali kuihifadhi Qur-aan ni kuanzia  utotoni kabla ya kufikia umri wa kubaleghe, kwani wakati huo vijana hushughulishwa na dunia, hasa zama hizi zilizojaa fitnah huwa si wepesi kuepukana nazo ila tu kwa Rahma ya Allaah (سبحانه وتعالى). Lakini mtoto anapokuwa angali katika umri mdogo, basi kuhifadhi kwake chochote kichwani huwa ni sahali kwa sababu bongo huwa na kumbukumbu nzuri bado na si wepesi kusahau anachokihifadhi. Imesemekana kwamba: 

 

"الْحِفْظُ فِي الصِّغَرِ كالنَّقْشِ عَلى الْحَجَرِ، والْحِفْظُ فِي الْكِبَرِ كالنَّقْشِ علَى الْمَاءِ"

"Kuhifadhi udogoni ni kama nakshi katika jiwe, na kuhifadhi ukubwani ni kama nakshi katika maji

 

 

(Kauli nyingine imetaja ‘Elimu udogoni ….)

 

Ina maana: Kuchonga au kuchora nakshi katika udongo uliomaji, mchoro huo hubakia milele kuwa ni alama katika jiwe litakapokauka. Ama mwenye kuchora katika maji, mchoro huo hutoweka.

 

 

Hata hivyo, haimaanishi kwamba aliyefikia umri mkubwa haitowezekana kwake kuihifadhi Qur-aan, bali mtu anapopendelea kutekeleza ‘amali hii tukufu, ajitahidi na Allaah (سبحانه وتعالى) Atamfanyia sahali kwa sababu ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwratul-Qamar haikutofautisha kati ya mtoto au mtu mzima. Wako walioihifadhi Qur-aan wakiwa na umri zaidi ya miaka arubaini. Bali imesemekana kwamba mtu aliyefikia miaka zaidi ya sabiini aliweza kuihifadhi Qur-aan. Muislamu anapaswa awe na iymaan na yakini kuhusu maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) na awe na dhana njema na matumaini na matarajio mazuri daima. Kufanya hivyo, itampa nguvu na azimio la kuihifadhi Qur-aan.

 

Hivyo ni fursa tukufu kwa Muislamu kuhifadhi Qur-aan. Lakini ikiwa fursa hii imekupita na sasa inaelekea kwamba huna uwezo wa kuhifadhi Qur-aan, basi fanya hima na juhudi kuwahifadhisha watoto wako wakiume na wakike.  Usiache fursa hii ikawapita wao pia kwani furaha yao ya kuhifadhi Qur-aan itakuwa ni furaha na fakhari kwako na kupata Radhi za Allaah (سبحانه وتعالى) na utakuwa umeshajitangulizia akiba huko Aakhera.

  

 

 

 

04-Nasaha Za Kuhifadhi Qur-aan

 

 

Kabla ya kuanza kuhifadhi Qur-aan jitayarishe kutekeleza nasaha zifautazo:

 

 

 

i-Kutia Niya Safi (Ikhlaasw)

 

 

Anza na kutia niya ya dhati kwamba unakusudia kuhifadhi Qur-aan kwa ajili ya kupata Radhi za Allaah (سبحانه وتعالى) na kutegemea fadhila na malipo yake, na hivi ndivyo inavyopasa katika ‘ibaada na amali zote.

 

 

 

ii-Weka Azimio La Nguvu Bila Ya Kukata Tamaa.

 

 

Weka azimio la nguvu, usichoke, usikate tamaa wala usivunjike moyo hasa pale utakapoona kwamba unazorota katika baadhi ya Aayah au Suwrah utakazoziona ngumu. Chukua mfano wa anayetaka kupanda mlima, akaupanda polepole hadi kufikia kileleni. Hivyo basi japokuwa utakuwa unahifadhi kidogo kidogo, endelea usiache na kumbuka kauli ya Nabiy :

 

((... لاَ يَمَلُّ اللَّهُ حَتَّى تَمَلُّوا وَكَانَ أَحَبَّ الدِّينِ إِلَيْهِ مَادَامَ عَلَيْهِ صَاحِبُهُ)) متفق عليه

(…Allaah Hachoki [kulipa thawabu] mpaka mchoke wenyewe. Na ‘Ibaadah Aipendayo zaidi ni ile inayodumishwa na mtendaji)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

iii-Kuomba Du'aa

 

 

Muombe Allaah (سبحانه وتعالى) Akupe tawfiyq ya kuhifadhi maneno Yake. Usiache kuomba kila mara. Tumia Wasiylah[5] na nyakati za kukubaliwa du'aa.

