13-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kumuaga Rafiki na Kumuusia Mnapotengana Kwa Ajili ya Safari na Kumuombea na Kutaka Akuombee Duaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب وداع الصاحب ووصيته عند فراقه للسفر وغيره والدعاء لَهُ وطلب الدعاء مِنْهُ

13-Mlango Wa Kumuaga Rafiki na Kumuusia Mnapotengana Kwa Ajili ya Safari na Kumuombea na Kutaka Akuombee Duaa

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٣٢﴾

Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na (kadhalika) Ya’quwb (akawaambia): Enyi wanangu! Hakika Allaah Amekukhitarini nyinyi Dini; basi msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.

  

 أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾

Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamwabudu Ilaaha wako (Allaah) na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaah Mmoja, nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake. [Al-Baqarah: 132-133]

 

 

Hadiyth – 1

حديث زيد بن أرقم رضي الله عنه – الَّذِي سبق في بَابِ إكرام أهْلِ بَيْتِ رسول الله صلى الله عليه وسلم - قَالَ : قَامَ رسول الله صلى الله عليه وسلم فِينَا خَطِيباً ، فَحَمِدَ الله ، وَأثْنَى عَلَيْهِ ، وَوَعَظَ وَذَكَّرَ ، ثُمَّ قَالَ : (( أمَّا بَعْدُ ، ألاَ أيُّهَا النَّاسُ ، إنَّمَا أنَا بَشَرٌ يُوشِكُ أنْ يَأتِيَ رَسُولُ رَبِّي فَأُجِيبَ ، وَأنَا تَارِكٌ فِيكُمْ ثَقَلَيْنِ ، أوَّلَهُمَا : كِتَابُ اللهِ ، فِيهِ الْهُدَى وَالنُّورُ ، فَخُذُوا بِكِتَابِ اللهِ وَاسْتَمْسِكُوا بِهِ )) ، فَحَثَّ عَلَى كِتَابِ اللهِ ، وَرَغَّبَ فِيهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( وَأَهْلُ بَيْتِي ، أذَكِّرُكُمُ اللهَ في أهْلِ بَيْتِي )) رواه مسلم ، وَقَدْ سَبَقَ بِطُولِهِ .

Na miongoni mwa Hadiyth ni ile ya Zayd bin Arqam ambayo tumeitaja katika mlango wa kuwakirimu Watu wa Nyumbani wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Naye amesema: "Alisimama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mbele yetu siku moja kutuhutubia.' Kisha akasema: 'Ama baada:... Sikilizeni enyi watu! Hakika mimi ni mwanadamu, huenda akaja mjumbe kutoka kwa Rabb wangu nami nikamuitikia. Hivyo nimewaachia nyinyi vitu viwili vikubwa na muhimu, cha kwanza ni Kitabu cha Allaah ambacho ndani yake kuna uwongofu na nuru. Shikamaeni vilivyo na Kitabu cha Allaah. Akahimiza sana nukta hii na kututaka tukifuate. Kisha akasema: "Na familia yangu. Ninawakumbusha kwa jina la Allaah kuhusu familia yangu." [Muslim] 

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي سليمان مالِك بن الحُوَيْرِثِ رضي الله عنه، قَالَ : أَتَيْنَا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، وَنَحْنُ شَبَبَةٌ مُتَقَارِبُونَ، فَأقَمْنَا عِنْدَهُ عِشْرِينَ لَيْلَةً، وَكَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم رَحِيماً رَفيقاً ، فَظَنَّ أنّا قد اشْتَقْنَا أهْلَنَا ، فَسَألَنَا عَمَّنْ تَرَكْنَا مِنْ أهْلِنَا ، فَأخْبَرْنَاهُ ، فَقَالَ : (( ارْجِعُوا إِلَى أهْلِيكُمْ ، فَأقِيمُوا فِيهمْ ، وَعَلِّمُوهُم وَمُرُوهُمْ ، وَصَلُّوا صَلاَةَ كَذَا فِي حِيْنِ كَذَا ، وَصَلُّوا كَذَا في حِيْنِ كَذَا ، فَإذَا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ فَلْيُؤَذِّنْ لَكُمْ أحَدُكُمْ وَلْيَؤُمَّكُمْ أكْبَرُكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

زاد البخاري في رواية لَهُ : (( وَصَلُّوا كَمَا رَأيْتُمُونِي أُصَلِّي ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Sulaymaan Maalik bin Al-Huwayrith (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Tulikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tukiwa vijana na rika moja. Tulikaa kwake siku ishirini (20) na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mpole mwenye huruma. Alidhania ya kwamba sisi tunahamu na familia zetu, hivyo alituuliza kuhusu wale tuliowaacha nyuma katika watu wa familia zetu, nasi tukampasha habari kuhusu hilo. akasema: "Rejeeni kwa familia zenu na muwe pamoja nao, na wafundisheni na muwaamrishe na Swalini Swalaah kadhaa wakati kadhaa, na Swalini Swalaah wakati kadhaa. Swalaah inapofika awaadhinie mmoja wenu na awaongoze mkubwa wenu katika Swalaah." [Al-Bukhaariy na Muslim].

