10-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kula Kwa Vidole Vitatu na Sunnah ya Kuramba Vidole na Karaha ya Kuvifuta Kabla ya Kuviramba na Kupendeza Kuramba Sahani na Kuchukua Tonge Lililo Anguka na Kulila
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب الأكل بثلاث أصابع واستحباب لعق الأصابع ، وكراهة مسحها قبل لعقهاواستحباب لعق القصعة وأخذ اللقمة الَّتي تسقط منه وأكلها ومسحها بعد اللعق بالساعد والقدم وغيرها
10-Mlango Wa Kupendeza Kula Kwa Vidole Vitatu na Sunnah ya Kuramba Vidole na Karaha ya Kuvifuta Kabla ya Kuviramba na Kupendeza Kuramba Sahani na Kuchukua Tonge Lililo Anguka na Kulila
Hadiyth – 1
عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أكَلَ أَحَدُكُمْ طَعَاماً ، فَلاَ يَمْسَحْ أَصَابِعَهُ حَتَّى يَلْعَقَهَا أَوْ يُلْعِقَها )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokula mmoja wenu asiufute mkono wake mpaka aurambe au aurambishe." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abuu Daawuwd]
Hadiyth – 2
وعن كعب بن مالك رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يَأكُلُ بثَلاَثِ أصابعَ ، فإذا فَرَغَ لَعِقَهَا . رواه مسلم .
Amesema Ka'b bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akila chakula kutumia vidole vitatu na anapomaliza alikuwa akiviramba. [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أمر بلعق الأصابع والصحفة ، وقال : (( إنَّكُمْ لاَ تَدْرُونَ في أيِّ طَعَامِكُمُ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha kurambwa vidole na sahani na akasema: "Hakika nyinyi hamjui ni katika sehemu gani ya chakula chenu imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أحَدِكُمْ ، فَلْيأخُذْهَا فَلْيُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً ، وَلْيَأْكُلْهَا ، وَلاَ يَدَعْهَا لِلشَّيْطَان ، وَلاَ يَمْسَحْ يَدَهُ بالمِنْدِيل حَتَّى يَلْعَقَ أصَابِعَهُ ، فَإنَّهُ لاَ يَدْري في أيِّ طَعَامِهِ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ikianguka tonge la mmoja wenu na aliokote na aondoshe uchafu na alile wala asimwachie shetani. Pia asifute mkono wake kwa kitambara mpaka avirambe vidole vyake, kwani yeye hajui ni sehemu gani ya chakula chake imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ الشَّيْطَانَ يَحْضُرُ أحَدَكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيْءٍ مِنْ شَأنِهِ ، حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ ، فإذَا سَقَطَتْ لُقْمَةُ أحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً ، ثُمَّ لِيَأْكُلْهَا وَلاَ يَدَعْهَا للشَّيْطَانِ ، فإذا فَرَغَ فَلْيَلْعَقْ أصابِعَهُ ، فإنَّهُ لا يَدْري في أيِّ طعامِهِ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Imepokes kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika shetani anahudhuria pamoja na mmoja wenu katika mambo yake yote mpaka anakuwa pamoja naye anapokula. Hivyo, linapoanguka tonge la mmoja wenu na aliokote na aliondoshe uchafu, kisha alile wala asimuachie shetani. Anapomaliza kula na avirambe vidole vyake, kwani hakika yake hajui ni sehemu gani chakula imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أكَلَ طَعَاماً ، لَعِقَ أصَابِعَهُ الثَّلاَثَ ، وقال : (( إِذَا سقَطَتْ لُقْمَةُ أحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا ، ولْيُمِطْ عنها الأذى ، وَليَأكُلْهَا ، وَلاَ يَدَعْها لِلْشَّيْطَان )) وأمَرَنا أن نَسْلُتَ القَصْعَةَ ، وقال : (( إنَّكُمْ لا تَدْرُونَ في أيِّ طَعَامِكُمُ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alipokuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akila chakula, akiviramba vidolevyake vitatu, na akasema: "Ikianguka tonge ya mmoja wenu na aliokote na aondoshe uchafu na aile wala asimuachie shetani kabisa, na akasema: "Hakika nyinyi hamjui ni katika sehemu gani ya chakula chenu imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن سعيد بنِ الحارث : أنّه سأل جابراً رضي الله عنه عنِ الوُضُوءِ مِمَّا مَسَّتِ النَّارُ ، فَقَالَ : لا ، قَدْ كُنَّا زَمَنَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم لا نَجِدُ مِثْلَ ذَلِكَ الطَّعامِ إِلاَّ قليلاً ، فإذا نَحْنُ وجَدْنَاهُ ، لَمْ يَكُنْ لنا مَنَادِيلُ إِلاَّ أكُفَّنا ، وسَواعِدَنَا ، وأقْدامَنَا ، ثُمَّ نُصَلِّي وَلاَ نَتَوَضَّأُ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Haarith kwamba alimuuliza Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) : "Je, ni wajibu wa kuchukua wudhu baada ya kula chakula kilichopikwa kwa moto?" Alisema: "Hapana! Hakika sisi tulikuwa katika zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nadhra kupata mfano wa chakula hicho; na tulipokuwa tukipata chakula aina hiyo basi hatukuwa na kitambara cha kufuta vitanga vyetu, mkono yetu na miguu yetu, kisha tulikuwa tunaswali bila ya kutawadha." [Al-Bukhaariy]