 

 

 

iv-Tambua Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan:

 

 

Soma fadhila hizo upate hima ya kuzichuma na ikupe azimio la nguvu.

 

 

 

v-Kubakia Katika Taqwa: 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ

Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni. [Al-Baqarah (2: 282)]

 

 

Kwa hiyo jisafishe kwanza na madhambi kwa kuomba maghfirah na kutubia kwa Allaah (سبحانه وتعالى), kisha jiepushe na maasi yote kwani maasi yanamzuia mja kushika maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى). Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنه)  amesema:

 

إِن َّالرَّجُلَ لَيُحْرَمَ العِلْمَ بِذَنْبٍ يُصِيبُه

"Hakika mtu hunyimwa elimu kwa dhambi anazozitenda"

 

Imaam Ash-Shaafi'iy   (رحمه الله)alikuwa mwepesi wa kuhifadhi Qur-aan lakini Qur-aan ilipokuwa nzito kuihifadhi alisema:

 

شَكَوْتُ إلَى وَكِيعٍ سُوءَ حِفْظِي،  فَأرْشَدَنِي إلَى تَرْكِ المعَاصِي . وَأخْبَرَنِي بأَنَّ العِلْمَ نُورٌ،

 ونورُ اللهِ لاَ يُهْدَى لِعَاصِي

"Nililalamika kwa Wakiy’i kuhusu kushindwa kuhifadhi Qur-aan akaninasihi kuacha maasi na akanijulisha kuwa nuru ya elimu na nuru ya Allaah haimfikii mwenye kuasi"

 

 

 

vi-Kutoshughulika Na Anasa Za Dunia

 

 

Inampasa mwenye kutaka kuhifadhi Qur-aan atumie muda wake wote kwa ajili ya kuhifahdi Qur-aan. Ajitenge na anasa za dunia asizichanganye na kazi hii, ili akili na moyo wake upate utulivu kwa ajili ya hifdhwul-Qur-aan. Watu hupoteza wakati wao mwingi kushughulika na mambo ya upuuzi yasiyomzidishia Iymaan wala kumfaa Aakhirah yake. Fitnah zimekuwa nyingi na nyenzo zake zimekithiri; mitandao, televisheni, simu za mkono na huduma zake n.k. Wengineo hukaa mabarazani kwa maongezi au michezo ya karata n.k. Anayechanganya anasa, upuuzi n.k. na huku akitaka kuhifadhi Qur-aan hatoweza kabisa kwani Anasema Allaah (سبحانه وتعالى): 

 

مَّا جَعَلَ اللَّـهُ لِرَجُلٍ مِّن قَلْبَيْنِ فِي جَوْفِهِ ۚ

Allaah Hakufanya mtu yeyote kuwa na nyoyo mbili kifuani mwake. [Al-Ahzaab: (33: 4)]

 

 

vii-Kuipa Hifdhwul-Qur-aan Kiupambele.

 

 

Katika ratiba za siku maishani mwako, lazima uipe hifdhwul-Qur-aan (kuhifadhi Qur-aan) kiupambele. Jiwekee wakati maalumu kila siku uwe kwa ajili ya kuhifadhi Qur-aan tu. Wakati bora kabisa uliotambulika kuwa ni muwafaka kuihifadhi Qur-aan ni nyakati za usiku ambako kuna ukimya na utulivu. Bali wakati mzuri kabisa ni kabla ya Alfajiri au baada ya kuswali tu Alfajiri kwa sababu hapo bongo bado liko tupu na safi na liko tayari kupokea na kuhifadhi kinachosomwa. Hilo limetambulikana kutokana na uzeofu wa waliohifadhi Qur-aan na jambo hilo halina shaka kwani kulingana na mchana, ni tofauti kabisa kwa sababu mchana kuna harakati nyingi ambazo zinaweza kukukatiza hifdhw yako; mfano watu ingia toka, simu n.k.

