02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Duaa za Kumuombea Mgonjwa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يُدعى به للمريض
02-Mlango Wa Duaa za Kumuombea Mgonjwa
Hadiyth – 1
عن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، كَانَ إِذَا اشْتَكى الإنْسَانُ الشَّيْءَ مِنْهُ ، أَوْ كَانَتْ بِهِ قَرْحَةٌ أَوْ جُرْحٌ ، قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بِأُصْبُعِهِ هكَذا – وَوَضَعَ سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَة الرَّاوي سَبَّابَتَهُ بِالأَرْضِ ثُمَّ رَفَعَها – وقال : (( بِسمِ اللهِ ، تُرْبَةُ أرْضِنَا ، بِرِيقَةِ بَعْضِنَا ، يُشْفَى بِهِ سَقِيمُنَا ، بإذْنِ رَبِّنَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anaposhtakiwa na mtu kwa maumivu asikiayo au jipu au jeraha, alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya hivi kwa kidole chake cha shahada, na akaweka Sufyaan bin 'Uyaynah, mpokezi wa Hadiyth hii kidole chake cha shahada kwenye ardhi, kisha anakinyanyua na akasema: "BismiLLaah Turbatu Ardhina Biriiqati Ba'dhina Yushfaa bihi Saqiimuna Biidhni Rabbina - Kwa jina la Allaah, huu ni mchanga wa ardhiyetu, kwa mate ya baadhi yetu, anaponywa mgonjwa wetu kwa idhini ya Rabb wetu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
عن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَعُودُ بَعْضَ أهْلِهِ يَمْسَحُ بِيدِهِ اليُمْنَى ، ويقولُ : (( اللَّهُمَّ رَبَّ النَّاسِ ، أذْهِب البَأسَ ، اشْفِ أنْتَ الشَّافِي لاَ شِفَاءَ إِلاَّ شِفاؤكَ ، شِفَاءً لاَ يُغَادِرُ سَقماً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akimtembelea mtu wa familia yake mgonjwa. Alikuwa akimgusa kwa mkono wake wa kulia na kusema: "Allaahumma Rabban Naas Adhhibul Ba'sa washfi Antash Shaafi Laa Shifaa' illaa Shifaa'uka Laa Yughaadiru Saqama - Ee Rabb wangu! Rabb wa watu, ondoa ubaya na ponyesha, Wewe Ndiye Mponyeshaji, hakuna ponyo isipokuwa ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنسٍ رضي الله عنه أنه قَالَ لِثابِتٍ رحمه اللهُ : ألاَ أرْقِيكَ بِرُقْيَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟ قَالَ : بَلَى ، قَالَ : (( اللَّهُمَّ رَبَّ النَّاسِ ، مُذْهِبَ البَأسِ ، اشْفِ أنْتَ الشَّافِي ، لاَ شَافِيَ إِلاَّ أنْتَ ، شِفَاءً لاَ يُغَادِرُ سَقماً )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) Alimwambia Thaabit: "Nikufanyie Ruqyah ya Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Ee Rabb wangu! Rabb wa watu, Mwenye kuondoa ubaya, ponyesha, Wewe ni Mponyaji, hakuna Mponyaji isipokuwa Wewe, ponyo lisiloacha ugonjwa." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن سعدِ بن أَبي وقاصٍ رضي الله عنه ، قَالَ : عَادَنِي رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( اللَّهُمَّ اشْفِ سَعْداً ، اللَّهُمَّ اشْفِ سَعْداً ، اللَّهُمَّ اشْفِ سَعْداً )) رواه مسلم .
