08-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake: Kuacha Khutbah Kumlingania Aliyetaka Kujua Kuhusu Dini

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 08-Hikma Zake: Kuacha Khutbah Kumlingania Aliyetaka Kujua Kuhusu Dini   

  

Alhidaaya.com

 

 

 

Katika hikma zake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ni kuwa alikuwa na himma kubwa ya kuwafundisha waliotaka kujua kuhusu Uislaam. Himma yake ilikuwa hadi kuacha kukhutubia khutbah katika minbari ili amsikilize mtu aliyeingia Misikitini kutaka kujua kuhusu Uislaam:

 

عن أَبي رِفَاعَةَ تَميم بن أُسَيْدٍ رضي الله عنه ، قَالَ : انْتَهَيْتُ إِلَى رَسولِ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يخطب ، فقلت : يَا رسول الله ، رَجُلٌ غَريبٌ جَاءَ يَسْألُ عن دِينهِ لا يَدْرِي مَا دِينُهُ ؟ فَأقْبَلَ عَليَّ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وتَرَكَ خُطْبَتَهُ حَتَّى انْتَهَى إلَيَّ ، فَأُتِيَ بِكُرْسيٍّ ، فَقَعَدَ عَلَيْهِ ، وَجَعَلَ يُعَلِّمُنِي مِمَّا عَلَّمَهُ اللهُ ، ثُمَّ أَتَى خُطْبَتَهُ فَأتَمَّ آخِرَهَا . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Rifaa'ah Tamim bin Usayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ambaye amesema: "Nilifika kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  akiwa anakhutubia (khutbah), nami nikamuuliza: 'Ee Rasuli wa Allaah! Mtu mgeni amekuja kuuliza kuhusu Dini yake kwani yeye hajui chochote kuhusu Dini yake?' Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alinikabili na akaja kwangu. Aliletewa kiti, akakikalia. Akawa ananifundisha aliyofundishwa na Allaah. Kisha alijia khutbah yake akaitimiza." [Muslim]

 

 

Share