 

 

 

viii-Jifunze Kwanza Kuisoma Qur-aan Bila Ya Makosa 

 

 

Inapasa mwenye kutaka kuhifadhi Qur-aan kwanza ajifunze kuisoma Qur-aan sawasawa bila ya makosa kwani unapohifadhi kosa huwa vigumu baadaye kulirekebisha. Juu ya hivyo kuisoma Qur-aan kimakosa hubadilisha na kupotosha kauli za Allaah (سبحانه وتعالى).[6]

 

 

ix-Jifunze Kuisoma Qur-aan Kwa Hukmu Za Tajwiyd

 

 

Kusoma kwa kufuata hukmu za Tajwiyd husaidia kutambua maneno yanayofuatia, mfano baada ya maddum-munfaswil (madd ya kuachana) utajua tu kwamba neno la pili litakuwa linaanzia na herufi ya hamza. Vile vile unapojifunza Tajwiyd ndipo utakapoweza kuisoma Qur-aan kwa kuitamka vizuri ipasavyo na kuvuta panapotakiwa na kufanya ghunnah[7] panapotakiwa n.k na ndipo qiraa-a cha mtu kinapokuwa kizuri.

 

 

 

x-Jifunze Lugha Ya Kiarabu

 

Muislamu anapaswa kujifunza lugha ya Kiarabu aweze kufahamu maneno ya Rabb wake. Lugha ya Kiarabu itamsadia pia mwenye kuhifadhi Qur-aan kutambua vipi kutamka neno linaloanzia au linalofuatia kwa vile maneno hubadilika kutokana na hukmu za serufi ya lugha ya Kiarabu.[8] Waislamu wengi hawatilii hima kujifunza lugha hii tukufu. Baadhi ya watu wako tayari kulipia gharama kubwa ya kujifunza lugha nyinginezo na hali lugha ya Kiarabu ndio iliyowajibika kwanza ili kuweza kufahamu maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) na ya Rasuli Wake .

 

 

xi-Tumia Aina Moja Ya Mswahafu

 

 

Tumia Mswahafu wa aina moja, usichanganye Miswahafu katika kuhifadh kwa sababu mpangilio wa Suwrah zinavyoanza na kumalizikia zinatofautiana katika baadhi ya miswahafu, na hivyo hata Ayaah huwa zimetofautiana katika kupangika kwake kwenye ukurasa. Utakuta katika aina ya Mswahafu mmoja Aayah fulani imeanzia juu ya ukurasa, lakini Aayah hiyo hiyo katika aina nyingine ya Mswahafu imepangika katikati au chini ya ukurasa. Kutumia aina mbili za mswahafu kutambabaisha mwenye kuhifadhi kwa sababu mtu anapohifadhi Aayah huwa ni kama taswira (picha) iliyotua akilini na kubakia katika kumbukumbu. Ndio maana utamuona aliyehifadhi Qur-aan huwa ni sahali kwake kutambua Aayah iko sehemu gani ya ukurasa. 

 

 

 

xii-Sikiliza Ulichohifadhi Kila Mara

 

 

Mchague Qaariu (msomaji) unayependa kumsikiza urudie kuzisikiliza Aayah ulokwishazihifadhi hadi zithibitike moyoni. Ni neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba imekuwa sahali mno zama hizi za maendeleo ya teknologia, kupata visaidizi mbali mbali vya kumsaidia mwanafuzi katika mafunzo ya Dini yake tena bila ya gharama kubwa.

