10-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake: Ugawaji Wa Ghanima Kwa Muhaajiruwn Na Waliosilimu Badala Ya Kuwagaia Answaar
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake:
10- Ugawaji Wa Ghanima Kwa Muhaajiruwn Na Waliosilimu Badala Ya Kuwagaia Answaar
Kutokana na hikma zake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) baada ya vita vya Hunayn, aliwagaia ghanima (mateka ya vita) Muhaajiruwna na Atw-Twulaqaa (waliosilimu) kwa sababu alitaka kuwatia nguvu nyoyo zao katika kupenda Uislaam ili wathibitike. Lakini Answaar kwanza hawakarudhika kwa kutokufahamu hikma yake. Kisha walipotambua sababu ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) kufanya hivyo na kwamba aliwapendelea wao zaidi warudi naye (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na aliposema kuwaambia:
“Kama watu wangepita njia ya bondeni na Anaswaar wakapitia nja ya milimani, kwa hakika, ningepita njia ya milimani ya Answaar.”
Wakafahamu kuwa chaguo hilo la kutokupokea ghanima na badala yake kurudi na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم), lilikuwa bora zaidi kwao kwani ni chaguo la kuwa pamoja naye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na ni chaguo la kupendelea Aakhirah badala ya mafao ya dunia ambayo walipewa Atw-Twulaqaa na Muhaajiruwn, na kutokana na mapenzi yao juu yake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na ahadi zao za kunusuru Dini ya Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) na kumnusuru Rasuli Wake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم):
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ مُعَاذٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ زَيْدِ بْنِ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمُ حُنَيْنٍ أَقْبَلَتْ هَوَازِنُ وَغَطَفَانُ وَغَيْرُهُمْ بِنَعَمِهِمْ وَذَرَارِيِّهِمْ، وَمَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم عَشَرَةُ آلاَفٍ وَمِنَ الطُّلَقَاءِ، فَأَدْبَرُوا عَنْهُ حَتَّى بَقِيَ وَحْدَهُ، فَنَادَى يَوْمَئِذٍ نِدَاءَيْنِ لَمْ يَخْلِطْ بَيْنَهُمَا، الْتَفَتَ عَنْ يَمِينِهِ، فَقَالَ " يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ". قَالُوا لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَبْشِرْ نَحْنُ مَعَكَ. ثُمَّ الْتَفَتَ عَنْ يَسَارِهِ، فَقَالَ " يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ". قَالُوا لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَبْشِرْ نَحْنُ مَعَكَ. وَهْوَ عَلَى بَغْلَةٍ بَيْضَاءَ، فَنَزَلَ فَقَالَ " أَنَا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ "، فَانْهَزَمَ الْمُشْرِكُونَ، فَأَصَابَ يَوْمَئِذٍ غَنَائِمَ كَثِيرَةً، فَقَسَمَ فِي الْمُهَاجِرِينَ وَالطُّلَقَاءِ وَلَمْ يُعْطِ الأَنْصَارَ شَيْئًا، فَقَالَتِ الأَنْصَارُ إِذَا كَانَتْ شَدِيدَةٌ فَنَحْنُ نُدْعَى، وَيُعْطَى الْغَنِيمَةَ غَيْرُنَا. فَبَلَغَهُ ذَلِكَ، فَجَمَعَهُمْ فِي قُبَّةٍ، فَقَالَ " يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ مَا حَدِيثٌ بَلَغَنِي عَنْكُمْ ". فَسَكَتُوا فَقَالَ " يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ أَلاَ تَرْضَوْنَ أَنْ يَذْهَبَ النَّاسُ بِالدُّنْيَا، وَتَذْهَبُونَ بِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم تَحُوزُونَهُ إِلَى بُيُوتِكُمْ ". قَالُوا بَلَى. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " لَوْ سَلَكَ النَّاسُ وَادِيًا، وَسَلَكَتِ الأَنْصَارُ شِعْبًا لأَخَذْتُ شِعْبَ الأَنْصَارِ ". فَقَالَ هِشَامٌ يَا أَبَا حَمْزَةَ، وَأَنْتَ شَاهِدٌ ذَاكَ قَالَ وَأَيْنَ أَغِيبُ عَنْهُ
