04-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Anayeongoza Katika Kheri Atapata Ujira Wa Mwenye Kutekeleza Kheri Hiyo
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 04
Anayeongoza Katika Kheri Atapata Ujira Wa Mwenye Kutekeleza Kheri Hiyo
وَعَنْ أَبِي مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ، فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujulisha kheri atapata mfano wa ujira (malipo) wa mwenye kuifanya.” [Muslim]
Na pia,
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ لاَ يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا)) مسلم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Yeyote anayelingania katika uongofu, atakuwa na ujira mfano ujira wa anayemfuata, hatapunguziwa kutokana ujira huo chochote)) [Muslim]