 

 

xiii-Vyakula Na Miti Shamba Ya Kusaidia Kumbukumbu

 

 

Imetambulikana kuwa baadhi ya vyakula au miti shamba husaidia ubongo kuamsha kumbukumbu na kutibu usahaulifu. Tumia vyakula na miti shamba ifuatayo ambayo imethibiti katika Qur-aan na Tiba Ya Nabiy upate natija nzuri In Shaa Allaah:

 

Asali, habbat-sawdaa (haba soda), lozi, tende, majani ya jarjiyr, zabibu, mafuta ya zaytuni au zaytuni zenyewe, tiyn, lubaan-adhikr (ubani wa kumbukumbu au ubani wa maji), nanaa (weka katika chai ukipenda), zaatari, tangawizi, 'arqisus (vijiti fulani vya mitishamba vinaponyesha kifua pia). Michanganyiko ifuatayo Imetambulikana kuleta manufaa:

 

 

  • Saga njugu za pistachio, zabibu nyeusi, lozi, lubaan-adhikr kisha tia katika asali kiasi cha kuchanganyika vitu vyote hivyo vizuri na kula asubuhi na jioni kijiko kimoja cha chai.

 

  • Loanisha nyuzi chache za zaafarani katika maziwa ya dafudafu, subiri ilowanike kisha kunywa.

 

 

 

05-Utaratibu Wa Kuhifadhia Qur-aan

 

 

Kuhifadhi Qur-aan inategemea uwezo wa mtu; kuna wanaoweza kuhifadhi ukurasa mmoja kwa dakika chache tu. Wengineo huwachukua masaa. Kulingana na uwezo wako, fuatilia utataribu ufuatao unaotumika zaidi kwa kuwa umeonekana ni muwafaka na unaoleta najita nzuri.

 

 

i-Soma Aayah unazotaka kuhifadhi uhakikishe unazisoma sawa sawa bila ya makosa yoyote.

 

 

 

ii-Anza kuhifadhi Aayah moja, ikithibitika moyoni, isome mara kumi.

 

iii-Ongeza Aayah ya pili ikithibitika soma mara kumi, kisha rudia Aayah ya mwanzo na hii ya pili usome mara kumi zote mbili.

 

 

 

iv-Ongeza Aayah ya tatu uhifadhi, ikithibitika, isome mara kumi, kisha rudi kuanzia Aayah ya mwanzo, ya pili na hii ya tatu usome mara kumi zote. Endelea hivyo hivyo kwa kadiri ya uwezo wako wa kuhifadhi kwa siku kama ni Aayah tatu utakomea hapo, kama una uwezo wa kuhifadhi zaidi utaendelea kwa utaratibu huo huo. 

 

 

 

v-Usiendelee mbele hadi uwe umezithibitisha Aayah ulizozihifadhi vizuri. Ukifanya kosa urudie kuihifadhi Aayah yenye kosa hadi kusikuweko na makosa kabisa. Hatimaye Utakapoweza kuhifadhi ukurasa mzima, usikilizwe na Mwalimu na pindi ukikosea makosa zaidi ya matatu basi urudie kuzihifadhi tena ukurasa huo mpaka uthibitike. Utaratibu huu wa kurudia tokea Aayah za mwanzo na kuzirudia kusoma mara kumi au zaidi husaidia kukumbuka mfuatano wa Aayah bila ya kuipita moja katikati.

 

 

 

vi-Ikiwa unajihifadhisha mwenyewe, ni muhimu upate mtu akusikilize kila unapothibitisha moyoni Aayah kadhaa. Akusikilize pia unapofanya marejeo ya hifdhw ya Suwrah ulizozihifadhi.

 

 

 

vii-Soma kwa sauti ya kusikilizika na sio kimya kimya. Ukiwa ni peke yako, jifungie chumbani uwe huru kuisoma kwa sauti ya juu.

 

 

 

viii-Siku ya pili, endelea kuchukua Aayah mpya kadiri uwezavyo. Zihifadhi kwa utaratibu huo huo.

 

 

 

ix-Utakapomaliza, fanya marejeo ya kuzisoma Aayah ulizohifadhi mwanzo yaani jana yake, kisha unganisha na hizi mpya hadi zote zithibitike moyoni.

 

 

 

x-Siku ya tatu endelea hivyo hivyo, kila unapozidi kuhifadhi ndipo unapozidi kupanua ubongo wako kuweza kuhazini Aayah nyingi akilini, lakini pia ndipo kila unapohitaji muda wa kurudia Aayah za mwanzo ulizozihifadhi.

