12-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Adabu za Kunywa na Kupendeza Kupumua Mara Tatu Nje ya Chombo na Karaha Kupumua Ndani ya Chombo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب أدب الشرب واستحباب التنفس ثلاثاً خارج الإناء وكراهة التَّنَفُّس في الإناء واستحباب إدارة الإناء عَلَى الأيمن فالأيمن بعد المبتدئ

12-Mlango Wa Adabu za Kunywa na Kupendeza Kupumua Mara Tatu Nje ya Chombo na Karaha Kupumua Ndani ya Chombo

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يَتَنَفَّسُ في الشَّرابِ ثَلاثاً . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipumua mara tatu nje ya chombo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  لاَ تَشْرَبُوا وَاحِداً كَشُرْبِ البَعِيرِ ، وَلَكِنِ اشْرَبُوا مَثْنَى وَثُلاَثَ ، وَسَمُّوا إِذَا أنْتُمْ شَرِبْتُمْ ، وَاحْمَدُوا إِذَا أنْتُمْ رَفَعْتُمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msinywe kwa mara moja (mkupuo mmoja) kama anavyokunywa ngamia lakini kunyweni mara mbili na tatu. Na litajeni jina la Allaah mnapokunywa na mshukuruni kwa kumsifu pindi mnapomaliza." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي قَتَادَة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى أنْ يُتَنَفَّسَ في الإناءِ . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupumua ndani ya chombo (hicho anachokunywia maji)." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أُتِيَ بِلَبَنٍ قَدْ شِيبَ بماءٍ ، وَعَنْ يَمِينهِ أعْرَابيٌّ ، وَعَنْ يَسَارِهِ أَبُو بَكْر رضي الله عنه ، فَشَرِبَ ، ثُمَّ أعْطَى الأعْرابيَّ ، وقال : ((  الأيْمَنَ فالأيْمَنَ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa maziwa yaliyochanganywa na maji, na kulikuwa na badui kuliani mwake na Abu Bakr (Radhwiya Allahu 'anhu) alikuwa kushotoni mwake. Alikunywa kisha akampa yule Mbedui, na akasema: "Kuliani, kuliani." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن سهلِ بن سعدٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أُتِيَ بِشرابٍ ، فَشَرِبَ مِنْهُ وَعَنْ يَمِينِهِ غُلامٌ ، وَعَنْ يَسَارِهِ أشْيَاخٌ ، فَقَالَ للغُلامِ : ((  أتَأْذَنُ لِي أنْ أُعْطِيَ هؤُلاَءِ ؟ )) فَقَالَ الغُلامُ : لا واللهِ ، لا أُوثِرُ بنَصيبـي مِنْكَ أَحَداً . فَتَلَّهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم في يَدِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa kinywaji, akanywa kutoka kwayo, na kuliani kwake alikuwepo kijana na kushotoni kwake kulikuwa na mzee. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamuuliza yule kijana: "Utaniruhusu niwape hawaa (yaani wazee)?" Yule kijana akajibu: "Naapa kwa Allaah! simpendelei yeyote achukuwe hisa yangu kutoka kwako." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akampa huyo kijana kile kinywaji kwenye mkono wake. [Al-Bukhaariy na Muslim] . Na huyu kijana alikuwa ni 'Abdallaah bin 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu)

 

 

 

 

Share