14-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Haipasi Kumwagwa Damu Ya Muislamu Isipokuwa Kwa Sababu Tatu
Hadiyth Ya 14
لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ
Haipasi Kumwagwa Damu Ya Muislamu Isipokuwa Kwa Sababu Tatu
عن ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ: الثَّيِّبُ الزَّاني، وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيّ وَمُسْلِمٌ
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Haipasi kumwagwa damu ya Muislamu isipokuwa kwa sababu tatu: Mzinifu aliyeolewa, uhai kwa uhai, na anayeacha Dini na akajifarikisha na jamaa-‘ah.” [Al-Bukhaariy, Muslim]