 

 

 

x-Kuziandika Aayah katika kitabu au ubao ni njia mojawapo iliyojaribiwa na kuonenakana imeleta natija ya kusaidia hifdhw ya Qur-aan.

 

06-Zingatia Aayah Zinazoshabihiana (Aayaat Al-Mutashaabihaat)

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara. [Az-Zumar (39: 23)]

 

Anayehifadhi Qur-aan aghlabu hutatizwa na kubabaika katika Aayah zinazoshabihiana katika Qur-aan. Kushabihiana kwake kunatofautiana  ima kwa kutangulia neno au maneno, au kunatofautiana katika herufi au irabu n.k. Utakapozitambua na kuzihifadhi sawa sawa kauli hizo, basi utajiepusha na kutatizwa huko In Shaa Allaah. Kuna vitabu kwa lugha ya Kiarabu ambavyo vimetaja Aayah hizo laiti kama vingefasiriwa vitabu hivyo kwa lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa Vitabu hivyo ni vifuatavyo:

 

  •    مصحف التبيان المفصل لمتشابهات القرآن
  •    الإيقاظ لتذكير الحفاظ بالآيات المتشابهة الألفاظ
  •    عون الرحمن في حفظ القرآن
  •    المعجم المفهرس للتراكيب المتشابهة لفظا
  •    دليل الحفاظ في متشابهه الألفاظ
  •    دليل الآيات متشابهة الألفاظ في كتاب الله العزيز
  •  معجم الأعلام والموضوعات في القرآن الكريم
  •   مفصل آيات القرآن ترتيب معجمي
  •   معجم ألفاظ القرآن لمجمع اللغة العربية بالقاهرة
  •   المعجم المفهرس للتراكيب المتشابهة لفظا أ. د. محمد زكي خضر
  •   هداية المرتاب وغاية الحفاظ والطلاب في تبيين متشابه الكتاب
  •    إعانة الحفاظ للآيات المتشابهة الألفاظ
  •    البرهان في توجيه متشابه القرآن
  •  اسرار التكرار فى القرآن المسمى البرهان فى توجيه متشابه القرآن للكرمانى
  •   السخاوية في متشابهات الآيات القرآنية
  •   متن هداية المرتاب / أداء المقرئ سعد الغامدي
  •  الضبط بالتقعيد للمتشابه اللفظي في القرآن المجيد للشيخ / فواز بن سعد الحنين
  •   المعجم الموسوعي لألفاظ القرآن الكريم وقراءاته
  •    سبيلُ الإتقان في مُتشابه القرآن
  •    كنز الحفاظ في متشابه الألفاظ
  •    البرهان في توجيه متشابه القرآن لما فيه من الحجة والبيان
  •     إرشاد الحفاظ الكرام إلى ضبط وتوجيه متشابهات سورة يونس
  •     الدليل إلى تعليم كتاب الله الجليل
  •    الضبط بالتقعيد للمتشابه اللفظي في القرآن المجيد للشاملة
  •    الإيقاظ لتذكير الحفاظ بالآيات المتشابهة في الألفاظ
  •   كشف المعاني في المتشابه المثاني لابن جماعة تحقيق مرزوق علي إبراهيم
  •   ملاك التأويل للغرناطي
  •    الدليل إلى تعليم كتاب الله الجليل - نسخة مصورة

 

Mifano michache ya kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zinazoshabihiana ni kama ifautavyo:

 

 

i-Mfano wa kwanza:

 

وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ

 

 [Al-Baqarah (2: 173)]

 

Aayah hii katika Suwratul Baqarah ni pekee iliyotanguliza neno la بِهِ   kabla ya  لغير الله.

 

Ama kwengineko kama katika Suwratul-Maaidah (5:3) Suwratul-An-aam (6: 145) Suwratun-Nahl (16:115) imekuwa tofauti na hiyo Aayah ya Suwratul-Baqarah kwa kuwa neno la بِهِ limekuja baada ya لغير الله

 

وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ

Pia katika Suwratun-Nahl haikuanzia na: !$tBur

 

 

ii-Mfano wa pili:      

 

Zingatia kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zifuatazo jinsi zilivyoshabihiana na tofauti zake:

 

 

y7ÏsŒ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾

 

[Al-Baqrah (2: 61)]

 

 

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿١١٢﴾ 

 

[Aal-‘Imraan (3: 112)]

 

 

Kauli zifuatazo zimeshabihiana lakini zimetofautiana katika irabu; ya kwanza imetajwa kwa fat-haa na pili kwa kasra.

