06-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miujiza Yake: Vidole Vyake Kutoa Maji Tele
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
06-Miujiza Yake: Vidole Vyake Kutoa Maji Tele
Hadiyth kadhaa zimethibiti kuhusu muujiza wa kutoka maji tele katika vidole vya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم); miongoni mwazo ni zifuatazo:
Hadiyth Ya 1:
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي عَدِيٍّ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ أُتِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِإِنَاءٍ وَهْوَ بِالزَّوْرَاءِ، فَوَضَعَ يَدَهُ فِي الإِنَاءِ، فَجَعَلَ الْمَاءُ يَنْبُعُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِهِ، فَتَوَضَّأَ الْقَوْمُ. قَالَ قَتَادَةُ قُلْتُ لأَنَسٍ كَمْ كُنْتُمْ قَالَ ثَلاَثَمِائَةٍ، أَوْ زُهَاءَ ثَلاَثِمِائَةٍ.
Amesimulia Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Bakuli la maji ililetwa kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alipokuwa Az-Zawraai. Alitia mkono wake ndani yake, maji yakaanza kutoka vidoleni mwake. Watu wote walitawadha (na maji hayo). Qataadah alimuuliza Anas: “Mlipokuwa wangapi?” Akasema: “Mia tatu au karibu na mia tatu”. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
Hadiyth Ya 2:
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، حَدَّثَنَا أَبُو أَحْمَدَ الزُّبَيْرِيُّ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنَّا نَعُدُّ الآيَاتِ بَرَكَةً وَأَنْتُمْ تَعُدُّونَهَا تَخْوِيفًا، كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَقَلَّ الْمَاءُ فَقَالَ " اطْلُبُوا فَضْلَةً مِنْ مَاءٍ ". فَجَاءُوا بِإِنَاءٍ فِيهِ مَاءٌ قَلِيلٌ، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِي الإِنَاءِ، ثُمَّ قَالَ " حَىَّ عَلَى الطَّهُورِ الْمُبَارَكِ، وَالْبَرَكَةُ مِنَ اللَّهِ " فَلَقَدْ رَأَيْتُ الْمَاءَ يَنْبُعُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، وَلَقَدْ كُنَّا نَسْمَعُ تَسْبِيحَ الطَّعَامِ وَهْوَ يُؤْكَلُ.
Amesimulia ‘Abdullaah (رضي الله عنه): Tulikuwa tukichukulia miujiza kuwa ni Baraka ya Allaah, lakini nyinyi mnachukulia kuwa ni onyo na tahadhari. Wakati mmoja tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini, nasi tukapungukiwa na maji. Akasema: “Nileteeni maji mliyo nayo.” Watu walileta chombo kilichokuwa na maji kidogo. Alitia mkono wake ndani yake, akasema: “Njooni kwenye maji ya Baraka na Baraka inatoka kwa Allaah.” Niliyaona maji yakitoka kutoka kwenye vidole vya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kwa hakika tulikuwa tunasikia chakula kikileta Tasbiyh (Subhaana Allaah) kilipokuwa kinaliwa na yeye. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
Hadiyth Ya 3:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ إِسْحَاقَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّهُ قَالَ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَحَانَتْ صَلاَةُ الْعَصْرِ، فَالْتَمَسَ النَّاسُ الْوَضُوءَ فَلَمْ يَجِدُوهُ، فَأُتِيَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِوَضُوءٍ، فَوَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي ذَلِكَ الإِنَاءِ يَدَهُ، وَأَمَرَ النَّاسَ أَنْ يَتَوَضَّئُوا مِنْهُ. قَالَ فَرَأَيْتُ الْمَاءَ يَنْبُعُ مِنْ تَحْتِ أَصَابِعِهِ حَتَّى تَوَضَّئُوا مِنْ عِنْدِ آخِرِهِمْ
Amesimulia Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) wakati ambapo Swalaah ya Alasiri ilikuwa imekaribia. Watu wakawa wanatafuta maji kwa ajili ya kushika wudhu lakini hawakuweza kupata (maji). Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aliletewa maji, naye Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akatia mkono wake katika chombo hicho cha maji, kisha akawaamuru watu washike wudhu kwa maji hayo. Niliona maji yakitoka chini ya vidole vyake na watu wakaanza kuchukua wudhu mpaka wote wakamaliza kushika wudhu. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
Hadiyth Ya 4:
حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا حُصَيْنٌ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ عَطِشَ النَّاسُ يَوْمَ الْحُدَيْبِيَةِ، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ يَدَيْهِ رَكْوَةٌ فَتَوَضَّأَ فَجَهَشَ النَّاسُ نَحْوَهُ، فَقَالَ " مَا لَكُمْ ". قَالُوا لَيْسَ عِنْدَنَا مَاءٌ نَتَوَضَّأُ وَلاَ نَشْرَبُ إِلاَّ مَا بَيْنَ يَدَيْكَ، فَوَضَعَ يَدَهُ فِي الرَّكْوَةِ فَجَعَلَ الْمَاءُ يَثُورُ بَيْنَ أَصَابِعِهِ كَأَمْثَالِ الْعُيُونِ، فَشَرِبْنَا وَتَوَضَّأْنَا. قُلْتُ كَمْ كُنْتُمْ قَالَ لَوْ كُنَّا مِائَةَ أَلْفٍ لَكَفَانَا، كُنَّا خَمْسَ عَشْرَةَ مِائَةً.
Amesimulia Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Watu walishikwa na kiu siku ya Hudaybiyah. Chombo kidogo kilichokuwa na maji kidogo kilikuwa mbele ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na alipomaliza kutawadha, watu walikimbilia kwake. Akauliza: “Mna nini?” Wakasema: “Sisi hatuna maji ya kutawadhia au ya kunywa isipokuwa yaliyo mbele yako.” Basi alitia mkono wake kwenye chombo hicho, maji yakaanza kutoka kwenye vidole vyake kama mfano wa kijito. Sote tulikunywa na kutawadha (kwa maji hayo). Nikamuuliza Jaabir, “Je, mlikuwa wangapi?” Akajibu: “Hata kama tungelikuwa laki moja (elfu mia moja – 100,000) ingewatosha, lakini tulikuwa elfu moja na mia tano.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]