04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ndoto na Yanayohusiana Nayo
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الرؤيا وَمَا يتعلق بها
04-Mlango Wa Ndoto na Yanayohusiana Nayo
قَالَ الله تَعَالَى:
وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ﴿٢٣﴾
Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni kulala kwenu usiku na mchana. [Ar-Ruwm: 23]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( لَمْ يَبْقَ مِنَ النُّبوَّةِ إِلاَّ المُبَشِّرَاتِ )) قالوا : وَمَا المُبَشِّرَاتُ ؟ قَالَ : (( الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliyesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna ishara ya Unabiy iliyobakia isipokuwa bishara njema (Mubashshiraat)." Wakasema: "Bishara njema ni nini?" Akasema: "Ndoto ya kweli." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا اقْتَرَبَ الزَّمَانُ لَمْ تَكَدْ رُؤيَا المُؤْمِنِ تَكْذِبُ ، وَرُؤْيَا الْمُؤْمِنِ جُزْءٌ مِنْ سِتَّةٍ وَأرْبَعِينَ جُزْءاً مِنَ النُّبُوَّةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية : (( أصْدَقُكُمْ رُؤْيَا ، أصْدَقُكُمْ حَدِيثاً )) .
Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Zama zinapokaribia (za kufufuliwa) ndoto ya Muumini haitaongopa, na ndoto ya Muumini ni sehemu moja ya sehemu arubaini na sita ya Unabiy." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Na katika riwaaya nyingine: "Ndoto za kweli ni kwa wale miongoni mwenu walio wakweli katika mazungumzo."
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ رَآنِي في المَنَامِ فَسَيَرَانِي في اليَقَظَةِ – أَوْ كَأنَّما رَآنِي في اليَقَظَةِ – لاَ يَتَمَثَّلُ الشَّيْطَانُ بِي )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aliyeniona usingizini basi ataniona akiwa macho (Aakhera) au kama kwamba ameniona akiwa macho, na shetani hajifananisha na mimi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي سعيدٍ الخدرِيِّ رضي الله عنه : أنَّه سَمِعَ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إِذَا رَأى أحَدُكُمْ رُؤيَا يُحِبُّهَا ، فَإنَّمَا هِيَ مِنَ اللهِ تَعَالَى ، فَلْيَحْمَدِ اللهَ عَلَيْهَا ، وَلْيُحَدِّثْ بِهَا – وفي رواية : فَلاَ يُحَدِّثْ بِهَا إِلاَّ مَنْ يُحِبُّ – وَإِذَا رَأَى غَيْرَ ذَلِكَ مِمَّا يَكْرَهُ ، فإنَّمَا هِيَ مِنَ الشَّيْطَانِ ، فَلْيَسْتَعِذْ مِنْ شَرِّهَا ، وَلاَ يَذْكُرْهَا لأَحَدٍ ؛ فَإنَّهَا لا تَضُرُّهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Anapoona mmoja wenu ndoto nzuri, hakika hiyo ni (baraka) kutoka kwa Allaah Ta'aalaa, hivyo anatakiwa amsifu na amshukuru Allaah na awahadithie wengine.
Na katika riwaayah nyengine: Asiwahadithie isipokuwa wale anaowapenda tu. Na anapoona ndoto kinyume na hivyo (ndoto mabaya), hakika hiyo inatokana na shetani hivyo ajilinde kwa Allaah na shari ya ndito hiyo na wala asimueleze yeyote. Kama atafanya hivyo haita mdhuru." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي قَتَادَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ – وفي رواية : الرُّؤْيَا الحَسَنَةُ – مِنَ اللهِ ، وَالحُلُمُ مِنَ الشَّيْطَانِ ، فَمَنْ رَأى شَيْئاً يَكْرَهُهُ فَلْيَنْفُثْ عَن شِمَالِهِ ثَلاَثاً ، وَلْيَتَعَوَّذْ مِنَ الشَّيْطَانِ ؛ فإنَّهَا لا تَضُرُّهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ndoto njema -
Na katika riwaayah nyengine: Ndoto nzuri inatoka kwa Allaah, na ndoto mbaya, inatoka kwa shetani, hivyo anapoota mmoja wenu ndoto asiyoipenda basi anapoamka, ateme, kushotoni mwake mara tatu. Na ajilinde kwa Allaah kutokana na shetani, kama atafanya hivyo haita mdhuru." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 6
وعن جابر رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا رَأى أحَدُكُمْ الرُّؤْيَا يَكْرَهُهَا ، فَلْيَبْصُقْ عَنْ يَسَارِهِ ثَلاثَاً ، وَلْيَسْتَعِذْ بِاللهِ مِنَ الشَّيْطَانِ ثَلاَثاً ، وَلْيَتَحَوَّل عَنْ جَنْبِهِ الَّذِي كَانَ عَلَيْهِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Anapoona mmoja wenu ndoto anayoichukia, ateme (kwa kupeleka mdomo bila kutokwa na mate) kushotoni mwake mara tatu. Na atake ulinzi kutoka kwa Allaah dhidi ya shetani mara tatu na ageuke upande mwingine katika malazi yake." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن أَبي الأسقع واثِلةَ بن الأسقعِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ مِنْ أعْظَمِ الفِرَى أنْ يَدَّعِيَ الرَّجُلُ إِلَى غَيرِ أبِيهِ ، أَوْ يُرِي عَيْنَهُ مَا لَمْ تَرَ ، أَوْ يَقُولَ عَلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم مَا لَمْ يَقُلْ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abil Asqa'i Waathilah bin al-Asqa'i (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika miongoni mwa uwongo mkubwa ni mtu kudai kwa baba asiyekuwa wake, au kudai kuwa ameona kitu (katika ndoto) kwa macho yake lakini hajaona, au anamsingizia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema jambo ambalo hakusema." [Al-Bukhaariy]