 

 

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾

 

[Aal-‘Imraan (3: 181)]

 

 

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِآيَاتِ اللَّـهِ وَقَتْلِهِمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ  

 

[An-Nisaa (4: 155)]

 

 

 

iii-Mfano wa tatu:

 

 

Aayah zilizoshabihiana lakini zimetafautiana kidogo katika kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu Nabiy Zakariyyah (عليه السلام) na Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) katika Suwratul-’Imraan:

 

 

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾

 

[Aal-‘Imraan (3: 40)]

 

 

قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ

 

[Aal-‘Imraan: (3: 47)]

 

 

 

iv-Mfano wa nne:

 

  وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ

 

[Al-Israa (17: 89)]

 

 

Hapa tunaona kwamba neno لِلناَّسِ  limetangulia. Ama katika Aayah ifuatayo limekuja baadaye.

 

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ

[Al-Kahf (18: 54)]

 

 

 

v-Mifano mingi mno imo katika Qur-aan iliyokuwa katika hali kama hizo, na vinginevyo. Na pia nyingi hutofautiana pale inapomalizika Aayah; mfano Aayah mbili zinazofuatiana katika Suwratul-Maaidah:

 

 

لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٢﴾

 

[Al-Maaidah (5: 62)]

 

  لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿٦٣﴾

 

[Al-Maaidah (5: 63)]

 

 

Kisha katika Aayah Namba 79 imetofautiana tena:

 

 

لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾

[Al-Maaidah (5: 79)]

 

 

Zingatia pia Asmaa na Swifaat za Allaah (سبحانه وتعالى) zinavyomalizika ambazo mara nyingi zimetajwa mbili mbili, huwa zinatofautiana mara kwa mara. Asmaa na Swifaat za Allaah (سبحانه وتعالى) zimekariri zaidi katika Suwratun-Nisaa. Pia aina za adhabu zinavvyotajwa mwishoni mwa Aayah. Almuradi darsa hili ni pana mno inahitaji mijalada ya vitabu!  Inatosheleza kwamba anayehifadhi Qur-aan atambue swala hii na awe makini mwenyewe katika kutambua kauli na maneno hayo.   

 

 

 

07-Kuithibitisha Qur-aan Baada Ya Kuihifadhi

 

Kuhifadhi Qur-aan si jambo gumu sana  kama kuithibitisha kwake, kwa sababu mtu anaweza kuhifadhi ukurasa mmoja chini ya nusu saa, lakini ikiwa hakuifanyia juhudi kukariri kuisoma hadi ithibitike vyema moyoni, basi hapo hatobakia katika kumbukumbu, na hivyo basi itakuwa ni khasara kubwa kwa kuwa mtu amepoteza juhudi kubwa na muda wingi kwa jambo ambalo mwishowe halikuthibiti lengo lake.

 

 

Nasaha zifuatazo zitakusaidia kuithibitisha hifdhw yako In Shaa Allaah:

 

 

i-Dumisha kusoma Qur-aan

 

 

Inakupasa ndugu uliyeihifadhi Qur-aan uendelee kuisoma Qur-aan kila siku, kila mara bila ya kuiacha. Kila siku uweke muda maalumu uwe khasa kwa ajili ya kuisoma Qur-aan na isiwe chini ya nusu juzuu kila siku! Na ukiweza kuisoma zaidi ndivyo utakavyoweza kuithibitisha zaidi. Ipe ratiba hii kiupambele katika kila siku ya maisha yako. Zingatia kauli zifautazo za Nabiy :  

 

Hadiyth ifuatayo Nabiy ameapa kupotea kwa Qur-aan pindi mtu asiposhikamana nayo: 

 

عَنْ أَبِي مُوسَى عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((تَعَاهَدُوا هَذَا الْقُرْآنَ فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَهُوَ أَشَدُّ تَفَلُّتًا مِنْ الْإِبِلِ فِي عُقُلِهَا))   

