19-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kumtolea Swadaqah Maiti na Kumuombea Dua
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الصدقة عن الميت والدعاء لَهُ
19-Mlango Wa Kumtolea Swadaqah Maiti na Kumuombea Dua
قَالَ الله تَعَالَى:
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ ﴿١٠﴾
Na wale waliokuja baada yao wanasema: Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan. [Al-Hashr: 10]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ رجلاً قَالَ للنبيِّ صلى الله عليه وسلم : إنَّ أُمِّي افْتُلِتَتْ نَفْسُهَا وَأُرَاهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ ، فَهَلْ لَهَا أجْرٌ إنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alisema mtu fulani alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mama yangu amekufa nadhani lau angesema angetoa sadaka. Je, anapata thawabu nikimtolea sadaka?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Ndiyo." [Al-Bukhaariy na muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا مَاتَ الإنْسَانُ انْقَطَعَ عَمَلُهُ إِلاَّ مِنْ ثَلاثٍ : صَدَقةٍ جَاريَةٍ ، أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ ، أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kwake Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokufa mwanadamu hukatika amali yake isipokuwa mambo matatu: Sadaka endelevu, au elimu yenye manufaa au mtoto mwema anamuombea dua." [Muslim]