11-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kumkirimu Mgeni
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب إكرام الضيف
11-Mlango Wa Kumkirimu Mgeni
قَالَ الله تَعَالَى:
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ﴿٢٤﴾ إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٢٥﴾ فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ﴿٢٦﴾ فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ﴿٢٧﴾
Je, imekufikia hadithi ya wageni wahishimiwao wa Ibraahiym? Walipoingia kwake wakasema: Salaam! Akasema: Salaam watu wasiotambulikana. Akaondoka bila kuhisiwa kuelekea kwa ahli yake akaleta ndama aliyenona. Akawakurubishia; akasema: Mbona hamli? [Adh-Dhaariyaat: 24 - 27]
وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ﴿٧٨﴾
Wakamjia kaumu yake wakimkimbilia na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Luutw) Akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa ni mabinti zangu, wao wametwaharika kwenu (kuwaoa kihalali) Basi mcheni Allaah, na wala msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Je, hakuna miongoni mwenu mtu muongofu? [Huwd: 78]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake; na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho na aunganishe kizazi; na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho na aseme kheri au anyamaze." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hadiyth – 2
وعن أَبي شُرَيْح خُوَيْلِدِ بن عَمرو الخُزَاعِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول: (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ جَائِزَتَهُ ))
قالوا : وَمَا جَائِزَتُهُ ؟ يَا رسول الله ، قَالَ : (( يَوْمُهُ وَلَيْلَتُهُ ، وَالضِّيَافَةُ ثَلاَثَةُ أيَّامٍ ، فَمَا كَانَ وَرَاءَ ذَلِكَ فَهُوَ صَدَقَةٌ عَلَيْهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية لِمسلمٍ : (( لاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أنْ يُقِيمَ عِنْدَ أخِيهِ حَتَّى يُؤْثِمَهُ )) قالوا : يَا رسول الله ، وَكيْفَ يُؤْثِمُهُ ؟ قَالَ : (( يُقِيمُ عِنْدَهُ وَلاَ شَيْءَ لَهُ يُقْرِيه بِهِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Shurayh Khuwaylid bin 'Amru Al-Khuzaa'iy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho na amkirimu mgeni wake Jaa'izatahu." Wakauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Jaa'izatahu ni nini?" Akasema: "Ni siku moja (mchana na usiku wake) na ugeni ni siku tatu. Zaidi ya siku hizo (tatu) ni swadaqah kwake." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Katika riwaayah ya Muslim: "Haifai kwa Muislamu kukaa siku nyingi kwa nduguye (mwenyeji wake) mpaka akamtia katika dhambi." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Na vipi atamtia katika dhambi?" Akasema: "Anakaa kwake na ilihali mwenyeji hana cha kumkirimu mgeni wake."