17-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hakika Allaah Ameandika Ihsani Katika Kila Kitu
Hadiyth Ya 17
إنَّ اللهَ كَتَبَ الإِحْسانَ على كلِّ شَيءٍ
Hakika Allaah Ameandika Ihsani Katika Kila Kitu
عَنْ أبي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رضي اللهُ عنه، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ اللهَ كَتَبَ الإِحْسانَ على كلِّ شَيءٍ، فإذا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، ولْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ ولْيُرِحْ ذَبيحَتَهُ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ya’laa Shaddaad bin Aws (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah Ameandika ihsaan katika kila kitu. Kwa hiyo mnapoua (mnyama), ueni vizuri na unapochinja chinjeni vizuri. Basi kila mmoja wenu anoe kisu chake barabara (anapotaka kuchinja) na amuondoshee mateso mnyama anayemchinja.” [Muslim]