01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Adabu za Kulala na Kujilaza na Kukaa na Kikao na Waliomo katika Kikao na Ndoto
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب آداب النَوم والاضْطِجَاع وَالقعُود والمَجلِس وَالجليس وَالرّؤيَا
01-Mlango Wa Adabu za Kulala na Kujilaza na Kukaa na Kikao na Waliomo katika Kikao na Ndoto
Hadiyth – 1
عن البَراءِ بن عازِبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أوَى إِلَى فِرَاشِهِ نَامَ عَلَى شِقِّهِ الأَيْمَن ، ثُمَّ قَالَ : (( اللَّهُمَّ أسْلَمْتُ نفسي إلَيْكَ ، وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إلَيْكَ ، وَفَوَّضْتُ أمْرِي إلَيْكَ ، وَألْجَأتُ ظَهْرِي إلَيْك ، رَغْبَةً وَرَهْبَةً إلَيْكَ ، لاَ مَلْجَأ وَلاَ مَنْجا مِنْكَ إِلاَّ إلَيكَ ، آمَنْتُ بكِتَابِكَ الَّذِي أنْزَلْتَ ، وَنَبِيِّكَ الَّذِي أرْسَلْتَ )) رواه البخاري بهذا اللفظ في كتاب الأدب من صحيحه .
Amesema Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapoyaendea malazi yake akilala kwa ubavu wake wa kulia, kisha akisema:
للَّهُمَّ أسْلَمْتُ نفسي إلَيْكَ ، وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إلَيْكَ ، وَفَوَّضْتُ أمْرِي إلَيْكَ ، وَألْجَأتُ ظَهْرِي إلَيْك ، رَغْبَةً وَرَهْبَةً إلَيْكَ ، لاَ مَلْجَأ وَلاَ مَنْجا مِنْكَ إِلاَّ إلَيكَ ، آمَنْتُ بكِتَابِكَ الَّذِي أنْزَلْتَ ، وَنَبِيِّكَ الَّذِي أرْسَلْتَ
"Allaahumma Aslamtu nafsiy Ilayka wawajahtu Wajhiy Ilayka wa Fawwadhtu Amriy Ilayka wa Alja'tu Dhahri Ilayka Raghbatan wa Rahbatan Ilayka laa Malja' wala Manjaa illaa Ilayka Aamantu Bikitaabikal Ladhiy Anzalta wa Bikitaabikal Ladhiy Anzalta wa Nabiyyikal Ladhiy Arsalta - Ee Rabb wangu! Hakika nimeikabidhi nafsi yangu Kwako na nikauelekeza uso wangu Kwako. Na jambo langu nimeliegemeza Kwako. Hali ya kupenda na kuhofu Kwako. Hakuna pa kukimbilia wala pa kusalimika na Wewe isipokuwa Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako ambacho Umekiteremsha na Nabiy Wako ambaye Umemtuma." [Al-Bukhaariy kwa tamshi hili]
Hadiyth – 2
وعن البَراءِ بن عازِبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أتَيْتَ مَضْجَعَكَ فَتَوَضَّأ وُضُوءكَ لِلْصَّلاَةِ ، ثُمَّ اضْطَجِعْ عَلَى شِقِّكَ الأَيْمَن ، وَقُلْ ...)) وذَكَرَ نَحْوَهُ ، وفيه : (( وَاجْعَلْهُنَّ آخِرَ مَا تَقُولُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Utakapoyaendea malazi yako tawadha kama unavyotawadha kwa ajili ya Swalaah. Kisha jilaze juu ya ubavu wako wa kulia, na sema:
للَّهُمَّ أسْلَمْتُ نفسي إلَيْكَ ، وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إلَيْكَ ، وَفَوَّضْتُ أمْرِي إلَيْكَ ، وَألْجَأتُ ظَهْرِي إلَيْك ، رَغْبَةً وَرَهْبَةً إلَيْكَ ، لاَ مَلْجَأ وَلاَ مَنْجا مِنْكَ إِلاَّ إلَيكَ ، آمَنْتُ بكِتَابِكَ الَّذِي أنْزَلْتَ ، وَنَبِيِّكَ الَّذِي أرْسَلْتَ
