09-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kutoa Salamu Unapofika na Kuondoka Katika Kikazi au Kuwaacha Wakazi Wake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب السلام إِذَا قام من المجلس
وفارق جلساءه أَوْ جليسه
09-Mlango Wa Kupendeza Kutoa Salamu Unapofika na Kuondoka Katika Kikazi au Kuwaacha Wakazi Wake
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا انْتَهى أَحَدُكُمْ إِلَى المَجْلِسِ فَلْيُسَلِّمْ ، فَإذَا أرَادَ أنْ يَقُومَ فَلْيُسَلِّمْ ، فَلَيْسَتِ الأُولَى بِأحَقّ مِنَ الآخِرَةِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapofika mmoja wenu katika kikazi atoe salamu na akitaka kuondoka pia atoe salamu. Hiyo ni kwa sababu salamu ya kwanza si bora kuliko ya mwisho." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]