05-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake: Kumkatalia Aliyetaka Kuzini Kisha Akamuombea Du’aa
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
05-Hikmah Zake: Kumkatalia Aliyetaka Kuzini Kisha Akamuombea Du’aa
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ قَالَ إِنَّ فَتًى شَابًّا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ ائْذَنْ لِي بِالزِّنَا فَأَقْبَلَ الْقَوْمُ عَلَيْهِ فَزَجَرُوهُ قَالُوا مَهْ مَهْ فَقَالَ ادْنُهْ فَدَنَا مِنْهُ قَرِيبًا قَالَ فَجَلَسَ قَالَ أَتُحِبُّهُ لِأُمِّكَ قَالَ لَا وَاللَّهِ جَعَلَنِي اللَّهُ فِدَاءَكَ قَالَ وَلَا النَّاسُ يُحِبُّونَهُ لِأُمَّهَاتِهِمْ قَالَ أَفَتُحِبُّهُ لِابْنَتِكَ قَالَ لَا وَاللَّهِ يَا رَسُولَ اللَّهِ جَعَلَنِي اللَّهُ فِدَاءَكَ قَالَ وَلَا النَّاسُ يُحِبُّونَهُ لِبَنَاتِهِمْ قَالَ أَفَتُحِبُّهُ لِأُخْتِكَ قَالَ لَا وَاللَّهِ جَعَلَنِي اللَّهُ فِدَاءَكَ قَالَ وَلَا النَّاسُ يُحِبُّونَهُ لِأَخَوَاتِهِمْ قَالَ أَفَتُحِبُّهُ لِعَمَّتِكَ قَالَ لَا وَاللَّهِ جَعَلَنِي اللَّهُ فِدَاءَكَ قَالَ وَلَا النَّاسُ يُحِبُّونَهُ لِعَمَّاتِهِمْ قَالَ أَفَتُحِبُّهُ لِخَالَتِكَ قَالَ لَا وَاللَّهِ جَعَلَنِي اللَّهُ فِدَاءَكَ قَالَ وَلَا النَّاسُ يُحِبُّونَهُ لِخَالَاتِهِمْ فَوَضَعَ يَدَهُ عَلَيْهِ وَقَالَ اللَّهُمَّ اغْفِرْ ذَنْبَهُ وَطَهِّرْ قَلْبَهُ وَحَصِّنْ فَرْجَهُ فَلَمْ يَكُنْ بَعْدُ ذَلِكَ الْفَتَى يَلْتَفِتُ إِلَى شَيْءٍ
وفي رواية أخرى فَقَالَ لَهُ فَاكْرَهْ مَا كَرِهَ اللَّهُ وَأَحِبَّ لأَخِيكَ مَا تُحِبُّ لِنَفْسِكَ
Amesimulia Abu Umaamah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Kijana mmoja alimjia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niruhusu nizini! Watu wakamgeukia kumtuhumu wakasema: Nyamaza! Nyamaza! Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: “Njoo hapa!” Kijana akakaribia akamwambia akae kitako. Kisha akamuuliza: “Je utapendelea hivyo (kuzini) kwa mama yako?” Kijana akajibu: Hapana wa-Allaah, nifidiwe kwa ajili yako! Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: “Basi hata watu hawatopendelea hivyo kwa mama zao.” Akasema tena: “Je utapendelea hivyo kwa binti yako?” Kijana akajibu: Hapana ee Rasuli wa Allaah, nifidiwe kwa ajili ya yako! Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: “Hata watu basi hawatopendelea hivyo kwa binti zao.” Akasema: “Je utapendelea hivyo kwa dada yako?” Akajibu: Hapana wa-Allaahi nifidiwe kwa ajili yako! Akasema: “Basi hata watu hawatopendelea kwa dada zao.” Akasema: “Je utapendelea hivyo kwa ammat (shangazi) yako?” Akasema: Hapana wa-Allaah, nifidiwe kwa ajili yako! Akasema: “Hata watu hawatopendelea kwa ‘ammaat zao.” Akasema: “Je utapendelea hivyo kwa khaalat (mama mkubwa na mdogo) wako?” Akajibu: “Hapana wa-Allaahi nifidiwe kwa ajili yako! Akasema: “Hata watu hawatopendelea hivyo kwa makhaalaat zao.” Akaweka mkono wake juu yake akamwombea:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ ذَنْبَهُ وَطَهِّرْ قَلْبَهُ وَحَصِّنْ فَرْجَهُ
“Ee Allaah Mghufurie dhambi zake, na utakase moyo wake, na mhifadhi uchi wake.”
Baada ya hapo, kijana huyo hakuelemea tena katika lolote (la dhambi).
Na katika Riwaayah: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alimwambia: “Basi chukia Analochukia Allaah, na mpendelee nduguyo unalopendelea nafsi yako.” [Musnad Ahmad (22211), Isnaad yake Swahiyh watu wake ni Swahiyh wa Thiqqah, na Al-Bayhaqiy katika Shu’b Al-Iymaan (5032), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (370)]