10-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ruhusa ya Kulia Unapofiwa Bila Kuomboleza
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب جواز البكاء عَلَى الميت بغير ندب وَلاَ نياحة
10-Mlango Wa Ruhusa ya Kulia Unapofiwa Bila Kuomboleza
أمَّا النِّيَاحَةُ فَحَرَامٌ وَسَيَأتِي فِيهَا بَابٌ فِي كِتابِ النَّهْيِ ، إنْ شَاءَ اللهُ تَعَالَى . وَأمَّا البُكَاءُ فَجَاءتْ أحَادِيثُ بِالنَّهْيِ عَنْهُ ، وَأنَّ المَيِّتَ يُعَذَّبُ بِبُكَاءِ أهْلِهِ ، وَهِيَ مُتَأَوَّلَةٌ ومَحْمُولَةٌ عَلَى مَنْ أوْصَى بِهِ ، وَالنَّهْيُ إنَّمَا هُوَ عَن البُكَاءِ الَّذِي فِيهِ نَدْبٌ ، أَوْ نِيَاحَةٌ ، والدَّليلُ عَلَى جَوَازِ البُكَاءِ بِغَيْرِ نَدْبٍ وَلاَ نِياحَةٍ أحَادِيثُ كَثِيرَةٌ ، مِنْهَا :
Ama kuomboleza ni haramu kabisa na kutakuja mlango kuhusu hilo katika kitabu cha makatazo, Allaah akipenda. Na ama kulia zipo Hadiyth nyingi zinazokataza, na hakika ni kuwa maiti anaadhibiwa kwa kulia watu wake. Katazo ni kule kulia pamoja na kujipiga na kuomboleza. Na dalili za kujuzu kulia bila kujipiga au kuomboleza ni nyingi, miongoni mwazo:
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم عاد سَعْدَ بْنَ عُبَادَةَ، وَمَعَهُ عَبدُ الرَّحْمانِ بْنُ عَوفٍ، وَسَعدُ بْنُ أَبي وَقَّاصٍ، وَعَبْدُ اللهِ بْنُ مَسْعُودٍ رضي الله عنه، فَبَكَى رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، فَلَمَّا رَأى القَوْمُ بُكَاءَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم بَكَوْا ، فَقَالَ : (( ألاَ تَسْمَعُونَ ؟ إنَّ الله لاَ يُعَذِّبُ بِدَمْعِ العَينِ ، وَلاَ بِحُزنِ القَلبِ ، وَلَكِنْ يُعَذِّبُ بِهذَا أَوْ يَرْحَمُ )) وَأشَارَ إِلَى لِسَانِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea Sa'd bin 'Ubadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akiwa pamoja na 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf na Sa'd bin Abi Waqqaas na 'Abdillaah bin Mas'uuwd (Radhwiya Allaah 'anhum) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alilia kuiona hali yake na watu walipomuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akilia nao pia wakalia. Akasema: "Sikilizeni! Hakika Allaah humuadhibu kwa kutokwa na machozi wala kwa huzuni ya moyo, lakini anaadhibu kwa hili au anawahurumia." Na hapo akaashiria mdomo wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أُسَامَة بن زَيدٍ رضي اللهُ عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم رُفِعَ إِلَيْهِ ابنُ ابْنَتِهِ وَهُوَ فِي المَوتِ ، فَفَاضَتْ عَيْنَا رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ لَهُ سَعدٌ : مَا هَذَا يَا رسولَ الله ؟! قَالَ : (( هذِهِ رَحْمَةٌ جَعَلَهَا اللهُ تَعَالَى في قُلُوبِ عِبَادِهِ ، وَإنَّمَا يَرْحَمُ اللهُ مِنْ عِبَادِهِ الرُّحَمَاءَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Usamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), alinyanyuliwa kwake mtoto wa binti yake akiwa katika hali ya mauti. Nabiy alibubijika machozi. Sa'd akasema: "Hii ni rehma Allaah ameiweka ndani ya nyoyo za waja Wake." Hakika Allaah anahurumia waja Wake wenye huruma." [Ahmad, Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنسٍ رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَى ابْنِهِ إبْرَاهيمَ رضي اللهُ عنه ، وَهُوَ يَجُودُ بِنَفسِهِ ، فَجَعَلَتْ عَيْنَا رسولِ الله صلى الله عليه وسلم تَذْرِفَان . فَقَالَ لَهُ عبدُ الرحمانِ بن عَوف : وأنت يَا رسولَ الله ؟! فَقَالَ : (( يَا ابْنَ عَوْفٍ إنَّهَا رَحْمَةٌ )) ثُمَّ أتْبَعَهَا بأُخْرَى ، فَقَالَ : (( إنَّ العَيْنَ تَدْمَعُ والقَلب يَحْزنُ ، وَلاَ نَقُولُ إِلاَّ مَا يُرْضِي رَبَّنَا ، وَإنَّا لِفِرَاقِكَ يَا إبرَاهِيمُ لَمَحزُونُونَ )) رواه البخاري ، وروى مسلم بعضه . والأحاديث في الباب كثيرة في الصحيح مشهورة ، والله أعلم .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa mtoto wake Ibraahim akiwa katika hali ya kukata roho. Hapo macho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yakadondokwa na machozi. Akamwambia 'Abdir-Rahmaan bin 'Awf: "Hata wewe, ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ee Ibn 'Awf! Hakika hiyo ni huruma." Baada ya hapo akaanza kulia tena na akasema: "Hakika jicho linatoa machozi na moyo unahuzunika na hatusemi ila yanayomridhisha Rabb wetu, nasi kwa kufarikiana nawe Ibraahiym tumehuzunika." [Al-Bukhaariy, na Muslim amenukuu baadhi yake. Na Hadiyth katika mlango huu ni nyingi zilizo Swahiyh na mashuhuri. Na Allaah anajua zaidi].