03-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miujiza Yake: Kupasuka Mwezi
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
03-Miujiza Yake: Kupasuka Mwezi
Quraysh wa Makkah katika inadi zao walimtaka Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) awaonyeshe muujiza, basi Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Akaleta muujiza wa kupasuka mwezi mbele ya macho yao, lakini kama kawaida yao waliendelea kumfanyia inadi na istihzai. Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾ وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾
Saa imekaribia na mwezi umepasuka. Na wanapoona Aayah (ishara, dalili) hukengeuka na husema: Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]
Na Hadiyth zifuatazo pia zinaelezea tukio hilo la muujiza wa kupasuka mwezi:
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ سَأَلَ أَهْلُ مَكَّةَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم آيَةً فَانْشَقَّ الْقَمَرُ بِمَكَّةَ مَرَّتَيْنِ فَنَزَلَت: ((اقتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ)) إِلَى قَوْلِهِ : ((سحْرٌ مُسْتَمِرٌّ)) يَقُولُ ذَاهِبٌ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba watu wa Makkah walimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awaletee Aayah (Ishara, muujiza), basi mwezi ukapasuka Makkah mara mbili (Yaani sehemu mbili), kisha ikateremka:
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾
Saa imekaribia na mwezi umepasuka
Mpaka kauli Yake:
سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ
Na pia,
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ انْشَقَّ الْقَمَرُ وَنَحْنُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بِمِنًى فَقَالَ " اشْهَدُوا ". وَذَهَبَتْ فِرْقَةٌ نَحْوَ الْجَبَلِ
Amesimulia ‘Abdallaah bin Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Mwezi ulipasuka (na kuwa vipande viwili) wakati tukiwa pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) huko Minaa. Akasema, "Shuhudieni." Kisha kipande cha mwezi kikaelekea upande wa mlima. [Al-Bukhaariy]
Na pia,
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ انْشَقَّ الْقَمَرُ وَنَحْنُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَصَارَ فِرْقَتَيْنِ، فَقَالَ لَنَا " اشْهَدُوا، اشْهَدُوا ".
Amesimulia ‘Abdallaah bin Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Ulipasuka mwezi wakati wa uhai wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) vipande viwili akatuambia: “Shuhudieni! Shuhudieni! [Al-Bukhaariy]
Na pia,
عَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، قَالَ: انْشَقَّ الْقَمَرُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ فَصَارَ فِرْقَتَيْنِ: فِرْقَةٌ عَلَى هَذَا الْجَبَلِ، وَفِرْقَةٌ عَلَى هَذَا الْجَبَلِ، فَقَالُوا: سَحَرَنَا مُحَمَّدٌ. فَقَالُوا: إِنْ كَانَ سَحَرَنَا فَإِنَّهُ لَا يَسْتَطِيعُ أَنْ يَسْحَرَ النَّاسَ كُلَّهُمْ.
Jubayr bin Mutw'im (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisema: "Mwezi ulipasuka vipande viwili zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na sehemu ya mwezi ulikuwa juu ya mlima na sehemu nyingine kwenye mlima mwingine. Wakasema (makafiri) "Muhammad ametufanyia sihri (uchawi)". Kisha wakasema: "Angeliweza kututeka kwa sihri asingeliweza kufanya kwa watu wote" [Imaam Ahmad]
Na Riwaayah nyenginezo kama hizo zimethibiti pia.