04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kurudia Salamu kwa Yule Mnayekutana Naye Mara Nyingi kwa Ukaribu wa Kuingia Kisha Kutoka au Ukawatenganisha Wao Mti na Mfano wake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب إعادة السلام عَلَى من تكرر لقاؤه عَلَى قرب بأن دخل ثم خرج
ثُمَّ دخل في الحال ، أَو حال بينهما شجرة ونحوهما
04-Mlango Wa Kupendeza Kurudia Salamu kwa Yule Mnayekutana Naye Mara Nyingi kwa Ukaribu wa Kuingia Kisha Kutoka au Ukawatenganisha Wao Mti na Mfano wake
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه في حديثِ المسِيءِ صلاته : أنّه جَاءَ فَصَلَّى ، ثُمَّ جَاءَ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ السَّلاَمَ ، فَقَالَ : (( ارْجِعْ فَصَلِّ فَإنَّكَ لَمْ تُصَلِّ )) فَرَجَعَ فَصَلَّى ، ثُمَّ جَاءَ فَسَلَّمَ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ ثَلاثَ مَرَّاتٍ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuhusu yule mtu aliyekosea katika Swalaah yake: ya kwamba alikuja akaswali, kisha akaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumsalimia. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na kumwambia: "Rudi ukaswali, kwani wewe hujaswali." Yule mtu alirudi kuswali, kisha akaja na kumtolea salamu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka akafanya hilo mara tatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا لَقِيَ أَحَدُكُمْ أخَاهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ ، فَإنْ حَالَتْ بَيْنَهُمَا شَجَرَةٌ ، أَوْ جِدَارٌ ، أَوْ حَجَرٌ ، ثُمَّ لَقِيَهُ ، فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ )) رواه أَبُو داود .
Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokutana mmoja wenu na nduguye amsalimie. Baada ya hapo ikiwa watatenganishwa na mti au ukuta au jabali (jiwe), kisha wakakutana tena basi amsalimie tena." [Abu Daawuwd]