Amesema Sa'd bin Abu Waqqaas: Alinitembelea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuombea: Ee Rabb wangu! ponyeshe Sa'd. Ee Rabb wangu! Mponyesha Sa'd. Ee Rabb wangu! Mponyeshe Sa'd." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي عبدِ الله عثمان بنِ أَبي العاصِ رضي الله عنه : أنّه شَكَا إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم وَجَعاً ، يَجِدُهُ في جَسَدِهِ ، فَقَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ضَعْ يَدَكَ عَلَى الَّذِي يَألَم مِنْ جَسَدِكَ وَقُلْ : بسم اللهِ ثَلاثاً ، وَقُلْ سَبْعَ مَرَّاتٍ : أعُوذُ بِعِزَّةِ الله وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أجِدُ وَأُحَاذِرُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaah 'Uthmaan bin Abil 'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alimshitakia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa maumivu anayoyasikia katika mwili wake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Weka mkono wako katika sehemu inayokuuma kwenye mwili wako kisha useme: 'BismiLLaah (Thalaath - mara tatu) na useme mara saba: A'uudhu Bi'izzati Llaahi wa Qudratihi min sharri maa Ajidu wa Uhaadhir (Najilinda kwa Nguvu za Allaah na Kudura Yake kwa shari iliyo ninayoiona na ambayo ninaiogopa." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ عَادَ مَرِيضاً لَمْ يَحْضُرْهُ أجَلُهُ ، فقالَ عِنْدَهُ سَبْعَ مَرَّاتٍ : أسْأَلُ اللهَ العَظيمَ ، رَبَّ العَرْشِ العَظيمِ ، أنْ يَشْفِيَكَ ، إِلاَّ عَافَاهُ اللهُ مِنْ ذَلِكَ المَرَضِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) ، وقال الحاكم : (( حديث صحيح عَلَى شرط البخاري )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumtembelea mgonjwa ambaye ajali yake haijafika na akasema mbele yake mara saba: 'As'alu Llaahal 'Adhiym Rabbal 'Arshil 'Adhiym an Yashfiyaka - Namuomba Allaah Al-'Adhiym, Rabb wa 'Arshi (Kiti cha enzi) Al-'Adhiym akupony)', isipokuwa Allaah hmuondolea maradhi hayo." [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan. Na akasema Al-Haakim: "Hii ni Hadiyth Swahiyh kwa sharti za Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 7
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَى أعْرَابِيٍّ يَعُودُهُ ، وَكَانَ إِذَا دَخَلَ عَلَى مَنْ يَعُودُهُ ، قَالَ : (( لاَ بَأسَ ؛ طَهُورٌ إنْ شَاءَ اللهُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea Mbedui mgonjwa. Na alikuwa akimtembelea mgonjwa husema: "Laa ba's Twahuur in shaa Allaah (Hakuna ubaya, ugonjwa wako ni tohara yako Allaah Akitaka)." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 8
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أن جِبريلَ أتَى النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا مُحَمَّدُ ، اشْتَكَيْتَ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) قَالَ : بِسْمِ الله أرْقِيكَ ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِدٍ ، اللهُ يَشْفِيكَ ، بِسمِ اللهِ أُرقِيكَ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Jibriyl alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Ee Muhammad! Unaumwa?" Akasema: "Ndio." Akasema: "BismiLlaah Arqiyk, min kuli Shay'in Yu'dhiyk, min kuli nafsin aw 'ayni haasid, Allaahu Yashfiyk, BismiLlaah Arqiyk (Kwa jina la Allaah nanakutibu kila kinacho kuudhi, kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasid. Allaah akuponye, kwa jina la Allaah ninakutibu)." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن أَبي سعيد الخدري وأبي هريرة رضي الله عنهما : أنَّهُمَا شَهِدَا عَلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، أنّه قَالَ : (( مَنْ قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَاللهُ أكْبَرُ ، صَدَّقَهُ رَبُّهُ ، فَقَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ أنَا وأنَا أكْبَرُ . وَإِذَا قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، قَالَ : يقول : لاَ إلهَ إلاَّ أنَا وَحْدِي لا شَريكَ لِي . وَإِذَا قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ، قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ أنَا لِيَ المُلْكُ وَلِيَ الحَمْدُ . وَإِذَا قَالَ : لاَ إله إِلاَّ اللهُ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ ، قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ أنَا وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بي )) وَكَانَ يقُولُ : (( مَنْ قَالَهَا في مَرَضِهِ ثُمَّ مَاتَ لَمْ تَطْعَمْهُ النَّارُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) na Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) wao wanashuhudia kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusema: Hapana Mola ila Allaah, Allaah ni Mkuu.' Allaah anamjibu Anasema: "Hapana Mola ila Mimi, na Mimi ni Mkuu.' Na anaposema: 'Hapana Mola ila Allaah, Peke yake hana mshirika.' Amesema: Anasema: 'Hapana Mola ila Mimi, Peke Yangu sina mshirika.' Na anaposema: 'Hapana Mola ila Allaah, ni Wake Ufalme, ni Kwake kuhimidiwa.' Amesema: 'Hapana Mola ila Mimi, Mimi ni Mfalme na Mimi ni mwenye kusifiwa.' Na anaposema: 'Hapana Mola ila Allaah, hakuna hila wala nguvu ila kwa Allaah.' Amesema: 'Hapana Mola ila Mimi, wala hila wala nguvu isipokuwa Kwangu.' Na Nabiy alikuwa akisema: Mwenye kuyasema katika maradhi yake kisha akafa Moto hautamla." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]