Imepokelewa toka kwa Abu Muwsaa (رضي الله عنه) : Amesema Nabiy : ((Dumisheni kuisoma Qur-aan. Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hiyo (Qur-aan) ni wepesi kukimbia kuliko ngamia anavyochopoka katika kamba yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

Na pia,

 

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((إِنَّمَا مَثَلُ صَاحِبِ الْقُرْآنِ كَمَثَلِ صَاحِبِ الْإِبِلِ الْمُعَقَّلَةِ إِنْ عَاهَدَ عَلَيْهَا أَمْسَكَهَا وَإِنْ أَطْلَقَهَا ذَهَبَتْ)) 

Imepokelewa toka kwa ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)  kwamba Rasuli wa Allaah amesema: ((Hakika mfano wa aliyehifadhi Qur-aan ni kama ngamia aliyefungwa, akimfunga atamzuia, na akimuacha ataenda zake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

ii-Kabla Ya Kulala Rudia Aayah Ulizozihifadhi

 

 

Imejaribiwa na kuonekana kwamba pindi mtu akirudia  alichohifadhi katika Qur-aan kabla ya kulala, inasaidia kuthibitisha hifdhw yake.   Bali ni amali bora kabisa kwamba unasoma Qur-aan kabla ya kulala kwani huenda ikawa ndio amali yako ya mwisho pindi umeandikiwa kufariki usingizini ukajaaliwa husnul-khaatimah (mwisho mwema) na hivyo ndivyo itakavyokuwa hali ya kufufuliwa kwako.

 

 

iii-Zisome Aayah Ulizozihifadhi katika Swalaah Za Sunnah.

 

 

Hii ni njia bora kabisa ya kuthibitisha hifdhw yako. Zitumie kwanza Aayah zilizothibitika vizuri moyoni kwenye Swalaah za Sunnah, kisha pole pole ongezea nyinginezo. Inaruhusiwa kutumia Mswahafu katika Swalaah za Sunnah, kwa hiyo weka Mswahafu katika rafu ndefu inayofikia urefu wa kiasi cha kuweza kuangaza Aayah, usome kwa hifdh lakini pale unapotatizwa na Aayah, upige jicho kuhakikisha au kurekebisha ulichokosea.

 

 

iv-Sikiliza Suwrah ulizozihifadhi.

 

 

Pia hii ni njia nyingineyo muwafaka kabisa ya kuithibitisha hifdhw ya Qur-aan. Isikilize kila wakati kila mahali, kila unapopata fursa. Sikiliza hata unapokuwa unafanya kazi zako nyinginezo ingawa inalotakiwa ni kuisikiliza kwa umakini. Imesemekana kwamba baadhi ya watu wameweza kuihifadhi Qur-aan kwa kuisikiliza tu.

 

Kuisikiliza Qur-aan itakusaidia pia kujirekebisha makosa yako na pia utakapomchagua Qaariu mwenye sauti nzuri inayekupendezea, utaweza nawe kuisoma kwa sauti hiyo hiyo.

 

 

 

v-Ifundishe Qur-aan

 

 

Kazi hii humsaidia sana mtu kuithibitsha hifdhw yake. Je, kuna kazi bora zaidi ya kujifunza na kufundisha Qur-aan?  Amesema Rasuli wa Allaah katika Hadiyth ya 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه)

 

((خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه))

((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 08-Hitimisho:

 

 

Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atufanyie sahali katika amali hii tukufu na Atupe tawfiyq ya kuisoma kwa njia inayomridhisha Yeye Pekee, na Atuwezeshe kuihifadhi katika vifua vyetu na kuifanyia kazi maamrisho na makatazo yake na Atutakabalie du’aa zetu zote na khasa zifuatazo:

 

اللَّهُمَّ اجْعَلِ القُرْآنَ الْعَظِيمَ رَبِيـعَ قُلُوبِنا، وَنورَ صُدُورِنا وجَلَاءَ أَحْزَانِنا وذَهَابَ هُمُومِنا وَغُمُومِنا. اللَّهُمَّ ارْحَمْنَا بِالْقُرآنِ الْكَرِيمِ وَاجْعَلْهُ لَنا إِمَامًا وَنُورًا وَهُدًى وَرَحْمَةً. اللَّهُمَّ ذَكِّرْنَا مِنْهُ مَا نَسِينا وَعَلِّمْنا  مِنْهُ مَا جَهِلْنا وَارْزُقْنَا تِلاَوَتَهُ آنَاءَ اللَّيْلِ وَآنَاءَ النَّهَارِ وَاجْعَلْهُ لَنا حُجَّةً يَارَبَّ الْعَالَمِينَ.

