01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mapenzi Yake: Kwa Swahaba Na Ummah Wake Ambao Hata Hajakutana Nao
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
01-Mapenzi Yake: Kwa Swahaba Na Ummah Wake Ambao Hata Hajakutana Nao
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَتَى الْمَقْبُرَةَ فَقَالَ " السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ بِكُمْ لاَحِقُونَ وَدِدْتُ أَنَّا قَدْ رَأَيْنَا إِخْوَانَنَا " . قَالُوا أَوَلَسْنَا إِخْوَانَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ " أَنْتُمْ أَصْحَابِي وَإِخْوَانُنَا الَّذِينَ لَمْ يَأْتُوا بَعْدُ " . فَقَالُوا كَيْفَ تَعْرِفُ مَنْ لَمْ يَأْتِ بَعْدُ مِنْ أُمَّتِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَقَالَ " أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّ رَجُلاً لَهُ خَيْلٌ غُرٌّ مُحَجَّلَةٌ بَيْنَ ظَهْرَىْ خَيْلٍ دُهْمٍ بُهْمٍ أَلاَ يَعْرِفُ خَيْلَهُ " . قَالُوا بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ . قَالَ " فَإِنَّهُمْ يَأْتُونَ غُرًّا مُحَجَّلِينَ مِنَ الْوُضُوءِ وَأَنَا فَرَطُهُمْ عَلَى الْحَوْضِ أَلاَ لَيُذَادَنَّ رِجَالٌ عَنْ حَوْضِي كَمَا يُذَادُ الْبَعِيرُ الضَّالُّ أُنَادِيهِمْ أَلاَ هَلُمَّ . فَيُقَالُ إِنَّهُمْ قَدْ بَدَّلُوا بَعْدَكَ . فَأَقُولُ سُحْقًا سُحْقًا
Amesimulia Abuu Hurayarah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alifika makaburini akasema:
السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ بِكُمْ لاَحِقُونَ
Assalaamu ‘alaykum watu wa nyumba za Waumini, nasi In Shaa Allaah tutakutana nanyi.
Natamani kuwaona ndugu zangu.” Wakasema (waliosikia): Je, kwani sisi sio nduguzo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Ninyi ni Swahaba zangu na ndugu zetu ni wale ambao, hadi sasa, hawajaja ulimwenguni. Wakasema: Ni vipi utamtambua yule ambaye bado hajakuja katika Ummah wako ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Niambieni, lau kama mtu ana farasi wenye alama usoni na miguuni wakawa baina ya farasi weusi wasio na mabaka, je hawezi kuwatambua farasi wake?” Wakasema: Ndio, atawatambua ee Rasuli wa Allaah. Akasema: “Basi wao watakuja nailhali wana nuru nyusoni, miguuni na mikononi kutokana na wudhuu. Na mimi ndiye nitakayewatangulia kwenye Al-Hawdh (Hodhi) Basi jueni kwa yakini kwamba watu watazuiliwa na kufukuzwa wasije kwenye Hawdh langu kama wanavyozuiliwa ngamia wasio na mchunga. Nitawaita: Haya njooni! Patasemwa: “Hakika hao walibadili baada yako.” Nitawaambia: Poteleeni mbali kabisa!” [Muslim]