01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kusafiri Siku ya Alkhaamis na Kupendeza Kuondoka Mwanzo wa Mchana
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب الخروج يوم الخميس ، واستحبابه أول النهار
01-Mlango Wa Kupendeza Kusafiri Siku ya Alkhaamis na Kupendeza Kuondoka Mwanzo wa Mchana
Hadiyth – 1
عن كعب بن مالك رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ في غَزْوَةِ تَبُوكَ يَوْمَ الخَمِيس ، وَكَانَ يُحِبُّ أنْ يَخْرُجَ يَوْمَ الْخَميسِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية في الصحيحين: لقَلَّمَا كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَخْرُجُ إِلاَّ في يَوْمِ الخَمِيسِ.
Imepokewa kutoka kwa Ka'ab bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka kwa ajili ya Vita vya Taabuk siku ya Alkhamisi. Na alikuwa akipenda kutoka siku ya Alkhamis." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]
Katika riwaayah iliyopo katika Swahiyh mbili: Ni mara chache sana Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoka isipokuwa siku ya Alkhamisi.
Hadiyth – 2
وعن صخر بن وَداعَةَ الغامِدِيِّ الصحابيِّ رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( اللَّهُمَّ بَارِكْ لأُمَّتِي في بُكُورِهَا )) وَكَانَ إِذَا بَعَثَ سَرِيَّةً أَوْ جَيْشَاً بَعَثَهُمْ مِنْ أوَّلِ النَّهَارِ . وَكَانَ صَخْرٌ تَاجِراً ، وَكَانَ يَبْعَثُ تِجَارَتَهُ أوَّلَ النَّهَار ، فَأَثْرَى وَكَثُرَ مَالُهُ . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Swahaba, Swakhr bin Wadaa'ah Al-Ghaamidy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Mola! Ubariki Ummah wangu katika kuwahi kwao." Na alikuwa anapotuma mwanzo wa mchana. Na Swakhr alikuwa ni mfanya biashara, naye alikuwa daima akituma biashara zake mwanzo wa mchana, hivyo biashara yake ikashamiri na mali yake kuongezeka." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]