60-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kitabu Chake (Qur-aan) Kimepewa Majina Na Sifa Kadhaa
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
60-Kitabu Chake (Qur-aan) Kimepewa Majina Na Sifa Kadhaa
Al-Qur-aan aliyoteremshiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ina Majina na Sifa kadhaa. Miongoni mwayo ni Uhai, Burhani (dalili za wazi) na Nuru. Majina na Sifa hizo Amezitaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika Qur-aan kwenye Aayah mbali mbali; mfano wa Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) ni:
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
Enyi Ahlal-Kitaab! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anasamehe mengi. Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainisha. [Al-Maaidah: 15]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾
Enyi watu! Kwa yakini imekujieni burhani kutoka kwa Rabb wenu na Tumekuteremshieni Nuru bayana. [An-Nisaa: 174]
Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٨﴾
Basi muaminini Allaah na Rasuli Wake na Nuru (Qur-aan) Tuliyoiteremsha, na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [At-Taghaabun: 8]
Na kuhusu Uhai Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ﴿٥٣﴾
Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutoka amri Yetu. Hukuwa uajua nini Kitabu wala iymaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. Njia ya Allaah Ambaye ni Vyake Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! Kwa Allaah Pekee yanaishia mambo yote. [Ash-Shuwraa: 52-53]
Baadhi Ya Majina Na Sifa Za Qur-aan:
|