12-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Aliyekuwa Umahiri Wa Qur-aan Yupamoja Na Malaika Anayejifunza Ana Thawabu Mara Mbili
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 12
Aliyekuwa Umahiri Wa Qur-aan Yupamoja Na Malaika,
Ama Anayejifunza Ana Thawabu Mara Mbili
عَنْ عَائِشَةَ قَالَتْ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ))
'Aaishah (رضي الله عنها) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Yule aliyekuwa mahiri (mwenye ujuzi) wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)) [Al-Bukhaariy na Muslim]