U-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari: 'Uwaymir Bin Zayd (Abu Dardaa)
A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari
‘Uwaymir Bin Zayd (Abu Dardaa) (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
Jina Lake: ‘Uwaymir Bin Zayd (Abu Dardaa)
Al-Answaariy
عويمر بن زيد
Maana Yake:
‘Uwaymir - (Kifupisho Cha ‘Aamir) Maana yake ni kuthibitika katika Iymaan, harufu nzuri, mwenye utulivu, mwenye kuamirisha, mjenzi, mwenye kupitisha umri mrefu
Wengine wasema jina lake ni ‘Uwaymiyr bin ‘Aamir, au ‘Uwaymir bin ‘Abdullaah, au ‘Uwaymir bin Tha’labah.
Dardaa Maana yake ni Lulu ya hikmah
Wasifu Wake:
Abu Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa tajiri na maarufu huko Madiyna na kila mtu alimpenda na kumheshimu.
Ni Swahaba mwenye hekima na busara. Abu Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) hakuzaliwa kwenye Uislaam, bali alisilimu baada ya vita vya Badr.
Iymaan yake katika Uislaam ilikuwa kutokutilia umuhimu wa kuwa na utajiri wa kidunia. Alisema “Nilikuwa mfanyabiashara kabla ya Unabiy wa Nabiy Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Wakati Uislamu ulipokuja, nilitafuta kuchanganya biashara na ‘ibaadah lakini hivi viwili havikuungana hivyo niliachana na biashara na nikachagua ‘ibaadah.
Kufariki Kwake:
Abu Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki akiwa na umri wa miaka 72. Kaburi lake lipo ndani ya Msikiti wa jina lake; Abu Dardaa huko Damascus mjini Syria.