Amesimulia Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Wakati wa vita vya Hunayn, makabila ya Hawaazin, Ghatwafaan na wengine, pamoja na wanyama wao na watoto (na wanawake) walikuja kupigana dhidi ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alikuwa na watu elfu kumi katika Atw-Twulaqaa (Waislamu wapya wa Makkah). Wakakimbia na kumwacha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaita mara mbili bila kuchanganya wito huo. Akageukia upande wa kuume na kusema, “Enyi kundi la Answaar!” Wakaitika: "Labbayka, ee Rasuli wa Allah! Pokea bishara, kwani sisi tuko pamoja nawe!” Akageukia upande wa kushoto na kusema, “Ee kundi la Answaar!” Wakasema: “Labbayka ee Rasuli wa Allaah, pokea bishara, kwani sisi tuko pamoja nawe!” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) wakati huo alikuwa juu ya nyumbu mweupe, kisha akashuka na kusema, "Mimi ni Mja wa Allaah na Rasuli Wake.” Makafiri wakashindwa na katika siku hiyo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alipata kiasi kikubwa cha ghanima ambayo aliwagawia Muhaajiruwn na Atw-Twulaqaa na hakuwapa chochote Answaar. Mtu mmoja katika Answaar akasema: "Kunapokuwa na shida tunaitwa, lakini ghanima wanapewa wengine.” Khabari zikamfikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na yeye akawakusanya chini ya hema la ngozi na kuwaambia: "Ni khabari gani zilizonifikia kutoka kwenu enyi kundi la Answaar?” Wakanyamaza. Akaongeza: “Enyi kundi la Answaar! Je, hamtaridhia watu wachukue vitu vya kidunia na nyinyi mwondoke pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) majumbani mwenu?” Wakajibu: “Ndiyo.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akasema: “Kama watu wangepita njia ya bondeni na Answaar wakapitia nja ya milimani, kwa hakika, ningepita njia ya milimani ya Answaar.” Hisham akasema: “Ee Abu Hamzah (yaani, Anas)! Ulishuhudia hayo?” Akajibu, "Ningekuwaje mbali na hilo?” [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib, Muslim Kitaab Az-Zakaah]
Na Riwaayah nyengine:
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَزْهَرُ، عَنِ ابْنِ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ زَيْدِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمَ حُنَيْنٍ الْتَقَى هَوَازِنُ وَمَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم عَشَرَةُ آلاَفٍ وَالطُّلَقَاءُ فَأَدْبَرُوا قَالَ " يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ". قَالُوا لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَسَعْدَيْكَ، لَبَّيْكَ نَحْنُ بَيْنَ يَدَيْكَ، فَنَزَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " أَنَا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ ". فَانْهَزَمَ الْمُشْرِكُونَ، فَأَعْطَى الطُّلَقَاءَ وَالْمُهَاجِرِينَ وَلَمْ يُعْطِ الأَنْصَارَ شَيْئًا فَقَالُوا، فَدَعَاهُمْ فَأَدْخَلَهُمْ فِي قُبَّةٍ فَقَالَ " أَمَا تَرْضَوْنَ أَنْ يَذْهَبَ النَّاسُ بِالشَّاةِ وَالْبَعِيرِ، وَتَذْهَبُونَ بِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم "، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم "لَوْ سَلَكَ النَّاسُ وَادِيًا وَسَلَكَتِ الأَنْصَارُ شِعْبًا لاَخْتَرْتُ شِعْبَ الأَنْصَارِ "
Amesimulia Anas Bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ):
Katika siku ya (vita vya) Hunayn, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aliwakabili kabila la Hawaazin ilhali kulikuwa na watu elfu kumi na Atw-Twulaqaa (waliosilimu katika Siku ya Fat-h [ukombozi] wa Makkah) pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). (Waislamu) walipokimbia, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) aliwaambia, “Enyi kundi la Answaar!” Wakajibu: "Labbayka, Ee Rasuli wa Allaah wa Sa’dayka! Tuko chini ya amri yako.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akateremka chini (kutoka juu ya nyumbu wake) na kusema: "Mimi ni Mja wa Allaah na Rasuli Wake.” Washirikina wakashindwa vita. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akawagawia ghanima (mateka) ya vita Atw-Twulaqaa na Muhaajiruwn na hakuwapa chochote Answaar. Answaar wakasema (maneno ya kutoridhika) basi akawaita na kuwakaribisha chini ya hema la ngozi na kuwaambia: "Je, hamtoridhia kuwa wao wamechukua kondoo na ngamia na nyinyi mtaondoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)?” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaongeza: “Kama watu wangepita njia ya bondeni na Answaar wakapita njia ya milimani, basi ningepita njia ya milimani ya Answaar." [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Maghaazi]