Al-Bukhaariy amezidisha katika riwaayah yake: "Na swalini kama mulivyoniona mimi nikiswali." 

 

 

Hadiyth – 3

وعن عمرَ بن الخطاب رضي الله عنه ، قَالَ : اسْتأذَنْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم في العُمْرَةِ ، فَأذِنَ ، وقال : (( لاَ تَنْسَانَا يَا أُخَيَّ مِنْ دُعَائِكَ )) فقالَ كَلِمَةً ما يَسُرُّنِي أنَّ لِي بِهَا الدُّنْيَا .

وفي رواية قَالَ : (( أشْرِكْنَا يَا أُخَيَّ في دُعَائِكَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khattaab (Radhwiya Allaah 'anhu) ambaye alisema: "Nilimuomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ruhusa ya kwenda kufanya Umrah, naye alinipatia idhini. Na akasema: 'Ee ndugu yangu! Usitusahau katika dua zako.' Akasema (Radhwiya Allaahu 'anhu): 'Hili ni neno ambalo sitataka kubadilishana hata na dunia yote." 

Na katika riwaayah nyengine, alisema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee ndugu yangu! Tushirikishe katika dua yako." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 4

وعن سالم بنِ عبدِ الله بنِ عمر : أنَّ عبدَ اللهِ بن عُمَرَ رضي الله عنهما، كَانَ يَقُولُ للرَّجُلِ إِذَا أرَادَ سَفَراً: ادْنُ مِنِّي حَتَّى أُوَدِّعَكَ كَمَا كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُوَدِّعُنَا ، فَيَقُولُ : (( أَسْتَوْدِعُ اللهَ دِينَكَ ، وَأمَانَتَكَ ، وَخَواتِيمَ عَمَلِكَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Saalimbin 'Abdillaah kwamba alikuwa 'Abdillaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) akimwambia mtu mwenye nia ya kusafiri: "Njoo karibu ili nikuage kama alivyokuwa akituaga Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kusema: Astawdi'u Allaah Diynaka wa Amanataka wa Khawaatiyma 'Amalika: Ninakuweka katika dhima ya Allaah kwa Dini yako, na amana yako na hatima ya amali zako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

 

Hadiyth – 5

وعن عبدِ الله بن يزيدَ الخطْمِيِّ الصحابيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أرَادَ أنْ يُوَدِّعَ الجَيشَ ، قَالَ : (( أسْتَوْدِعُ اللهَ دِينَكُمْ ، وَأمَانَتَكُمْ ، وَخَواتِيمَ أعْمَالِكُمْ )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود وغيره بإسناد صحيح .

Amesema 'Abdillaah bin Yaziyd Al-Khatmiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye ni Swahaaba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipotaka kuiaga jeshi alikuwa akiwaambia: "Ninawaageni na kuwaweka katika dhamana ya Allaah katika Dini yenu, amana zenu na mwisho wa amali zenu." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na wengineo kwa Isnaad Swahiyh].

 

 

Hadiyth – 6

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبي صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا رسولَ الله ، إنّي أُرِيدُ سَفَراً ، فَزَوِّدْنِي ، فَقَالَ : (( زَوَّدَكَ الله التَّقْوَى )) قَالَ : زِدْنِي قَالَ : (( وَغَفَرَ ذَنْبَكَ )) قَالَ : زِدْنِي ، قَالَ : (( وَيَسَّرَ لَكَ الْخَيْرَ حَيْثُمَا كُنْتَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ninataka kusafiri, hivyo naomba unipatie cha kunisaidia (yaani uniombee)." Akasema: "Allaah akuzidishie uchaji Mungu (Taqwaa)." Akasema yule mtu: "Nizidishie." Akasema: "Na akusamehe dhambi zako." Akasema (tena): "Nizidishie." Akasema: "Na akusahilishie kufanya kheri na mema popote ulipo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

 

Share