13-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupenda Kuwa na Jamaa Kubwa Katika Swalaah ya Jeneza na Kuzifanya Safu Zake Tatu na Zaidi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب استحباب تكثير المصلين عَلَى الجنازة

وجعل صفوفهم ثلاثة فأكثر

13-Mlango Wa Kupenda Kuwa na Jamaa Kubwa Katika Swalaah ya Jeneza na Kuzifanya Safu Zake Tatu na Zaidi

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ مَيتٍ يُصَلِّي عَلَيْهِ أُمَّةٌ مِنَ المُسْلِمِينَ يَبْلُغُونَ مِئَةً كُلُّهُمْ يَشْفَعُونَ لَهُ إِلاَّ شُفِّعُوا فِيهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna maiti yeyote anayeswaliwa na kikundi cha Waislaamu wanaofika mia moja wote wanamuombea isipokuwa Allaah anakubali maombi yao." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ رَجُلٍ مُسْلِمٍ يَمُوتُ ، فَيقومُ عَلَى جَنَازَتِهِ أرْبَعُونَ رَجُلاً لاَ يُشْرِكُونَ بِاللهِ شَيْئاً ، إِلاَّ شَفَّعَهُمُ اللهُ فِيهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna mtu Muislaamu aliyefariki, wakasimama kwenye jeneza lake watu arubaini wasiomshirikisha Allaah na chochote isipokuwa Allaah humsamehe (maiti)." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن مرثدِ بن عبدِ الله اليَزَنِيِّ ، قَالَ : كَانَ مَالِكُ بن هُبَيْرَة رضي اللهُ عنه إِذَا صَلَّى عَلَى الجَنَازَةِ ، فَتَقَالَّ النَّاس عَلَيْهَا ، جَزَّأَهُمْ عَلَيْهَا ثَلاَثَةَ أجْزَاءٍ ، ثُمَّ قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ صَلَّى عَلَيْهِ ثَلاَثَةُ صُفُوفٍ فَقَدْ أوْجَبَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

imepokewa kutoka kwa Marthad bin 'Abdillaah Al-Yazaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alikuwa Maalik bin Hubayrah anaposwalia jeneza yenye watu kidogo anawagawa safu tatu, kisha anasema: "Mwenye kuswaliwa na safu tatu hakika imethibiti (yaani imewajibika kuingizwa Peponi)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

Share