"Allaahumma Aslamtu nafsiy Ilayka wawajahtu Wajhiy Ilayka wa Fawwadhtu Amriy Ilayka wa Alja'tu Dhahri Ilayka Raghbatan wa Rahbatan Ilayka laa Malja' wala Manjaa illaa Ilayka Aamantu Bikitaabikal Ladhiy Anzalta wa Bikitaabikal Ladhiy Anzalta wa Nabiyyikal Ladhiy Arsalta - Ee Rabb wangu! Hakika nimeikabidhi nafsi yangu Kwako na nikauelekeza uso wangu Kwako. Na jambo langu nimeliegemeza Kwako. Hali ya kupenda na kuhofu Kwako. Hakuna pa kukimbilia wala pa kusalimika na Wewe isipokuwa Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako ambacho Umekiteremsha na Nabiy Wako ambaye Umemtuma." Na akasema: "Na uyajaaliye haya ni maneno ya mwisho utakayoyasema." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي مِنَ اللَّيْلِ إحْدَى عَشرَةَ رَكْعَةً ، فَإذا طَلَعَ الفَجْرُ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ ، ثُمَّ اضْطَجَعَ عَلَى شِقِّهِ الأَيْمَن حَتَّى يَجيءَ الْمُؤَذِّنُ فَيُؤْذِنَهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali rakaa kumi na moja za usiku, lakini pindi inapoingia Alfajiri alikuwa akiswali rakaa mbili hafifu (fupi), kisha akijilaza kwa ubavu wake wa kulia mpaka aje muadhini amuarifu ya kwamba watu wamejumuika (kwa ajili ya Swalaah)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن حُذَيْفَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا أخَذَ مَضْجَعَهُ مِنَ اللَّيْلِ وَضَعَ يَدَهُ تَحْتَ خَدِّهِ ، ثُمَّ يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ بِاسْمِكَ أمُوتُ وَأحْيَا )) وَإِذَا اسْتَيْقَظ قَالَ : (( الْحَمْدُ للهِ الَّذِي أحْيَانَا بَعْدَمَا أمَاتَنَا وَإِلَيْهِ النُشُورُ )) رواه البخاري .
Na amesema Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapoelekea kwa malazi yake usiku akiweka mkono wake chini ya shavu lake, kisha akisema: "Allaahumma Biismika Amuutu wa Ahyaa - Ee Rabb wangu! Kwa jina Lako nina kufa na kupata uhai." Na anapoamka alikuwa akisema: "Alhamdu Lillaahi ladhiy Ahyaana Ba'damaa Amaatana wa Ilayhi Nushuwr - Sifa njema ni za Allaah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha, ni Kwake tu ufufuo (marudio)." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 5
وعن يَعيشَ بن طِخْفَةَ الغِفَارِيِّ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ أَبي : بينما أَنَا مُضْطَجِعٌ في الْمَسْجِدِ عَلَى بَطْنِي إِذَا رَجُلٌ يُحَرِّكُنِي برجلِهِ ، فَقَالَ : (( إنَّ هذِهِ ضجْعَةٌ يُبْغِضُهَا اللهُ )) ، قَالَ : فَنظَرْتُ ، فَإذَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم . رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Ya'iysh bin Twikhfah Al-Ghifariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba aliniambia baba yangu: Nilipokuwa nimejilaza katika Msikiti juu ya tumbo langu mara nikahisi mtu ananitingisha kwa mguu wake, akisema: "Hakika ulalaji huu Allaah haupendi." Akasema: "Nikamuangalia na kumuona kuwa ni Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]
Hadiyth – 6
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ قَعَدَ مَقْعَدَاً لَمْ يَذْكُرِ الله تَعَالَى فِيهِ ، كَانَتْ عَلَيْهِ مِنَ اللهِ تَعَالَى تِرَةٌ ، وَمَنِ اضْطَجَعَ مَضجَعاً لاَ يَذْكُرُ اللهَ تَعَالَى فِيهِ ، كَانَتْ عَلَيْهِ مِنَ اللهِ تِرَةٌ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ حسن .
Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote anayekaa kikao bila ya kumtaja Allaah Ta'aalaa ndani yake, atakuwa na upungufu mbele ya Allaah. Na yeyote anayejilaza katika malazi yake bila ya kumtaja Allaah Ta'aalaa ndani yake, atakuwa na upungufu mbele ya Allaah Ta'aalaa." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]