12-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Miongoni Mwa Uzuri Wa Uislamu Wa Mtu
Hadiyth Ya 12
مِنْ حُسْنِ إسْلاَمِ الْمَرْءِ
Miongoni Mwa Uzuri Wa Uislamu Wa Mtu
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مِنْ حُسْنِ إسْلاَمِ الْمَرْءِ تَرْكُهُ مَا لاَ يَعْنِيهِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ، وَغَيره هكذا
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Miongoni mwa uzuri wa Uislamu wa mtu, ni kuacha yale yasiyomuhusu.” [Hadiyth Hasan, Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na wengineo]