19-Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Malaika Huwateremshia Mbao Zao Mtafutaji ‘Ilmu Na Wanaridhia Naye
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 19
Malaika Huwateremshia Mbao Zao Mtafutaji ‘Ilmu Na Wanaridhia Naye
عَنْ زِرِّ بْنِ حُبَيْشٍ، قَالَ أَتَيْتُ صَفْوَانَ بْنَ عَسَّالٍ الْمُرَادِيَّ فَقَالَ مَا جَاءَ بِكَ قُلْتُ أُنْبِطُ الْعِلْمَ . قَالَ فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ يَقُولُ " مَا مِنْ خَارِجٍ خَرَجَ مِنْ بَيْتِهِ فِي طَلَبِ الْعِلْمِ إِلاَّ وَضَعَتْ لَهُ الْمَلاَئِكَةُ أَجْنِحَتَهَا رِضًا بِمَا يَصْنَعُ " .
Zirr bin Hubaysh (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimwendea Swafwaan bin ‘Assaal Al-Muraadiyy akasema: Nini kilichokuleta? Nikasema: Kutafuta ‘Ilmu. Akasema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakuna yeyote atokaye kutoka nyumbani kwake kwa ajili ya kutafuta ‘Ilmu isipokuwa Malaika huteremsha mbawa zao wakiridhia analolifanya. “ [Ibn Maajah na ameisahihisha Imaam Al-Abaaniy: Swahiyh Ibn Maajah (186), Swahih Al-Jaami’ (5702)]