07-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake: Alikataza Na Kutahadharisha Kudanganywa Watoto
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:
07-Alikataza Na Kutahadharisha Kudanganywa Watoto
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na huruma yake, na uadilifu wake kwa watoto, alionya na kutahadharisha kutokuwadanganya Watoto kwa lolote:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَامِرٍ أَنَّهُ قَالَ دَعَتْنِي أُمِّي يَوْمًا وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَاعِدٌ فِي بَيْتِنَا فَقَالَتْ هَا تَعَالَ أُعْطِيكَ . فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " وَمَا أَرَدْتِ أَنْ تُعْطِيهِ " . قَالَتْ أُعْطِيهِ تَمْرًا . فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَمَا إِنَّكِ لَوْ لَمْ تُعْطِيهِ شَيْئًا كُتِبَتْ عَلَيْكِ كِذْبَةٌ "
Amesimulia ‘Abdullaah ibn ‘Aamir kwamba: Mama yangu aliniita siku moja pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ameketi nyumbani kwetu. Aksema: Njoo hapa nitakupa kitu! Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Je, ulidhamiria kumpa nini?” Akajibu: Nilidhamiria kumpa tende. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwmabia. “Ingelikuwa hukumpa chochote, basi ungelirekodiwa uongo dhidi yako.” [Sunan Abiy Daawuwd na amepa daraja ya Hasan Imaam Al-Albaaniy]