05-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuwa Kati na Kati Katika Mavazi na Kujiepusha na Mavazi Fulani Bila ya Haja Wala Makusudio ya Kisheria
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب التوسط في اللباس وَلاَ يقتصر عَلَى مَا يزري بِهِ لغير حاجة وَلاَ مقصود شرعي
05-Mlango Wa Kupendeza Kuwa Kati na Kati Katika Mavazi na Kujiepusha na Mavazi Fulani Bila ya Haja Wala Makusudio ya Kisheria
عن عمرو بن شعيب ، عن أبيهِ ، عن جَدِّهِ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ يُحِبُّ أنْ يُرَى أثَرُ نِعْمَتِهِ عَلَى عَبْدِهِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Shu'ayb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah anapenda kuona athari ya neema Yake kwa mja Wake." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan]