01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutoleana Salamu na Maamrisho ya Kutoa Salamu
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل السلام والأمر بإفشائه
01-Mlango Wa Kutoleana Salamu na Maamrisho ya Kutoa Salamu
قَالَ الله تَعَالَى:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَىٰ أَهْلِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٢٧﴾
Enyi walioamini! Msiingie nyumba zisizokuwa nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salamu wenyewe. Hivyo ni bora kwenu ili mpate kukumbuka. [An-Nuwr: 27]
فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً ۚ ﴿٦١﴾
Mtakapoingia majumbani toleaneni salaam; maamkizi kutoka kwa Allaah, yenye Baraka, mazuri. [An-Nuwr: 61]
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ ﴿٨٦﴾
Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo. [An-Nisaa: 86]
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ﴿٢٤﴾ إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٢٥﴾
Je, imekufikia hadithi ya wageni wahishimiwao wa Ibraahiym? Walipoingia kwake wakasema: Salaam! Akasema: Salaam watu wasiotambulikana. [Adh-Dhaariyaat: 24-25]
Hadiyth – 1
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رجلاً سأل رسول الله صلى الله عليه وسلم : أيُّ الإسْلاَمِ خَيْرٌ ؟ قَالَ : (( تُطْعِمُ الطَّعَامَ ، وَتَقْرَأُ السَّلاَمَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba kuna mtu mmoja aliyemuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni Uislamu gani ulio bora?" Akasema: "Kulisha watu chakula na kuwatolea salamu unaowajua na usiowajua." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَمَّا خَلَقَ اللهُ آدَمَ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : اذْهَبْ فَسَلِّمْ عَلَى أُولئِكَ – نَفَرٍ مِنَ المَلاَئِكَةِ جُلُوس – فَاسْتَمِعْ مَا يُحَيُّونَكَ ؛ فَإنَّهَا تَحِيَّتُكَ وَتَحِيَّةُ ذُرِّيتِكَ . فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، فقالوا : السَّلاَمُ عَلَيْكَ وَرَحْمَةُ اللهِ ، فَزَادُوهُ : وَرَحْمَةُ اللهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa alipomuumba Aadam alimwambia: 'Nenda ukawatolee salamu wale Malaaikah waliokaa na kisha usikilize majibu yao, kwani jibu watakalo toa ndio litakalokuwa jibu lako na la wazawa wako (kizazi chako).' Adam akasema: 'Assalaamu 'Alaykum - Amani iwe juu yenu.' Wakasema: 'Assalaamu 'Alayka Wa Rahmatullaah -Amani iwe juu yako na rehma ya Allaah.' Wakaongeza: 'Wa Rahmatullaah.' [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي عُمَارة البراءِ بن عازِبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : أمرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم بِسَبْعٍ : بِعِيَادَةِ المَرِيضِ ، وَاتِّبَاعِ الجَنَائِزِ ، وَتَشْمِيتِ العَاطِسِ ، وَنَصْرِ الضَّعيفِ ، وَعَوْنِ المَظْلُومِ ، وَإفْشَاءِ السَّلاَمِ ، وَإبْرَارِ المُقسِمِ . متفقٌ عَلَيْهِ ، هَذَا لفظ إحدى روايات البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Ummarah Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru kufanya mambo saba: "kumtembelea mgonjwa, kulisindikiza jeneza, kumuombea dua anapopiga chafya, kumnusuru dhaifu, kumsaidia aliyedhulumiwa, kueneza salamu na kutekeleza kiapo." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya riwaayah moja ya Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَدْخُلُوا الجَنَّةَ حَتَّى تُؤمِنُوا ، وَلاَ تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا ، أوَلاَ أدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ ؟ أفْشُوا السَّلاَمَ بَيْنَكُمْ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hamutaingia Peponi mpaka Muamini, na wala hamtaamini mpaka mpendane. Je, niwaonyesheni kitu ambacho lau mutakifanya mutapendana? Enezeni salamu baina yenu." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي يوسف عبد الله بن سلام رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( يَا أيُّهَا النَّاسُ ، أفْشُوا السَّلاَمَ ، وَأطْعِمُوا الطَّعَامَ ، وَصِلُوا الأرْحَامَ ، وَصَلُّوا والنَّاسُ نِيَامٌ ، تَدْخُلُوا الجَنَّةَ بِسَلاَم )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Yusuf 'Abdillaah bin Salaam (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Enyi watu! Toleaneni salamu na mulishe watu chakula na unganisheni kizazi na swalini wakati watu wamelala, mutaingia Peponi kwa salama na amani." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 6
وعن الطُّفَيْل بن أُبَيِّ بن كعبٍ : أنَّه كَانَ يأتي عبد الله بن عمر ، فيغدو مَعَهُ إِلَى السُّوقِ ، قَالَ : فإذَا غَدَوْنَا إِلَى السُّوقِ ، لَمْ يَمُرَّ عَبدُ الله عَلَى سَقَّاطٍ وَلاَ صَاحِبِ بَيْعَةٍ ، وَلاَ مِسْكِينٍ ، وَلاَ أحَدٍ إِلاَّ سَلَّمَ عَلَيْهِ ، قَالَ الطُّفَيْلُ : فَجِئْتُ عبد الله بنَ عُمَرَ يَوْماً، فَاسْتَتْبَعَنِي إِلَى السُّوقِ ، فَقُلْتُ لَهُ : مَا تَصْنَعُ بالسُّوقِ ، وَأنْتَ لا تَقِفُ عَلَى البَيْعِ ، وَلاَ تَسْأَلُ عَنِ السِّلَعِ ، وَلاَ تَسُومُ بِهَا ، وَلاَ تَجْلِسُ في مَجَالِسِ السُّوقِ ؟ وَأقُولُ : اجْلِسْ بِنَا هاهُنَا نَتَحَدَّث ، فَقَالَ : يَا أَبَا بَطْنٍ – وَكَانَ الطفَيْلُ ذَا بَطْنٍ – إنَّمَا نَغْدُو مِنْ أجْلِ السَّلاَمِ ، فنُسَلِّمُ عَلَى مَنْ لَقيْنَاهُ . رواه مالك في المُوطَّأ بإسنادٍ صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Twufayl bin Ubayy bin Ka'b anaeleza kwamba alikuwa akimzuru 'Abdillaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) asubuhi, ambaye alikuwa akimchukua sokoni. Twufayl anasema: :Tulipokuwa tukielekea sokoni, 'Abdillaah alikuwa hapiti kwa wachuuzi wadogo (wenye kuuza vitu duni), wala wafanya biashara wala masikini wala mtu mwingine yeyote isipokuwa alikuwa akiwasalimia." Akasema Twufayl: "Nilikuwa kwake siku moja kama kawaida yangu na akanitaka nimfuate sokoni. Nikamwambia: 'Utafanaya nini sokoni, kwani wewe huulizi bei ya vitu wala huuzi wala hukai katika vikazi vya sokoni? Tukae hapa ili tuzungumze'." Akasema: "Ee Abu Batwn (na alikuwa Twufayl mwenye tumbo kubwa)! Hakika sisi tunakwenda sokoni asubuhi kwa ajili ya kuwasalimia (tunaokutana nao)." [Maalik katika Al-Muwatwaa' yake kwa Isnaad Swahiyh]