اللَّهُمَّ اجْعَلنَا مِنْ أَهِلِ الْقُرْآنِ الَّذِينَ هُمْ أَهْلُكَ وَخآصَّتُك. اللَّهُمَّ اجْعَلِ الْقُرْآنَ الْكَرِيمَ لَنَا فِي الدُّنْيا قَرِينًا،  وَفِي الْقَبْرِ مُؤْنِساً وَعَلَى الصِّرَاطِ نُوراً،

 وَفِي الْقِيَامَةِ شَفِيعاً، وَإلَى الْجَنَّةِ رَفِيقاً، وَمِنَ النَّارِ سِتْراً وَحِجَاباً،  وَإِلَى الْخَيْرَاتِ كُلِّهَا دَلِيلاً وَإِمَاماً بِفَضْلِكَ وَجُودِكَ يَا أَكْرَمَ الأَكْرَمْينَ. وَصَلَّ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّنا مُحَمَّدٍ وَعَلى آلِهِ وَاَصْحَابِهِ وَسَلَّمَ تَسْلِيماً  كَثِيراً .

 

Ee Allaah Ijaaliye Qur-aan tukufu kuwa ni raha na uchanuzi wa nyoyo zetu, na Nuru ya vifua vyetu, na utatuzi wa huzuni zetu, na sababu ya kuondoka wahka na dhiki zetu. Ee Allaah, Turehemu kwa Qur-aan na ijaalie iwe ni kiongozi, nuru, Hidaaya na Rahma. Ee Allaah tukumbushe tunayoyasahu humo, na tufunze tuliyokuwa hatuayajui, na turuzuku kuisoma usiku na mchana na ijaalie iwe hoja yetu (isiwe hoja dhidi yetu) ee Rabb wa walimwengu.

 

Ee Allaah tujaalie tuwe watu wa Qur-aan ambao ni watu wako Uwapendao. Ee Allaah ijaalie Qu-raan kuwa rafiki mwandani duniani, na kaburini iwe ni yenye kutuliwaza, iwe Nuru katika Asw-Swiraatw, na iwe Shafaa’ah (kiombezi) Siku ya Qiyaamah, na tuambatane nayo Peponi, na iwe sitara na kizuizi cha Moto. Na iwe dalili katika kila kheri na kiongozi kwa Ukarimu Wako ee Mbora wa wanaokirimu.

 

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾ وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ ﴿١٨١﴾ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٨٢﴾

 

وَصَلَّ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّنا مُحَمَّدٍ وَعَلى آلِهِ وَاَصْحَابِهِ وَسَلَّمَ تَسْلِيماً  كَثِيراً

 

 

[1] Sehemu ya mifugo ya farasi

 

[2] Sehemu katika Msikiti wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) waliyokuwa wakikaa Swahaba ambao hali zao walikuwa ni masikini.  

 

[3] Bonde lilioko Kusini mwa mji wa Madiynah kuelekea upande wa Magharibi karibu na Jabali la Sal’. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitawadha katika bonde hili siku ya vita vya Khandaq

 

[4] Bonde maarufu kabisa katika mji wa Madiynah au eneo la Al-Hijaaz yote. Liko umbali wa maili kilometa mia Kusini na linaelekea upande wa Mashariki. Linajulikana kuwa ni ‘Bonde lenye Baraka’.

 

[5] Kujikurubisha kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa ‘ibaadah

 

[6] Rejea kitabu cha: Alhidaayah Katika Ahkaam Za Tajwiyd- Mlango wa ‘Makosa Ya Dhahiri Na Yaliyofichika’

 

[7] Sauti inayaotokea puani

 

 

Share